FT | Simba SC 1-0 Stellenbosch FC | Nusu Fainali CAFCC | New Amaan Stadium | 20.4.2025

FT | Simba SC 1-0 Stellenbosch FC | Nusu Fainali CAFCC | New Amaan Stadium | 20.4.2025

Heri ya Pasaka babu Grahams

Endelea kuandaa kibunda wiki ijayo kinakutoka, biashara inaenda kuishia kwa Madiba.

Kwa leo, hongera.
Hivi tukifika fainali na kubeba hilo kombe si mtakufa kwa vihoro, maana mna stress kweli kwa kuhofia kwamba tutaifikia rekodi yenu na pengine kuivunja kabisa, hilo halina budi kutokea mpende msipende na msimu huu simba inamaliza na treble take this from me
 
Hua najiuliza kocha ni kua Kuna mambo hua anayaona ambayo hatuyaoni? Mtu anaomba sub unamkatalia ..
Fadlu ni Conservative Sana. Jinsi asivyopenda kufanya mabadiliko hadi inashangaza.

Kwa mfano Kwa Sasa Nouma ni Bora zaidi kuliko Mohamed Hussen ambaye nadhani anapangwa kimazoea tu.
 
Chonde kule south msiende kuwasha moto uwanjani tena,makolo uchawi upo kwenye damu
 

Attachments

  • VID-20250420-WA0002.mp4
    6 MB
Mechi za muhimu, mnapata nafasi kadhaa za kufunga magoli na mnashindwa kuzitumia!
 
Chonde kule south msiende kuwasha moto uwanjani tena,makolo uchawi upo kwenye damu
Kwa roho zenu za mkaa ndiyo maana meishia makundi.
Mlikuwa kwa waarabu Al Maesry, mkaangukia pua. Leo kapigwa Zanzibàr mnaenda South Africa.
Kwa ushauri tu Mwakakikundi, jiliwaze na ile mechi ya 5-1 mliyoifunga Simba.
 
Refa alishaweka kati
Hujaelewa.
Issue iko hivi.
Goli lilifungwa na Refa akasema ni goli mpira uwekwe kati na hakuna aliyekuwa akilalamika. Lakini uwepo wa VAR ukagundua kuna utata, refa akaambiwa subiri kwanza waamuzi wa VAR wanacheck, baada ya waamuzi wa VAR kucheck ikaonekana kuna utata huenda sio goli hivyo Refa atafakari upya maamuzi yake. Refa akaamua kwenda kucheck VAR yeye mwenyewe, na alipokuwa akicheck nasi kupitia runinga zetu tunaona alichokuwa anakifanya. Haya ndio tuliona.
1. Refa akajikita kucheck kama Kibu aliuingilia mpira ama la. (Mantiki ni kwamba tayari Refa alijiridhisha kuwa Kibu alikuwa kwenye Offside, issue ni je alihusika na mpira ama la)

2. Video zikaonyesha kwa hakika 100% ni kweli Kibu aliuingilia mpira japokuwa haioneshi kama Kibu aliugusa mpira.

3. Baada ya Refa kumaliza kucheck VAR, body language ilionekana bado hakuwa na maamuzi ya moja moja na akaongea na mwamuzi wa akiba aliyekuwepo pembeni yake ambaye alimpa ishara ya kumwambia aweke mpira kati tu maana lile ni goli!
 
Ni kweli lakini shida ya hawa wachezaji wa west Africa ni ubinafsi ili wajiuze kwenye timu zenye Mpunga mwingi. Ni mara nyingi Ahou ana huo utoto.
Jamaa siku hizi wanaitumia Afrika ya Mashariki hasa Simba na Yanga kama njia yao ya kupata mafanikio kimataifa.

Yaani wengi wanakuja hapa hata timu zao za Taifa hawaitwi ila wakifika hapa wanaitwa kwenye timu zao za Taifa.

Unakumbuka Pape Sakho. Mpaka akajulikana na Sadio Mane!
 
