Godbless Lema, hospitali zote hizi nchini lakini unaenda Kenya ukaangaliwe bega, una hofu gani?

Godbless Lema, hospitali zote hizi nchini lakini unaenda Kenya ukaangaliwe bega, una hofu gani?

Imeripotiwa kuwa ndugu Lema alizuiwa mpakani Namanga akidai kuwa alikuwa akienda kwa akina Martha Karua kuangaliwa afya ya bega lake na shida nyingine ambayo hakuitaja. Ukweli hii ilinifikirisha sana kama mtanzania kama kweli tumefika hapo.

Ni kweli Tanzania hakuna hospital na wataalam ambao wanaweza kumsadia mtanzania mwenzao kujua na kurekebisha afya yake hadi aende Kenya?.

Maswali:
1. Kuacha kutibiwa nchini ni ukosefu wa utaalamu au ni hofu tu ya kuhujumiwa na madaktari wa hapa?
2. Je, anakwenda kwa matibabu kweli au kwa mengineyo?
Kuna mahali katiba inakataa mtu asiende kutibiwa nje ya Tanzania? Hata ningekua mimi Lema singetibiwa hapa, wanawez akumuwekea sumu wakammaliza
 
Hizi hizi hospital mnazoua ma Dr bingwa?
download (11)~3.jpeg
 
Kuna mahali katiba inakataa mtu asiende kutibiwa nje ya Tanzania? Hata ningekua mimi Lema singetibiwa hapa, wanawez akumuwekea sumu wakammaliza
Hiyo sio kweli, Lema ana ujanja gani wa kukwepa kuwekewa sumu? Hakuna mtu mwenye roho hiyo bado.
 
Hiyo sio kweli, Lema ana ujanja gani wa kukwepa kuwekewa sumu? Hakuna mtu mwenye roho hiyo bado.
Kama mmeweza kumuua daktari wa kawaida tu anbae hna impact yeyote kwenye siasa, sembuse Lema, watekaji nyinyi
 
Mie mwenyewe sina helaa lakini siendi hospital walojazana akina shangazi mjomba na baba mkubwa(Zero competence), sembuse wenye vijisentii.
Kwa kweli hospitali nyingi za Tanzania madaktari wanachojua kwa ufasaha ni kukuandikia midawa tu.
Maabara nazo nyingi hazina vifaa vya kutosha wala wafanyakazi wenye ujuzi. Wengi waliopo ni vishoka pro max
 
Hoja zingine bwana, ni muda wa Lunch, nisije nikaharibu siku yangu.
 
Demokrasia kwa Afrika na nchi maskini inaruhusu maadui kupita kwenye mwanya uliopo kati yangu na wewe Ikulu. Demokrasia imeonyesha kushindwa kulikwamua kiuchumi bara lote Afrika, haitusaidii kabisa. Rwanda inasifika kupiga hatua kwakuwa hakuna demokrasia inayotakiwa na nchi za Magharibi. China uchumi wake unapaa kwakuwa hakuna demokrasia ya Magharibi. Sisi tunanaswa kwenye mitego huohuo wa demokrasia. Afrika inahitaji mifumo imara ya kuwaajibisha wabadhilifu na wezi mali ya umma bila kujali cheo cha mwizi.
Kama Demokrasia sio Muarobaini wa matatizo yetu, unashauri nini kama mbadala? ni Jeshi lichukue nchi? Ni Utawala wa Kifalme? Turudishe Utawala wa Machifu? Maana hiyo ndio jadi yetu! Hiyo mifumo Imara unayoshauri ya kudhibidi wezi wa mali ya Umma bila kujali cheo cha mtu, itajengwa juu ya msingi upi hasa ?
 
No reforms, No election
No reforms, No election
No reforms, No election
No reforms, No election
No reforms, No election
No reforms, No election
No reforms, No election
No reforms, No election
No reforms, No election
 
Hiyo ni propaganda kwa vijana ambao hawajui dunia ilivyofumwa. Nyerere na ubabe wake na uzalendo wake alilazimishwa na mfumo auze viwanda na mashirika yote ya umma, Mwinyi na Mkapa hivyohivyo waliuza hata Yale mashirika yanayofanya vizuri. Magufuli alikuwa mbishi na rasilimali zetu zitunifaishe sisi, lakini bei ya tanzanite ikashushwa na mabeberu. Mtu/mpinzani anaweza kudhani viongozi wa Afrika wooooooooote ni wapumbavu nchi zao kuwa vile zilivyo kiuchumi na kimaendeleo ila yeye tu kama ataingia Ikulu. Hizi ndizo propaganda ambazo mm napigana nazo kwenye mitandao Kila nipatapo muda hata kidogo tu.

Tusiwadanganye watoto wetu kwakuwa wewe unaweza kuwadanganya wakawachukia viongozi waliopo ili wewe uende Ikulu ukafanye hayahaya wanayofanya waliopo. Mfano, maisha ya vijana wa Kenya yamebadilika baada ya Ruto kuwa Rais tofauti na alipokuwa Uhuru Kenyatta? Zambia na Malawi je?

