Habari za Kiuchunguzi kuhusu Maelfu ya Askari wa Rwanda waliouawa katika mapigano ya DRC

Sio kwamba wanalink na nchi Yao hapana wanatumika na wanaaminishwa Kwa maslahi ya kagame na kusambaziwa propaganda kuwa wao ni watu Bora sana
 
Suala la Hutu na Tutsi ni suala fulani la kihisia zaidi kuliko uhalisia na hizo hisia zote zimehengeka katika misingi siku ukisikia wanaojinasibu kuwa ni waTutsi na WaHutu wanavyoongea ndo utajiuliza tofauti zenu ni nini? Mfano Mhutu anajejiita anasalimia Amakulu, Mtutsi anasalimia Amakulu yaani ni kwamba wanakamusi moja hakuna kamusi ya Wahutu au Watutsi ila kunakamusi ya Kinyarwanda na Kirundi sasa unapoongelea habari za Ubantu mara Unilotic unakuwa umeenda nje sana hata hivyo Rwanda na Burundi kamusi zao zinaelekeana kwa asilimia 80% lakini kote kuna Watutsi na Wahutu ambao sio makabila ila ni makundi ya kujinasibu pia kuna kundi dogo sehemu zote wanaitwa Watwa.
Vita ya M23 ina lundo la habari nyuma yake na inakuwa ngumu kuikabili moja kwa moja kwa kuwa ina maslahi ya wenye nguvu ya uchumi wa Dunia nyuma yake ndo maana nchi nyingi kujiingiza moja kwa moja zinasita hasa nchi jirani
 
EAC na AU ni vijiwe vya wahuni Africa Ina laana Angalia Aiti
 
Baada ya Burundi ni Kigoma M23 wako mitano Tena subiri Pengo la Mkapa ni Kubwa
 
Sio kwamba wanalink na nchi Yao hapana wanatumika na wanaaminishwa Kwa maslahi ya kagame na kusambaziwa propaganda kuwa wao ni watu Bora sana
Hii sio kweli na ndio sababu hii vita inatokea, haki za uraia na usalama wao ndio issue sio hizi conspiracies mnazodanganyana humu, Kagame alikuwa mkimbizi for almost 30 years na walipojaribu kurudi waliambiwa nchi imejaa and you don’t belong here na wengine kuuliwa, Banyamurenge going through the same thing, acha waitafute haki yao and they don’t need your help pigeni mdomo tuu
 
Kama kagame alikuwa mkimbizi na kurudi Rwanda hao wengine wanajiona wakimbizi SI warudi Rwanda?
 

Kama Rwnda wanakufa hivyo. Je, DRC itakuwaje!?
 
Suala la Hutu na Tutsi ni suala fulani la kihisia zaidi kuliko uhalisia na hizo hisia zote zimehengeka katika misingi siku ukisikia wanaojinasibu kuwa ni waTutsi na WaHutu wanavyoongea ndo utajiuliza tofauti zenu ni nini?
Hapa unacHanganya mambo. Wahutu na Watusi wamekaa pamoja kwa karne siyo siku moja. Zaidi ya hapo nchi zao ni ndogo na jamii zao zinaishi kwa ukaribu sana. Lugha zao zinafanana kwasababu ya mwingiliano. Kule Musoma kuna Waruli, Wakwaya na Wajita. Wanaongelea lugha zinazoingiliana kwa asilimia 90! lakini hawa ni makabila tofauti
Matumizi ya neno Banyarwanda limekuzwa sana baada ya mauaji ya Kimbari. Anayehimiza ni PK kwa kuangalia mfano wa Tanzania. Kwamba ukiwa Tanzania wewe ni Mtanzania lakini haiondoi ukweli kwamba katika Tanzania kuna Wabantu, Nilotics n.k.

Kamusi ya Tanzania ni moja, Kiswahili. Mmakonde, Mngoni, Mkurya, Muha, Mchaga, Msukuma, Mmasai, Mbarabaigi, Mrangi wote wakiongea utaulizwa swali lako, tofauti ya hawa watu ni nini? Jibu lake ni kwamba wanaunganishwa na lugha lakini haindoi ukweli kwamba kuna Wabantu, Nilotic n.k.

Rwanda kuna Wahutu na Watusi, wana kamusi moja, lakini haiondoi ukweli kwamba Watusi walikuja.
Historia inasema hivyo! Bila kukubali historia hawa watu wataendelea kuuana kama ilivyotokea miaka ya 90

JokaKuu
 
Usifananishe lugha na kabila. Lugha ni kitu unachoweza kujifunza ila kabila lina chimbuko la asili ya mtu. Hata wewe kama unaifahamu lugha yao unaweza kusalimia na kuitikia hivyo. Ila hutu na tutsi ni kabila mbili tofauti. Kwenye mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 unadhani wahutu na watutsi hawakujua nani ni mhutu na nani mtutsi?
 
Rwanda kuna Wahutu na Watusi, wana kamusi moja, lakini haiondoi ukweli kwamba Watusi walikuja.
Historia inasema hivyo! Bila kukubali historia hawa watu wataendelea kuuana kama ilivyotokea miaka ya 90
Rwanda pale hakuna amani. Kuna utulivu wa muda tu na sababu ni hiyo ya kutoshughulikia tofauti zao za kikabila. Wahutu wakishika madaraka kama walivyoshika Burundi watutsi nao hawatakubali kutawaliwa na ndio utakuwa muendelezo wa mapigano ya kikabila kati yao.
 
Si mlisema wale wanyarwanda waliopo Congo ni wakaazi wa Congo ambao ni raia wa Congo ila tu wanabaguliwa kwa unyarwanda wao! Sasa inakuwaje wanapelekwa kuzikwa Rwanda? So ni ushahidi kwamba Rwanda anasapoti m23?
 
Tatizo ni Watusi wana '' superiority complex'' na Wahutu wana ''inferiority complex'' . Tazama sakata la DRC, ni Watusi wanaoleta mapigano kwamba wananyimwa haki. Ukiuliza haki gani, wanasema ya kushirikishwa serikalini!!! Wana haki zote lakini moja tu wanaitaka, kuwemo serikalini tena wakitaka asilimia

Niambie wapi ambapo Watusi wamewahi kuishi pakawa salama. Unakumbuka ya Uganda?

Mkapa aliwarudisha baada ya vita. JK naye akawarudisha katika sakata lake na PK.
Mkapa na Kikwete walifahamu wakipewa kata ipo siku watadai Wilaya n.k.

Watu wasikatae kwamba hakuna Utusi na Uhutu! lazima watu wakubali historia ili wajifunze kupitia kwalo
 
Eti watusi walikuja, kwa akili hii ya kipumbavu ndio maana vita haviishi then mnaishia kulaumu kina PK, una same thinking ya Tshesekedi Uber driver from Brussels, anawaambia Banyamurenge ambao wako Congo kabla ya mkoloni sio raia warudi kwao , wtf acha zipigwe tuu kitaeleweka
 
Historia ndiyo imeandika hivyo na Watusi hawajakanusha. Ikiwa ni upumbuvu basi ni wa Historia si Wasomaji
Pili, PK analaumiwa kwa kuunga mkono M23 kwa silaha na askari. Soma mada ya Uzi huu utaelewa.
Tatu, Banyamurenge walikuwepo wakati wa Mobutu, mbona hawakuwahi kubeba silaha!
Nne, Tshesekedi kuwa dereva Uber haondoi ukweli kwamba ni Rais wa DRC. Udereva wake si hoja
Tano, ikiwa Banyumulenge ni Raia haki gani wanayodai na kupelekea wabebe silaha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…