Hawa jamaa wa Iringa chini ya Producer Ambha walitisha sana

Hawa jamaa wa Iringa chini ya Producer Ambha walitisha sana

Acha kabisa Broo, enzi hizo natoa hadithi zangu gazeti la Mwananchi, nikilipwa napeleka Pesa Studio. Ukisharekodi kumfikia Baba Wawili pale Ebony au DJ Fetty na wengine sio rahisi. Japo kwangu kilichonishinda 'Maisha yaliyo kwenye muziki' niliona siyawezi kabisa.
siwezi tu kushare experience zangu baadhi ila sekta ya burudani ina mambo ya ajabu sana. Labda uwe na kazi ya kukupa kipato au back up ya kukusogeza la sivyo utaingia kwenye mambo ya ajabu sana
 
siwezi tu kushare experience zangu baadhi ila sekta ya burudani ina mambo ya ajabu sana. Labda uwe na kazi ya kukupa kipato au back up ya kukusogeza la sivyo utaingia kwenye mambo ya ajabu sana
Mfano? But muziki si sasa unalioa? watu kama chino kid naona ndani ya muda mfupi wamebadilika.
 
siwezi tu kushare experience zangu baadhi ila sekta ya burudani ina mambo ya ajabu sana. Labda uwe na kazi ya kukupa kipato au back up ya kukusogeza la sivyo utaingia kwenye mambo ya ajabu sana
Ukweli mchungu huu

Kwa kifupi mambo yapo ndivyo sivyo na yanavyoonekana nje
 
hiyo ngoma ya country ina miezi mitatu ameifanya ammy wave
 
Ambha anadai kwamba alifanya production lakini hakutoboa akawa ameamua kufunga studio aachane na muziki maana nyimbo zilikuwa hazipigwi na hapati fedha. Sasa akiwa ashaamua kufunga studio, asubuhi kalala kaja yaki anamgongea dirishani anamwita ambha aamke kuwa kaja na faridah anataka wakarekodi. Kama mnakumbuka zama hizo faridah alikuwa ni msanii wa kike ambaye nyimbo zake kama pesa zilikuwa ikipigwa sana RFA ambayo ilikuwa kwenye peak zama hizo.
Basi ambha kusikia farida akaamuka na kwenda studio na yaki na farida ndipo wa karekodi wimbo unaitwa we ni wangu ulikuwa na beat ya crank na crank ndiyo ilikuwa mainstream.
Baada ya hapo akarekodi hits kibao hadi wasanii wakaanza kutoka dar wanamfuata iringa. Moja ya msanii aliyefanya ngoma naye ambazo mpaka leo nazikubali ni Rama Dee ambapo alifanya naye ngoma inaitwa kikao cha family na ngoma nyingine. Ambha anadai ngoma za rama dee zilikuwa zimejaa back vocal zake mwenyewe na rama dee alimkubali jamaa jinsi alivyokuwa anapika nyimbo zake.
Ila kati ya vijana ambao alifanya nao ngoma zikahit kutokea iringa ni yaki, roho saba, na vijana wengine.

View: https://www.youtube.com/watch?v=H6MWWxMkDhM&list=RDH6MWWxMkDhM&start_radio=1

View: https://www.youtube.com/watch?v=PihvQOA_gxo

View: https://www.youtube.com/watch?v=chdP7c91Qs4
Lakni my favorite ni yaki ya tonight.

Yombo za kiazi kipya bhana daah
 
Back
Top Bottom