Full Time: Pyramids FC 2 - 1 Mamelodi Sundowns FC | CAFCL Final | 2nd Leg | 30 June Stadium | 01-06-2025 (Ag 3 -2) Pyramids Mabingwa

Hili kombe Mwakani linatua jangwani
 

Attachments

  • FB_IMG_1748196804254.jpg
    46.4 KB · Views: 17
Mental health illness is actually existing, hili povu si ungeagiza makontena ya nguo hata buku ya badarini ufulie kwa mashine Watu wanukie sop sop?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Mental health illness is actually existing, hili povu si ungeagiza makontena ya nguo hata buku ya badarini ufulie kwa mashine Watu wanukie sop sop?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
Ukiniquote uhakikishe unajIbu hoja zangu usiniletee taarab
 
Mimi mwanzo nilitamani mamelodi washinde sababu nilidhani pyramids wakishinda, watatushusha simba kwenye caf ranking ila baada ya kujua kwamba hata pyramids wakishinda, hawawezi kutushusha kwenye hiyo nafasi yetu basi sina wasiwasi yeyote ashinde tu
kuwa nafasi ya tano huwa mnalipwa shi ngapi wenzetu?
 
kwamba ulikufa kiume kufungwa na berkane?
 
Sioni kitu ambacho Simba kamzidi Yanga hakuna hakuna labdah uchawi tu
 
Motsepe kampa Kanu business card inaonekana anataka Kumtumia kuijenga zaidi Mamelody
Mayele alikuwa tz mamelody walikuwa na nafasi ya kumchukua ila wakakomaa na shalulile
Azizi kaenda wydad wao bado wanakomaa na viungo nyatunyatu acha Pyramid achukue
 
Motsepe kampa Kanu business card inaonekana anataka Kumtumia kuijenga zaidi Mamelody
Mayele alikuwa tz mamelody walikuwa na nafasi ya kumchukua ila wakakomaa na shalulile
Azizi kaenda wydad wao bado wanakomaa na viungo nyatunyatu acha Pyramid achukue

Kanu ndie bosi wa enyimba.

Timu yake ya nyumbani kwao anayoiongoza yeye imefeli, anaanzaje kuijenga mamelodi
 
Kanu ndie bosi wa enyimba.

Timu yake ya nyumbani kwao anayoiongoza yeye imefeli, anaanzaje kuijenga mamelodi
Unaweza kupata ushauri mzuri hata kwa Alie fail maana ana experience
Kumbuka Kanu kacheza arsenal na ulaya kwa ujumla ana uzoefu wa masuala ya mpira
 

Mkuu kwanza elewa katika mpira mafanikio ya kwanza ni kupata taji na ndio lengo la kila shabiki kufurahia kuona timu yake inakusanya taji kwavile mafanikio ya kipesa hayawezi kugaiwa kwa kila shabiki.

Mpaka sasa Yanga anagombea mataji mawili kati ya mataji matatu aliyoshiriki ( CAFCL, ligi kuu na CRDB FA) wakati Simba ikiwa inagombea taji moja tu kati ya mataji matatu aliyokuwa anashiriki. Siwezi kusema kugombea taji ni lazima uchukue lakini tayari Simba kabakisha shindano moja tu ambalo akilikosa anakuwa kamaliza msimu patupu kwa mara nyingine tena.

Kwenye mashindano ya klabu bingwa uzoefu haufanyi kazi bali ni ubora, mbinu sahihi dhidi ya mpinzani ndio hufanya kazi. Simba ilitolewa hatua ya robo fainali na timu ya Kaizer Chief ambayo hawakuwa na mwendelezo wa kushiriki mashindano ya CAF kwa muda mrefu sana tofauti na Simba ambao mara kwa mara wameshiriki mashindano ya CAF. Alkadharika Belouizdad pamoja na uzoefu wao wa kucheza robo fainali mara kwa mara ila wanashindwa kufuzu robo fainali kwa kutolewa na Yanga katika makundi hivyo achana na mambo ya uzoefu bali deal na current form kama navyokusisitiza mara kwa mara, mpira ni current form sio mambo ya uzoefu.

Umeongelea upande wa mashindano ya kimataifa twende in terms of numbers:

Mara ya kwanza Simba kuanza kufanya vizuri mashindano ya CAF ilikuwa ni msimu wa mwaka 2018/2019 ambapo ndio walianza kuwa na muendelezo wa kuingia mara kwa mara katika mashindano ya CAF.
Kutoka msimu wa 2018/ 2019 hadi msimu huu wa 2024/2025 Simba wamevuna point 48 katika misimu 7 ambapo ndani ya misimu 7 misimu 5 imefanyika performance ranking hivyo anapata wastani wa poont 9.6 kwa kila msimu

wakati Yanga wameanza kuingia katika kufanya vizuri CAF msimu wa 2022/2023 na kufanya muendelezo kwa misimu mitatu mfululizo na kupata point 34 zilizopatikana kwa performance ya misimu mitatu hivyo Yanga anakuwa na wastani wa point 11.333 kwa msimu. Kwa maana nyingine ni kwamba Yanga imepitwa na Simba lakini wanakuja kwa kasi katika kupata point za CAF na kuwa na wastani mzuri kama wataendelea kuwa na muendelezo.
 
Marumo alikua ameshuka daraja
Mashindano ya CAF na ligi ni mashindano mawili tofauti mkuu, ligi ni marathon hivyo lazima uvimbe haswa.

Kwenye CAF:
Hatua ya kwanza ni mechi 2
Hatua ya pili mechi 2
Makundi mechi 6
Robo fainali mechi 2
Nusu fainali mechi 2

Kutoka hatua ya kwanza hadi kuingia fainali kuna michezo 14 katika michezo 14 michizo 8 ni ya mfumo wa mtoano ina maana kwenye mashindano ya CAF ni ujanja wa mbinu sahihi ya kuzichanga karata ipasavyo tofauti na ligi kuu ambapo mechi hazipungui 30 ni mbio ndefu haswa yenye milima na mabonde mpaka kuweza kustahimili na ndio maana sio ajabu kumuona Constantine kipindi anacheza mechi ya kwanza dhidi ya Simba alikuwa anaongoza ligi ya Algeria lakini leo hii kamaliza nafasi ya 9 wakati kwenye CAFCC kacheza hadi nusu fainali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…