FT: Tanzania 0-2 Morocco Kufuzu Kombe la Dunia, Novemba 21, 2023

Vincenzo Jr

Platinum Member
Joined
Sep 23, 2020
Posts
24,262
Reaction score
58,728
Naam leo ndo leo majira ya saa 4 usiku kwa saa za afrika mashariki kutakuwa na mchezo kati ya Tanzania na Morocco

KUFUZU WORLD CUP: TANZANIA YAPOTEZA 2-0 DHIDI YA MOROCCO KWA MKAPA
Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imepoteza kwa magoli 2-0 licha ya kuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Mkapa ikicheza dhidi ya Morocco katika mchezo wa Kundi E Kuwania Kufuzu Kombe la Dunia 2026.

Magoli yamefungwa na Hakim Ziyech anayeitumika Galatasaray ya Uturuki na Lusajo Mwaikenda wa Azam FC aliyejifunga.

Matokeo mengine ya Kundi E, Niger imeifunga Zambia magoli 2-1, hivyo timu zote hizo zina pointi tatu kasoro Congo ambayo haina alama.
 
Wanasemaga too much is harmful, ndivyo ilivyo kwa ushiriki wa mama ktk michezo.

Mwanzoni ilikuwa nzuri, kwa kuonekana mama anapenda michezo na anatoa support.

Ila sasa hivi limekaa kisiasa zaidi, halivutii tena!
 
Back
Top Bottom