Mpaka sasa nchi ina Idadi ya majiji sita, ambayo ni ;
- Dar es Salaam
- Mwanza
- Tanga
- Mbeya
- Arusha
- Dodoma
Ni miaka 3+ tangia kuongeza kwa Idadi ya majiji, ambapo Dodoma ilipandishwa hadhi na kuwa jiji. Mpaka kufika 2035 ni Manispaa/Mji upi utakuja kupandishwa hadhi na kuwa Jiji.
Manispaa/Miji hiyo ni,
- KINONDONI
- SONGEA
- KIBAHA
- MOROGORO
- BUKOBA
- KAHAMA
- IRINGA
- NJOMBE
- MOSHI
- SUMBAWANGA
Kwa mtazamo wako lipi ni Jiji linalofuata...!?
KUMBUKA
- Hadhi ya Jiji hugewa Wilaya
- Kuna mikoa ina majina sawa na mojawapo ya Wilaya zao
- Mkoa mmoja unaweza kuwa na majiji mawili au zaidi.
- Majibu ya wadau ,yatakusaidia kujua sehemu mpya ya kwenda kuwekeza.
- Vigezo vikubwa vya kuwa Jiji ni Idadi ya watu + pato la Wilaya.
- Majengo ya ghorofa siyo kipimo cha jiji,,
Hadhi za Wilaya kwa mpangilio wa ukubwa wa hadhi ni.
- Halmashauri ya Wilaya
- Halmashauri ya mji mdogo
- Halmashauri ya mji
- Halmshauri ya manispaa
- Halmashauri ya Jiji