Gigy Money kafanya nini huko kwenye ziara ya Tumewasha na Tigo?

Gigy Money kafanya nini huko kwenye ziara ya Tumewasha na Tigo?

Chief!

Mileage! Mileage! mileage!

Hicho ndyo muhimu kwa sasa

Wakitoka hpo wanaenda kuangalia YouTube huyo kichaa kawapa mileage ngapi mtandaoni.
Hiyo mileage inaweza compasate hasala wanayoipata? Wasafi ni brand kubwa kwa sasa na wana content za kutosha, hawawezi kutegemea kick.
 
Mimi sijui kuishi kwangu marekani muda mrefu ndio kunanisumbua?
Honestly,, sijaona Cha ajabu alichofanya gigy money kwenye Hilo tamasha mpaka astahili adhabu kubwa Kama hiyo.
Ni wivu tu na mihemuko ya viongozi wa awamu ya meko
 
Nikiri kwamba mimi sikutazama live show ya Giggy Money iliyorushwa na Wasafi TV ambayo TCRA hawakuipenda.

Lakini kupitia platforms tofauti za social network nimeweza kuona picha ya Giggy akiwa kwenye vazi fulani hivi inayojadiliwa sana kwamba ndiyo alikuwa amevaa wakati wa show (picha ipo chini hapa).

Binafsi sijaona tatizo na vazi lile. Vazi limebuniwa vizuri linaonesha maungo ya Giggy vizuri kabisa. Shida iko wapi?

Mbona ndiyo hayo mavazi nayaona bichi, kwenye swimming events na maahindano ya mamiss. Bila kusahau huko kwenye mabaa, mitaani n.k. Sasa ninyi TCRA mnalinda maadili ya watazama TV tu?

Mko dunia gani nyie? Mnataka wasanii wavae madela na mashuka?

Halafu huu unafiki tutauacha lini watanzania? Hivi kweli tukipekuwa simu zenu ninyi mnaodai kukerwa na picha za Giggy hatutakuta picha za "pilau"?

Ninyi mnaojitia kukirihishwa na picha za Giggy ndiyo ninyi wenye nyumba ndogo na michepuko kama yote. Hayo ni maadili? Lkn mkisimama majukwaani mwajitia wasafi kama malaika.

Kama kweli tunataka kulinda maadili basi tuzuie uchafu kila idara, ofisi, sehemu za starehe, vyombo vya usafiri na kwingineko. Katika hili kuna kitu hakiko sawa.

2658342_JamiiForums-770985563_352x403.jpg
 
Huyo Demu alichofanya ni utovu wa nidhamu, binafsi sijapenda.

Mbaya zaidi hakuna anachoimba Cha maana huyo ni Slay Queen na video Queen TU mziki kavamia.

Alianza mwenzake Anaitwa .....Rutty (Kama sikosei Jina lake), akaharibu Sasa kafuata yeye. Mbaya zaidi TV inafungiwa ambayo ni ofisi ya vijana wenzetu.

Kila career ina talanta ndani yake hata kama anayeifanya ni kipofu usiige.

Ni wakati wa BASATA kukaa chini kuweka vigezo kabla ya mtu kuwa msanii, maana Kuna wimbi kubwa kwa wasanii uchwara ambao wana effect kubwa kwa Jamii.

Mfano ikatokea baada ya adhabu kuisha ndani ya wiki moja kuna msanii uchwara mwingine anarudia kosa lilelile na media ikafungiwa. Tena hii itakuwa kuchezea maisha ya watu.
 
Giggy hata angekuwa amevaa baibui ndio chanzo cha kufungiwa WCB miezi 6, mi ningefarijika tu.

Waliambiwa WCB msichanganye siasa na sanaa. Na huyo mnaempigia kampeni za urais 2020 hana fadhila wala hana rafiki. Ila zile kofia walizokua wanavalishwa zilikua zina wazuzua.

Acha WCB wapate malipo yao kwa kumpigia debe stone.
 
Gigy hata angekuwa amevaa baibui ndio chanzo cha kufungiwa WCB miezi 6, mi ningefarijika tu.

Waliambiwa WCB msichanganye siasa na sanaa. Na huyo mnaempigia kampeni za urais 2020 hana fadhila wala hana rafiki. Ila zile kofia walizokua wanavalishwa zilikua zina wazuzua.

Acha WCB wapate malipo yao kwa kumpigia debe stone.
Ile kampeni hawakupiga bure, walilipwa! just imagine uko kwa sebure na wazee umekaa unaangalia tv mara Gigy na nguo zimechorwa Qhuma huyu hapa, hiyo fedheha iliyoje, pia hata team nzima ya Wasaf waajibike, mtu anatoka back stage na nguo za aina hivyo hakuna hata mmoja alimuona?
 
Back
Top Bottom