Wakati fulani wa ujana wangu nilijaribu huu ujinga wa kutaka kumiliki mke na kimada(ndoa ikiwa na mwaka ½ baada ya wife kujifungua mtoto wa kwanza),yupo mmoja tulikutana kwenye issue za kibiashara alikuwa mteja wangu nikaona huyu huyu mwenye akili ya biashara nisogee nae since alishaniambia umri umesogea amekata tamaa ya kuolewa so nikaona niingize vocal.
Nikiwa ktk process(sijamtamkia bado ila alishahisi kitu) nikajikuta nimejichanganya ana deni langu 1.4mill na sikuwahi kuwaza kwamba kuna siku nita-spend more than 1mill kwa mwanamke asiyekuwa mke wangu nikajua huyu nikileta ujinga hela yangu imeondoka so nika-mute nikawa namsikilizia alipe then niropoke,yale mazoea ya kijinga niliyokuwa nimeanza yakaanza kuni-cost alikuwa hakai na deni langu zaidi ya wiki tatu ameshanilipa lakini mara hii ukaenda mwezi miezi miwili ikiwa tunautafuta wa tatu siku hiyo nimeamka asubuhi nakuta text yake ”jamani A naomba nikoposhe mill 2 nataka nikanunue kiwanja kuna best'angu kaka'ake amekwama kipo sehemu nzuri kweli yani”
Wife alikuwa amechelewa kuamka nikageuka nikamtizama pale kitandani amejilaza kwa utulivu na mwanetu mchanga kichwani nikawa natafuta sababu ni nini hasa nakikosa kwa huyu hadi nigharamike kiasi hiki?akili ilinirudi baadae nipo ofisini ananipigia kuuliza kama niliona ujumbe wake nikamwambia ujumbe nimeuona lakini siwezi kukukopesha wakati nakudai nikamkazia kwanza niletee hela yangu (ile 1.4)nina kazi nayo,alinuna wiki mwisho heshima ikarudi.
Ukishakuwa na familia yote fanya kwa ajili yao,wafurahishe ukiona una hela kidogo ya ziada nunulia wanao kitu siyo kwenda kutapanya,hukosi cha kununua kama ni nguo hata viatu au ule muda unaenda kwa vimada kaa na familia yako furahi nao utapata baraka zaidi.wanawake wengi wanaokubali kuwa vimada siyo wanakupenda sana hao wapo na wewe ili wakuibie tu hizo hela za kuwalipia nyumba sijui kununua simu nzuri nenda kawekeze kwa ajili ya familia yako,una watoto wanasoma wanataka wale vizuri walale pazuri mkeo afurahie kuolewa na wewe ukiendekeza vimada haya huyafanyi.