Hakuna kitu kinachoitwa kipaji (kuzaliwa na uwezo wa kufanya kitu fulani)

Kama ni mzazi kaa na watoto wako uwasome halafu utapata majibu.
Mtoto anaweza kuvutiwa na kile ambacho kipo kwenye jamii/ mazingira yake kwa mfano mtoto wa mhadzabe hawezi kuvutiwa na mpira wanmiguu wakati hicho kitu hakiko katika jamii yao.

Hii inamaanisha kuwa hakuna kitu kinachokaa damuni bila hicho kitu kuwepo katika mazingira husika.

Are we together? Say yes.
 
Hiyo ya Vishu Mtata ni tamaa mbaya hivyo aichunge😂
 
Kwenye mamipira nitajitoa
Tukutane kwenye jukwaa la siasa tujadili no reform no election'
 
Kipaji ni kufanya kitu au jambo katika ubora na ufanisi zaidi Kwa urahisi bila kuumia
Vipaji vipo na watu wana vipaji
Wewe huwezi kuwa Bora kwenye football kama mesi
Yeah!...mfano mzuri wa tofauti ya kipaji na juhudi utauona kati ya Messi na CR7.
 
Dogo mishangazi si ndio mambo yako
 
Hapana mkuu vishu hayo mambo anajikuta kupenda..
Alishawahi jaribu mpaka tukaenda tanga kwa msisi ili tuu aache lakin daah haijawezekana mkuu
Vishu ni mtata sana anajifanya anataka kuachana na mishangazi kumbe kiuhalisia hataki kabisa kuwaacha kwa sababu wanamlea.
 
Na kweli kwenye elimu kuna watu wamepata shida sana aisee, hasa wale wanaorudia mitihani, mtu anarudia pepa zaidi ya mara 4 enzi hizo na bado hatoboi
 
Mchezaji yupi wa soka asiyefanya mazoezi huyo, physical bod fitness inapatikanaje bila ya kufanya mazoezi? Muwe mnaacha hadithi za vijiweni.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Na kweli kwenye elimu kuna watu wamepata shida sana aisee, hasa wale wanaorudia mitihani, mtu anarudia pepa zaidi ya mara 4 enzi hizo na bado hatoboi
Sasa mtu anasoma kitabu halafu muda huo huo anawaza mapenzi, mpira na mambo mengine lakini mwenzake anasoma kitabu na anawaza anachokisoma na akimaliza kusoma anawaza alichokisoma na kukihusianisha na jamii halafu anategemea kufaulu kweli😎.

Atarudia shule mara mia mbili na hatatoboa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…