FT: Yanga 0-1 Azam | VPL | Benjamin Mkapa | April 25, 2021

FT: Yanga 0-1 Azam | VPL | Benjamin Mkapa | April 25, 2021

Poleni sana ndugu zangu, mjifunze mpira hauchezwi kwa maneno meng! Leo Usingizi mwororooooooooo huku wengine wamelala na viatu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Poleni sana ndugu zangu, mjifunze mpira hauchezwi kwa maneno meng! Leo Usingizi mwororooooooooo huku wengine wamelala na viatu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Shikalo kiwango kimeisha. Hii ni mechi ya pili mfululizo anafungwa goli nje ya 18! Yanga iangalie namna ya kutafuta mbadala wake.

Kuna magolikipa wengi sana wazawa, wa bei nafuu na wanao mzidi kiwango Farouq Shikalo kwa mbali. Naamini viongozi wanapitia humu. Fanyieni kqzi huu ushauri wangu.
Kwani Metacha ameenda wapi mkuu?
 
nawaona mnavyofurahia ushindi
1619004460113.jpg

Mwache Numbisa wangu asheherekee ushindi wa Azam

View attachment 1764195
 
Kwani Metacha ameenda wapi mkuu?
Hata sijui aisee! Maana hata Fei Toto ndiyo namuona leo. Shikalo ni majanga kwa mipira ya mbali na ile ya kona! Na hana kabisa timing nzuri ya kutokea mipira.

Msimu ujao ni bora tu timu ikasajili magolikipa wa ndani! Wako wengi tu wanaofanya vizuri kuliko huyu Shikalo. Kama timu itafuzu kucheza mashindano ya kimataifa, halafu mlangoni akaachwa Shikalo! Hakika yatatukuta yale ya watani zetu msimu uleee wa hamsa hamsa.
 
Viongozi wa Yanga ni wapumbavu sana, toka Kaze atoke nini wanafanya sasa, haya Mwambusi katoka ujinga tu.
Nafasi ya pili hatuipati, Prison anatusubili shirikisho kule kwao ajipigie ushenzi tu.

Kumbe mnajua kabisa nafasi ya kwanza sio yenu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Utabiri umetimia! Ubingwa ni wa Simba, kwa mwaka wa nne mfululizo. Wanastahili. Yanga ina matatizo. Kuanzia wachezaji, benchi la ufundi na viongozi.

Ni wakati sasa kwa Viongozi kuharakisha mchakato wa kuibadili timu kutoka kwenye mfumo huu wa sasa. Wachezaji wengi walio sajiliwa ni wa kiwango cha kawaida sana ukilinganisha na usajili wa Simba.

Sarpong, Jaqouba na Saidoo kwa kifupi ni wasanii tupu kazi yao kubwa ni kujiangusha ndani ya Box ili wapate huruma ya kutenga pira wapewe goli na wasipopewa wanalia kama mtoto anayelilia titi la mama yake, bado wale waliotia brechi nywele za leo sijui walienda saloon wakijitayarisha kupendeza tarehe 08/05/2021?
 
Aiseee, leo daku litanoga na kuna mahala litadoda.

Tangu awali Utopolo walikuwa wamedhamiria kumtoa barabarani kijana wa watu, kama ile head to head iliyopita. Maana sio kwa lile Shaolin soccer walilomchezea.

Kuna wakati alianza kukata tamaa na kidogo tu aombe sub. Kwenye vibanda umiza sisi wa Msimbazi tulishamwonea huruma na kujiuliza:"kwanini Lwandamina asimtoe huyu, watamuua!". Walikuwa wamvunje mgongo au kiungo chochote kwa mara nyingine.

Nadhani Mungu naye hakupendezwa na namna walivyokuwa wanamtendea, ghafla tu akamkumbuka. BOOONGE LA GOOOOAL! Yule mtesaji Abdallah Shaibu 'Ninja' akabaki ametoa macho kama mtaalamu wa maabara anayeangalia minyoo kwenye kinyesi cha mgonjwa.

Simba mmemuona Dube lakini?Huyu hahitaji majaribio wala nini,mtafuteni haraka kuimarisha pale mbele.
 
Back
Top Bottom