Hapo juu watu wameuliza, Simba atamfunga nani?
Nawajibu, atamfunga Horoya, Vipers mara 2 na droo kwa Raja hukohuko kwao.
Wala haitakuwa maajabu ya dunia.
Mchezo na Raja pia ni makosa na yanarekebisheka vizuri tu.
Ni kweli kiuwezo mchezaji mmojammoja Raja wapi vizuri mno.
Lakini kumbukeni Simba ilifika pia langoni mwa Raja zaidi ya mara tatu.
Tatizo la Simba kama ilivyokuwa kwa hata ligi ya ndani ni kusubiri msitu wa walinzi.
Hata hivyo, hilo linarekebishika kwa zaidi ya asilimia 75 na kwa wachezaji hawahawa mnao waponda.
Enyi wachezaji kama mnasoma hii habari ifanyieni kazi. Ushindi upo.