Kifungu gani katika sheria za uhamiaji kinataja hili suala?Kwani alikuwa nakwenda kutibiwa hospitali gani na dk nani lini?
Lema ni private citizen sio senior citizen , Lema hana cheo chochote katika utumishi wa umma hivyo hahitaji kibali kutoka kwa mwajiri ili asafiri.kumbuka Lema ni senior citizen
Wabunge wana siri gani?, amepata kuwa mabunge wa taifa letu, anazo siri nyingi kuhusu nchi.
Wewe zinakutosha kweli?
Siku hizi mtu ukiwa na siri za nchi walikudanganya ili kama umeazimia kuzimwaga lazima utoke nje ya nchi?
Mbona waliovujisha mabilioni ya IGP Wambura hawakutoka nje bali hapo hapo Tanzania?
Waliovujisha dili za kina Lugumi hadi mama Abdul akawaka walitoka nje si hapo hapo ofisini kwao?
Wazalendo waliovujisha mkataba wa kitapeli wa kuuza bandari si walitoka hapo hapo ikulu akaamua apige fagio .
Kupuyanga ni nini ?Hawezi kupuyanga tu anavyotaka.
Utajuaje mtu kapuyanga, wewe kwa akili hizi za cold war ndio zinairudisha nchi nyuma kama miaka hiyo kusafiri mpaka upate kibali cha ticket ya ndege kwa gavana wa BoT.
Huu ni upumbavu , kama wao walikuwa na uhitaji wa interrogation na Lema walisubiri nini hadi asafiri ndio wamuite huoni kuna ukakasi , stop order waliitoa lini?