Iko hivyo China, NKorea, Russia, India, Uganda, Rwanda, Cuba, Iran, saudi Arabia, na kwingineko kwingi. Chama tawala ni kimoja tu, na mataifa ya Magharibi vyama tawala ni viwiliwili tu vinavyopokezana.
Hapa kwetu kura ya maoni, 80% ya watu walikataa uwepo wa vyama vingi . Hii ni kuonyesha kuwa hili zigo tumelazimishwa kulibeba na nchi za Magharibi kwa ajenda zao. Demokrasia haiwezi kuzuka tu Ikulu kama haipo kwenye ngazi ya familia, mashuleni na ndani ya jamii, ni fujo tu na kutumia muda mwingi kupishana badala ya kujenga taifa .
Vyama vingi havipo na havitakuwepo Afrika kama vitalazimishwa kwa nguvu za wazungu. Hata Magharibi Sasa hivi hakuna demokrasia, chaguzi zinaibwa na kusingizia Urusi kuingilia chaguzi zao. Trump alitaka kuuliwa ili asigombee sembuse sisi huku Africa?
Mtu anataka kuwa Rais lakini haamini muungano kama ni halali Wala muhimu, nani atakuruhisu uwe Rais? Hata Marekani, Sprain na UK wana shida na Miungano yao lakini hakuna mgombea anaruhusiwa iwe ajenda yake ya uchaguzi. Sisi hapa wapinzani wetu eti hawana miiko na Wala taifa halina miiko wala tamaduni zake. Hawafai asubuhi, mchana na jioni. Wanapinga Kila kitu kuanzia Katiba, jeshi polisi, mahakama, mbio za mwenge, muungano, utawala wa mikoa nk. Yaani wao ni wabelgiji mwanzo mwisho, matusi njenje,kiongozi gani wa Afrika aliyelelewa kwenye familia za kiafrika na kusoma shule na vyuo vya Afrika atakuruhusu wewe uende Ikulu uwe Rais?