Hatari ya kuwalazimisha watoto wa Watu kwenda JKT!

Mkuu mafisadi wote wanaoutusumbua hapa nchini wamepita JKT. Ina maana wao hawakukunjika huko (kama unavyotoa mfano wa samaki) ili wawe viongozi wazalendo?
 
Haswaaa
 
Mkuu mafisadi wote wanaotamba ktk nchi hii wamepita JKT. Mbona hawana uzalendo, utii na faida kwa taifa? Nani kakwambia JKT ni chuo cha uzalendo na kwamba mtu anaweza kuwa mzalendo kwa kuteswa kwenye makambi haya ya kishetani kwa miezi 3 tu?
 
Huu ni uongo mtupuu, wala hakuna ukweli wowote.
 
Mkuu mafisadi wote wanaotamba ktk nchi hii wamepita JKT. Mbona hawana uzalendo, utii na faida kwa taifa? Nani kakwambia JKT ni chuo cha uzalendo na kwamba mtu anaweza kuwa mzalendo kwa kuteswa kwenye makambi haya ya kishetani kwa miezi 3 tu?
acha upotoshaji gentleman,
mafunzo ya stadi za maisha, ukakamavu, uadilifu, uzalendo na kujitegemea sio mateso please.

uvivu wako ndio umaskini wako, acha dhana potofu na visingizio nonsense dhidi ya viongozi na watumishi wa umma nchini 🐒
 
Uongoo wengi wao wanalazimishwaa.
 
JKT haina mambo mabaya kama alivyosema mwandishi. Kama unalitoto umelilea bila adabu huko linaweza fundishwa kwa kiasi chake.

Kama mtoto wako katoka 6 na unaona muda wa kusubiri kwenda chuo hana cha kufanya mruhusu aende kule.

Lakini naweza kusema JKT haina faida yeyote baada ya mtu kutoka kule,hakuna cha kujivunia na hauta apply popote.
 
Mkuu Taikon umemaliza kila kitu. JKT haina faida yoyote kwa vijana zaidi ya kuwapotezea muda na kuwasababishia mzongo wa mawazo na pia kuwaingiza wazazi kwenye gharama zisizokuwa na tija.
 
Unalalamika kuhusu wabunge wakati kioindi wanapitisha hyo sheria wao ndo walikua wakwanza, Akina zito walienda JKT kipi kipya sasa?
Kwa hiyo hoja ikipitshwa na Zitto, hata ikiwa ya kipuuzi, lazima tuikubali tu mkuu?
 
Mtoto wangu asipoenda watamfanyia nini ?
Watamnyima nafasi ya kwenda Chuo Kikuu na kumuwekea mizengwe
Kaka yangu alienda JKT akaangukia kwenye kambi ya mateso inayojihusisha na kilimo cha mpunga. Kwa bahati mbaya alijikata mguu na jembe wakati anaandaa jaruba la mpunga. Hicho kidonda kiliendelea kukua na kumtesa bila kutibiwa hadi kikageuka kuwa kidonda ndugu. Alikuja kuponeshwa na daktari bingwa kwa gharama kubwa baada ya kuhitimu mateso. Hata hivyo, baada ya kidonda kukauka, kimeacha kovu kubwa sana mguuni ambalo linamtesa kwa ganzi hadi leo. JKT ni makambi ya mateso kama yalivyo makambi ya Gwantanamo na makambi mengine ya mateso.
 
Hii mimi sikubaliani nayo kabisa
 
Si bora huku ni wahitimu wa kidato cha 6 tu nchi nyingine ni kwa kila raia ni lazima kupata mafunzo ya kijeshi bila kujali na ukithubutu kukwepa jera inakuhusu.
Katika nchi yenye mamilioni ya raia, kuwachukua wahitimu wa kidato cha sita tu kunaleta manufaa au tija gani mkuu?
 
Wewe ndiye ulipaswa kutueleza mbadala wake ambao ni better, lakini uliishia katika kulalamika tu!
Mimi nimeeleza mabaya ya JKT. Sasa wewe unayeshupaa kuwa JKT kuna "faida nyingi sana", hebu tutajie walau faida mbili zenye mashiko za kuhudhuria JKT.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…