Hali ya SGR ni mbaya na mradi haujulikani utakamilika lini

KIZIMKAZI ANAJUA HILI?
 
Nani kakwambia mradi umesimama!?

Mbona hamjiongezi kufatilia zaidi ya kusaka vijarida vya udaku na kuleta hapa

Mradi unaenda vizuri zaidi ya jana
Ha ha haaa unaendelea kufa au? Kuna vitu sio mpaka uambiwe macho yanaona
 
Bashungwa ni Kafara la Mzanzibari. Mradi ulishahujumiwa.
Innocent bashungwa ...... wizara yake haihusiki na mradi wa sgr mtamlaumu bure kijana wa watu ....yeye yupo wizara ya ujenzi ,anasimamia miradi ya barabarani.iliyochini ya tanroad,na magorofa yaliochini ya tba na NHc
 
This is unaccepatable huu mradi haiwezekan ukaachwa ukafa itakuwa loss kubwa ya takriban trillion 23+ sisi kama taifa hatuiwez hii hasara na fedhea
SGR ilikuwa propaganda
Hapakuwa na sababu ya kutumia pesa zetu au za kukopa kujenga reli
 
"Sisi tunajua nani yuko nyuma ya hasara hii kubwa kwa hili taifa na tunajua nguvu inatumika kumficha na kumlinda" - Nukuu Kama mtu ama kikundi kinafahamika kuwa kipo nyuma ya ufisadi huu, basi ni vyema wahusika wakawekwa wazi ili mijadala kwa umma ianze, natambua itabamba sana kama ilivyokuwa katika sakata la mkataba wa DPW na bandari.
 
Nani yupo nyuma ya hujuma hii?
Nyuma ya hujuma hizi wamo,
1. Mawaziri na wabia wao wenye kampuni za usafirishaji eg. Esther Luxuries, Lake Oil etc
2. Wabunge na wabia wao wenye kampuni za Usafirishaji eg. Aboob Bus service, Shabiby Line,, GSM
3. Wabia wa wakurugenzi na watoa maamuzi kwenye Serikali wenye kampuni za usafirishaji eg. Sharoom, world Oil, Nas etc.
Kwa sasa chuma kimeingia kutu, huu mradi ambaye engeweza kuthubutu kukamilisha JPM (RiP); hujuma za miradi kama hii zinafanywa na hao juu!
 
Pita tandale,sinza nk uone
Nyie sahv kufagia tu barabara mtihani...

Ova
Ili la kufagia hizo barabara limekuea mtihani kweli kweli. Inaonyesha tumezoea barabara za vumbi. Barabara unakuta imejaa mchana kwa zaidi ya 70% ya njia nzima.
Maintenance hatuwezi kabisa. Tunachoweza ni kuzindua tu
 
Jiwe alikuwa na mabaya yake lakini angekuwepo leo SGR ingeshakuwa inapiga kazi na sehemu nyingine ujenzi unaendelea vizuri
Yule jamaa alikuwa vizuri sana kwenye miradi
 
Bila kumdhibiti Mzee wa Msoga na yule rafiki yake aliyenunua kampuni ya Tigo,hatutoboi milele!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Shida wale watu wa Ngome wanatuangusha na kutukosea sana.Hivi wanaelewa jukumu lao la kulinda kweli!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Sasa tufanye nini mkuu?
Mi nadhani hilo ndilo la muhimu zaidi kwetu sote.
Huu mradi lazima uishe lakini kuna kitu nchi hii lazima tufanye kwa dhamira kubwa bila kujali itikadi zetu. Ni lazima kuwe na sheria kali kabisa za kuwakamata hawa wanaofaidika na miradi hii sababu njia kubwa ya kuiba pesa ni miradi dunia nzima, hata UN majanga yakianza ndio vichaka vya kupiga. Ni lazima tufike wakati na sio kwenye mradi huu tu mingine wawe wanaitwa na kuhojiwa Live kwenye TV na kueleza kila kitu kwa uwazi na mtu akikutwa anahatia basi apelekwe mahakamani na hawa sio kufungwa tu ni kutaifishwa mali zote, pia ku trace kama mali zimeandikwa majina mengine kuepuka kushikwa zote zinataifishwa mnamrudisha kama alivyotoka kijijini kwao tukija kufanya hivi ndio tutakuwa na adabu. Ni kama ukishikwa unaiba maji au umeme haijalishi umeanza jana tu kuiba unapigwa fine ya miaka 30 huko ulikuwa unaiba, bila kuwa serious katika hili tunapoteza muda tu. China sijui South Korea hawana msalie mtume kwenye kuiba mali ya umma wana sheria kali sana hapa duniani.
 
Chakufanya wapelekwe aridhini, kwa hatua yalipofikia haya majizi hakuna namna nyingine.
Ninakubaliana na wewe; lakini swali jingine linakuja: tutaanzia wapi, nani atasimamia kazi hiyo ya kusafisha taifa letu kuondokana na takataka hizi.

Kwa hali ya kawaida, mimi ni muumini mkubwa wa kinachoitwa "Demokrasi"; lakini kwa hali tuliyonayo hapa kwetu, tukipata 'Dikteta', kiongozi asiyetenda uovu kwa mtu bila sababu za msingi, lakini anayejali maslahi ya nchi hii, kiongozi huyo anahitajika sana wakati huu kuliko wakati mwingine wowote.
 
hii itamfumua mtu kwenye kampeni za 2025 hii. walisema pesa zimekopwa, zipo. halafu kuna mpunga mwengine mrefu sana ulikpwa benki ya dunia ili kujenga gati za bandari, tunataka tujue na hizo pesa zimeenda wapi manake kwa namna wanavyotaka kutaifisha bandari basi hizo pesa wangepeleka kwengine, wangepeleka imalizie SGR. yajayo yanafurahisha.
 
Shida wale watu wa Ngome wanatuangusha na kutukosea sana.Hivi wanaelewa jukumu lao la kulinda kweli!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Nami mara kadhaa najiuliza swali hilo mara kwa mara, ingawaje bado ninayo matumaini kwamba haitakuwa lazima wahusike wao, kwani hali hii tuliyofikia sasa italazimu tu tuirekebishe wenyewe nje ya ushiriki wa hao watu wa ngome.
 
Unayoeleza hapa, ni moja ya mambo aliyosifiwa nayo Magufuli, pamoja na maswala mengine ambayo hakuyfanya vizuri.

Mimi ninakubaliana nawe, haya yote yakifanyika ndani ya sheria zetu zilizopo, bila kuoneana.
Sasa tatizo linabaki palepale, tuanzie wapi?
Nani ataongoza juhudi hizi.
Tutampata wapi Magufuli mwingine (mwenye utulivu wa akili zaidi) aongoze mapambano haya?
Mie namtafuta Edward Sokoine, zaidi ya Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…