Mechi kali ya mkondo wa kwanza Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika inapigwa leo, ambapo Mnyama Simba SC anawakaribisha Stellenbosch FC kutoka Afrika Kusini, katika dimba la Amaan, Visiwani Zanzibar.

Mchezo huo utachezwa kuanzia saa 10:00 jioni.

Kaa karibu kwa Live updates

Asubuhi Zanzibar watu wameamka na baraka ya mvua kuelekea mtanange mkali jioni ya leo

Kutoka nje ya Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar mvua inaendelea kunyesha.

Baadhi ya mashabiki wa Simba wameanza shangwe mapema nje ya Uwanja wa New Amaan Complex kuelekea mchezo wa saa 10 wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini.

Namna mambo yalivyo muda huu New Amaan stadium Zenji kuelekea mbungi ya Jioni hii baina ya mnyama na msauzi.

Stellenbosch wako uwanjani kwa ajili ya ukaguzi wa sehemu ya kuchezea uwanjani.

Kikosi Simba SC kikiondoka kambini kwenda uwanjani.


Kikosi cha Simba Sports Club dhidi ya Stellenbosch FC, CAFCC

Kikosi cha Stellenbosch FC dhidi ya Simba Sports Club, CAFCC


Mechi imeanza: Simba SC 0-0 Stellenbosch FC

1' Stellenbosch FC wameanzisha mtanange
4' Kona - Simba wanapiga
8' Faulo - Stellenbosch FC wanapiga
10' Faulo - Stellenbosch FC wanapiga
12' Kona - Simba wanapiga
15' Faulo - Simba SC wanapiga
16' Kona - Simba wanapiga
17' Kapombe anakosa kutumia nafasi
18' Mechi imesimama - Masuluke (GK) anatibiwa
20' Mechi inaendelea, hakuna mbabe
21' Kona - Simba wanapiga
22' Ngoma anafanya madhambi
25' Faulo - Simba wanapiga
27' Camara anafanya save
30' Kona - Simba wanapiga
35' Kadi ya Njano - Enyinnaya

Dakika 4 zimeongezwa

45+2' Goooal - Ahoua

VAR - Goal Check

45+6' Maamuzi ya VAR - Goal

HALF TIME


Simba SC 1-0 Stellenbosch FC
⚽ J. Ahoua 45+2'

Kipindi cha pili kimeanza

45' Simba wanaanza mpira
48' Kichwa - Ahoua anapoteza nafasi
61' Mechi imesimama - Camara anatibiwa
73' Mapadiliko - Simba SC (Kibu Out-Mutale In, Zimbwe out-Nouma In)
80' Mabadiliko - Simba SC (Chamou out-Debora In)
84' Mabadili - SImba SS (Mukwala out-Ateba In)

Dakika 6 zimeongezwa

FULL TIME
HALF TIME


Simba SC 1-0 Stellenbosch FC
⚽ J. Ahoua 45+2'
Simba wanayo nafasi kufuzu kwenda finali. Lakini kuna kazi ya ziada ya kufanya kuipenya midblock na low block yenye utulivu mkubwa ya Stelenbosch!

Bila hivyo, Simba wameumaliza mwendo
 
Jamaa siku hizi wanaitumia Afrika ya Mashariki hasa Simba na Yanga kama njia yao ya kupata mafanikio kimataifa.

Yaani wengi wanakuja hapa hata timu zao za Taifa hawaitwi ila wakifika hapa wanaitwa kwenye timu zao za Taifa.

Unakumbuka Pape Sakho. Mpaka akajulikana na Sadio Mane!

Mchezaji kucheza Tanzania anarahisisha sana kazi ya wakala wake. Maana visibility ni 100%.

Vijana wetu sijui kama wanafanyia kazi hii fursa ya visibility, sijui mawakala wa wachezaji wenyeji kama wanatumia fursa ya visibility kuwauza vijana mbele huko...maana biashara ni matangazo, na matangazo ni kuonekana.
 
Back
Top Bottom