Hali ya kiuchumi Arusha inazidi kushuka kila uchwao

Tatizo la Arusha na Miji mingine inayotegemea sekta za Utalii na Madini ni kwamba pesa hizo huenda Kwa watu wachache , makampuni na Serikali ila mtu wa chini hazimfikii sana.

Ikiingia hapo Mjini unaona magorofa yanapanda sana Kwa Ajili ya Mahoteli ila Sasa huku kwenye grassroots ndio Changamoto.

Ni tofauti sana na Dar ,Mwanza au Mbeya ambako Kuna shughuli za aina nyingi hasa zile za watu wa chini wanapata uhakika wa hela.
 
Kipindi pekee ambacho Arusha ilipitia hali mbaya zaidi kiuchumi ni kipindi cha Covid, na hapo kabla kile kipindi cha Magufuli.
Lakini tangu huyu mama Samia aingie, flow ya pesa imeongezeka zaidi kupitia Utalii.
Na huu ndio ukweli.Angalia tuu hapo Mjini Magorofa yanavyopanda, mikutano haikauki hapo AICC na Watalii Wanazidi kufurika.

Shida ni hizo sekta ni za wachache na Serikali ndio maana unaona watu wa chini wanalalamika
 
Na huu ndio ukweli.Angalia tuu hapo Mjini Magorofa yanavyopanda, mikutano haikauki hapo AICC na Watalii Wanazidi kufurika.

Shida ni hizo sekta ni za wachache na Serikali ndio maana unaona watu wa chini wanalalamika
Kwani hujui huyo aliyeanzisha hii thread ni mtu wa ziwani kwa lengo la kuipondea arusha hawa watu kutwa kuishambulia arusha sijui imewafanyaga nini🤣 wapi uliskia mtu wa arusha amelalamika hakuna kipindi kuna mzunguko arusha kama sasa hivi, hakuna kipindi kuna magari, biashara na ujenzi kama sasa hivi mji uko busy kwelikwel
 
Swala la msingi ni kwamba competition ya Arusha ni kubwa ,huko kwingine unakosema ni kwamba Bado watu ni mbumbumbu.

Moja ya Mji watu wanajua biashara na customer care ni Arusha
Kuhusu customer care ni swala binafsi haliangalii kabila mji wala jinsia. Issue ya ubaguzi hiyo ipo wazi sana, Arusha ukabila bado upo, Dar inaizidi Arusha kwa kila kitu mpaka competition lakin hakuna ubaguzi wa kikabila ndiosababu mpaka wakinga licha ya uchache wao lakini wanafanya vizuri kibiashara
 
Sio swala binafsi ni swala linloletwa na level of competition
 
Leo umeangukiwa na kitu kizito kichwani.

Eti mnaitwa Jiji la Wadudu 😁😁😁😁

Ukweli ni kwamba competition ya Arusha ni kubwa ndicho kimemshinda mtoa mada.

Anatakiwa kwenda Kwa washamba huko Mikoani
Mkoani ndio wapi? Je Arusha sio mkoani? Kitanzania tanzania mjini ni dar tu,kulikobaki hakujapishana kiivyo.
 
Kwahiyo na huko dar watu waarusha wameshaleta ukabila kwenye biashara? Maana wamejaa huko!

Mbona Kuna watu kibao wameingia Arusha hawana kitu na wamekuwa mamilionea, au mnazungumzia biashara za kioski?

Nyumba ya vyumba vitatu Arusha kwa 150,000 hata nduruma huipati mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…