Hakuna kitu kinachoitwa kipaji (kuzaliwa na uwezo wa kufanya kitu fulani)

Utakuwa huelewi dhana ya neno kipaji! Kwani huko kuchorachora panzi wewe ulifundishwa na mtu au ulianza tu kuchora mara baada ya kujua kushika kalamu? Kama la mwisho ndiyo jibu basi hicho ndicho kipaji! Ndiyo maana unaona hata Messi alianza kucheza matambara mtaani baada ya kuonekana ana kipaji cha mpira akachukuliwa kwenda kwenye academy ili kukuza hicho kipaji. Pia unaona kuna watu wasiokuwa na kipaji wanalazimishwa kufanya jambo lakini mwisho wa siku wanachemka! Chukulia mfano wa mtoto wa mchambuzi fulani wa mpira hapa nchini (jina kapuni), amelazimishwa kucheza mpira mpaka kupelekwa kwenye academy za maana lakini wapiiii kwa vile hana kipaji cha mpira ameshindwa kufurukuta! Hivyo kipaji mtu anazaliwa nacho bali ujuzi ule wa kusomea hicho siyo kipaji!
 
Tazama vizuri namna yao ya uchezaji....juhudi na kipaji vinajionyesha.
Pia tazama Kila mmoja alianza kucheza lini, akiwa na umri gani na katika mazingira gani kisha uje na majibu.

Halafu angalia pia maumbile yao halafu pia angalia umakini wao wawapo uwanjani.
 
Ushakuza mtoto wa muhadzabe ukaona havutiwi na mpira,?
 
Mtoto wanhuyo mchambuzi kipaumbele chake siyo kucheza mpira ndiyo maana akili yake haiko huko.

Halafu huwezi ukaanza kuchora tu pasipokuwa na kitu kinachokuvutia kufanya hivyo.
 
Hicho Ndio kipaji!
 
Kuna Jamaa alifeli kabisa form four kwa kupata division 4. Alianza kusoma Certificate, Diploma na Bachelor Degree akipata A+ za kutosha na akiwa first no kwa wastani wa GPA. Alipomaliza chuo kikuu X alibakizwa pale pale chuoni kupata tutorial lectures na hadi sasa ni Mwalimu mkubwa tu wa chuo kikuu X nchini kwenye sciences faculty ingawa form 4 hakufaulu vizuri zaidi kwenye masomo hayo hayo ya sayansi.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Ali switch akili yake na kuanza kusoma kwa strategy tofauti hata akafikia alichokikusudia.

Halafu mtu anakuambia kuwa hicho ni kipaji.
 
Unachora Rada Kama wezi au unachora Nini ?

Unazungumziaje Jambo ambalo wewe unatumia miaka kumi kulielewa na miaka Saba kulimudu huku Kuna mwenzio anatumia wiki.
Hakuna cha mwenye kipaji ni illusions tupu.
Inamaana huyu naye hakuwa na kipaji aliyefanya majaribio ya kutengeneza mwanga wa balbu zaidi ya mara 1,000?
Kama alikuwa na kipaji kwanini ilimgharimu mara nyingi kwa muda mrefu kutengeneza mwanga wa balbu aliyetengeneza pekee duniani?


Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Mkuu kwani neno 'kipaji' kwako unalielewaje?

Hivi uanelewa tofauti ya hobby na kipaji?

Nikuulize swali dogo, mnapokuwa vijana:
Kwanini mmoja apende udereva, mwingine apende ualimu, mwingineapende uhandisi nk nk na kila mmoja aione kazi anayoifanya ama kuipenda mwenzake, yeye haiwezi?

Embu fikiria mara mbili mbili katika kuchambua majibu ya utafiti wako huo.

Wewe kung'ang'ania sanaa ya uchoraji mpaka kuwa mahiri ni kipaji chako hicho, mwingine hawezi hata akifundishwa, maana anakuwa hapendi toka rohoni mwake.
 
Huyu alifanya bidii kujifunza wapo wenye kipaji
 
Hahaha πŸ˜‚ watakuambia alikuwa na kipaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…