Hiyo ni propaganda kwa vijana ambao hawajui dunia ilivyofumwa. Nyerere na ubabe wake na uzalendo wake alilazimishwa na mfumo auze viwanda na mashirika yote ya umma, Mwinyi na Mkapa hivyohivyo waliuza hata Yale mashirika yanayofanya vizuri. Magufuli alikuwa mbishi na rasilimali zetu zitunifaishe sisi, lakini bei ya tanzanite ikashushwa na mabeberu. Mtu/mpinzani anaweza kudhani viongozi wa Afrika wooooooooote ni wapumbavu nchi zao kuwa vile zilivyo kiuchumi na kimaendeleo ila yeye tu kama ataingia Ikulu. Hizi ndizo propaganda ambazo mm napigana nazo kwenye mitandao Kila nipatapo muda hata kidogo tu.
Tusiwadanganye watoto wetu kwakuwa wewe unaweza kuwadanganya wakawachukia viongozi waliopo ili wewe uende Ikulu ukafanye hayahaya wanayofanya waliopo. Mfano, maisha ya vijana wa Kenya yamebadilika baada ya Ruto kuwa Rais tofauti na alipokuwa Uhuru Kenyatta? Zambia na Malawi je?
Demokrasia ni nzuri kweli, lakini Sioni Lissu na Lema na Heche watakavyoweza kuifanya Tanzania iwe kama Korea Kusini bila kuiuza nchi kwa Marekani au ubelgiji. Uhuru wa Korea Kusini, Taiwan umepotea kwa Marekani. Kenya haina Uhuru tena, military bases wa mabeberu ziko pale kulinda mitaji yao. Is that what we want and need?