Demokrasia ni nzuri kweli, lakini Sioni Lissu na Lema na Heche watakavyoweza kuifanya Tanzania iwe kama Korea Kusini bila kuiuza nchi kwa Marekani au ubelgiji. Uhuru wa Korea Kusini, Taiwan umepotea kwa Marekani. Kenya haina Uhuru tena, military bases wa mabeberu ziko pale kulinda mitaji yao. Is that what we want and need?

Kavulata: Unaandika with too much generalization angalau uwe unajaribu hata kuangalia historia..

" Uhuru wa Korea Kusini, Taiwan umepotea kwa Marekani."

Labda uwe unarudia historia kidogo za nchi kama Taiwan na hiyo Korea Kusini......
 
Haya mambo ya kupangiana maisha, na pia kuzuia watu kusafiri kwenda nje kisa tu wataenda kuyaanika maovu yenu; ni ya kishamba na kipumbavu. Mngekuwa siyo wachafu, hata msinge jishughulisha kuwazuia.

Inakera sana kuona watu wqlazima mnafanya mambo ya kitoto.
Yeye kama mpinzani aoneshe mfano wa kutibiwa hapa hapa Tanzania,kama anavyoongea kwenye majukwaa

Kama hawezi aache kuwananga viongozi wanaokwenda nje
 
Unampangia atibiwe wapi? We ni nani? mkewe.

No Reforms....
 
CCM hamuaminiki mlitaka aende hospitali gani mummalize?
 
Imeripotiwa kuwa ndugu Lema alizuiwa mpakani Namanga akidai kuwa alikuwa akienda kwa akina Martha Karua kuangaliwa afya ya bega lake na shida nyingine ambayo hakuitaja. Ukweli hii ilinifikirisha sana kama mtanzania kama kweli tumefika hapo.

Ni kweli Tanzania hakuna hospital na wataalam ambao wanaweza kumsadia mtanzania mwenzao kujua na kurekebisha afya yake hadi aende Kenya?.

Maswali:
1. Kuacha kutibiwa nchini ni ukosefu wa utaalamu au ni hofu tu ya kuhujumiwa na madaktari wa hapa?
2. Je, anakwenda kwa matibabu kweli au kwa mengineyo?
Mtu yupo haki ya kutibiwa popote, ili hali hajakuomba mchango
 
Kwa kweli hospitali nyingi za Tanzania madaktari wanachojua kwa ufasaha ni kukuandikia midawa tu.
Maabara nazo nyingi hazina vifaa vya kutosha wala wafanyakazi wenye ujuzi. Wengi waliopo ni vishoka pro max
Je, unalipa Kodi? Kama unazo nenda aga Khan, regency, TMJ, Kairuki, Rabinsia, Hindu Mandal, Ibrahim Haji. Hadi Nairobi?
 
Kama Demokrasia sio Muarobaini wa matatizo yetu, unashauri nini kama mbadala? ni Jeshi lichukue nchi? Ni Utawala wa Kifalme? Turudishe Utawala wa Machifu? Maana hiyo ndio jadi yetu! Hiyo mifumo Imara unayoshauri ya kudhibidi wezi wa mali ya Umma bila kujali cheo cha mtu, itajengwa juu ya msingi upi hasa ?
Tuandamane kudai watu wote wasiwe na kinga ya kushitakiwa kama wametuibia. Mwizi wa mali ya umeme atenganishwa kichwa na kiwiliwili chake. Hicho ndicho kinachofanyika China NKorea, Soviet, Iran, Saudi Arabia nk ambako demokrasia hakuna. Hapa kwetu waliua Azimio la Arusha na kuletA Azimio la Zanzibar.

Sasa wanajitokeza wajinga fulani wanasema watakinukisha vibaya sana siku ya uchaguzi ili usiwepo. Maana yake wanataka kuharibu hata kile kidogo kinachowasaidia wananchi, pili wanasababisha CCM iendelee kuwepo madarakani kirahisi kabisa kwa miaka 7 mingine, tatu watanzania wenzao wataumia na kufa kipumbavu kabisa. Safari hii wananyang'anywa passport zao wabaki hapahapa kwenye nchi itakayokuwa umevinjwavunjwa kwa vurugu.
 
Kuna mahali katiba inakataa mtu asiende kutibiwa nje ya Tanzania? Hata ningekua mimi Lema singetibiwa hapa, wanawez akumuwekea sumu wakammaliza
Sheria zetu Zina referral systems zake kwenye maswala ya matibabu kuanzia mtu anaumwa nyumbani kwake hadi kwenda kutafuta matibabu nje ya nchi (abroad). Kumbuka kuwa raia wote ni mali (rasilimali) ya taifa, huwezi kujichomokea tu kama nyumbu wa Serengeti na masaimara.
 
Lema anakwend akutibiwa aprivate,mimi nilimpeleka mwanangu kutibiwa south africa na sikuanzia hospitali yoyote hapa bongo, na wala sikuzuiliwa airpoort, acha kupotosha watu
 
😁😁😁Hiki kipande huwa nikisoma mahali popote kina nichekesha sana hivi kwa nini waliamua kumuita mgonjwa ghali 😁
Alitibiwa kwa bill kubwa kuwahi kutokea na bado alienda na delegation kubwa ambayo hakuwa na sababu kwenda nayo.
 
Back
Top Bottom