Hamza Johari: Timu ya Uchunguzi wa Mkataba wa DP World iliteuliwa na Hayati Magufuli, Rais Samia anaendeleza mchakato

Hamza Johari: Timu ya Uchunguzi wa Mkataba wa DP World iliteuliwa na Hayati Magufuli, Rais Samia anaendeleza mchakato

Siko Serikalini Wala TPA so siko kwenye nafasi ya kujibu Hilo.

Wa tag wahusika wapo kwenye social media..

Mimi ni independent variable
Huwezi kuwa "Independent Variable" wakati unapokea kila lisemwalo ukalimeza na kulisambaza.

Umeleta hoja, jibu hoja za majadiliano. Kama una hoja isiyo na ushahidi, usiileta humu JF
 
😂😂😂😂 ya ndani yanazidi kuwekwa Wazi johnthebaptist

-
“Timu ya uchunguzi [kuhusu bandari] iliteuliwa na Hayati Magufuli. Kimsingi ni mwendelezo wa kazi, sio kitu ambacho kimekurupuka ghafla, ni mchakato wa muda mrefu wa serikali kuhakikisha tunakuwa na bandari yenye ufanisi.”

Manabii na mitume nendeni kwenye kaburi lake mkamfufue aje athibitishe kama kuna ukweli.
 
😂😂😂😂 ya ndani yanazidi kuwekwa Wazi johnthebaptist

-
“Timu ya uchunguzi [kuhusu bandari] iliteuliwa na Hayati Magufuli. Kimsingi ni mwendelezo wa kazi, sio kitu ambacho kimekurupuka ghafla, ni mchakato wa muda mrefu wa serikali kuhakikisha tunakuwa na bandari yenye ufanisi.”

Bora ungekuwa wa mda mfupi tungeona wamekurupuka. Kama ni wa muda mrefu na kuja na madudu kama haya, basi hii ni aibu kubwa kwa taifa
 
Wamuache mzee wa watu alale kama alivyolala, kama wameamua kuuza uhuru wetu kwa waarabu waache historia iwahukumu wao.

Yeye Magufuli ana yake, haya ya bandari ni maujinga yao wenyewe.
 
Tatizo tunamuona JPM kuwa ni shujaa wa taifa na tumeshalipa tafsiri potofu suala zima la DP World.

Tunadhani SSH kwa maamuzi yake mwenyewe alienda Dubai na kuingia mikataba, tunasahau kuwa hawa wawili ni wateuliwa wa chama kimoja cha siasa. Wanatekeleza ilani moja ya uchaguzi.

Tumembagua na kumtusi SSH tukisahau chanzo halisi cha huu mradi ni nani, tukashindwa hata kujiuliza gharama kubwa ya ujenzi wa SGR kwa kuilinganisha na mradi huu wa waarabu.

Siasa kuzitafakari inamtaka mtu atulize kichwa chake vizuri.
 
Wamuache mzee wa watu alale kama alivyolala, kama wameamua kuuza uhuru wetu kwa waarabu waache historia iwahukumu wao.

Yeye Magufuli ana yake, haya ya bandari ni maujinga yao wenyewe.
Hujui ulisemalo. SGR ilianza kujengwa 2015 na muda mfupi uliofuatia ndio majadiliano yakaanza juu ya biashara za DRC na Rwanda, kuhusu namna logistic chain nzima itakuwa vipi.
 
Back
Top Bottom