Hawa jamaa wa Iringa chini ya Producer Ambha walitisha sana

Hawa jamaa wa Iringa chini ya Producer Ambha walitisha sana

Mkuu nililenga ambha records na marlow alitokea kwa tuddy thomas
Studio ya Amba inaitwa AB Records na pindi Marlaw anafanya bembeleza, Tuddy Thomas alikuwa Iringa records na bwana Temmy G
 
WAKONGWE MNATEMA MADINI SANA ILA OMBI LANGU NI MOJA KAMA KUNA MTU ANAYO NGOMA YA FARIDA OOH PESA NAOMBA AIWEKE HAPA NITASHUKURU SANA MTU YOYOTE AKIFANIKISHA KUIWEKA HAPA
 
Ambha alikua vizuri sana alijaribu kuiheshimisha iringa kwa wakati wake..
Kuna msanii wake mwingine alikua anaitwa E2K sijui yupo wapi yule mwamba.
Ambha Kuna kipindi alicha habari za music production akafungua bakery ameuza sana mikate akisaidiana na binamu yake kenani- Sasa hivi ni RC simiyu
Sijui kama Bado anaendelea na bakery ila sasahivi namuona Instagram amekua pastor.
E2K ni wakili wa kujitegemea na pia wakala wa wachezaji wa soka. Yupo Dar
 
Omary Kombo a.k.a KGT sasa hivi amekua Ras.

Yupo bado anafanya music Ila hakuna mainstream artist anaweza kwenda kurekodi kwake. Muda ushamua
Omary Kombo a.k.a KGT sasa hivi amekua Ras.

Yupo bado anafanya music Ila hakuna mainstream artist anaweza kwenda kurekodi kwake. Muda ushamuacha
Hivi yule jamaa hakuwa mkenya?.. nilikuwa namuona pale Kino mkwajuni/moscow ... kuna ka studio flan kilianzishwa na jamaa yangu alikuwa anakujaga kurecord... kipindi hicho kama mtu hana ndoto ya kuwa mwanamuziki basi ana ndoto ya kuanzisha studio

Sasa kuna mtu alinambiaga anatokea kenya
 
Hivi yule jamaa hakuwa mkenya?.. nilikuwa namuona pale Kino mkwajuni/moscow ... kuna ka studio flan kilianzishwa na jamaa yangu alikuwa anakujaga kurecord... kipindi hicho kama mtu hana ndoto ya kuwa mwanamuziki basi ana ndoto ya kuanzisha studio

Sasa kuna mtu alinambiaga anatokea kenya
FL studio ilileta shida sana zama hizo. Halafu sio TZ tu duniani kote vijana FL iliwasaidia sana kuweza kuwa ma beat maker. WE fikiria mwamba Allan Walker ngoma zake kali zote kazigonga via FL studio kwa kujifunz amwenyewe home na anakwambia alijaribu software zingine akaona zinazingua akarudi kwa FL. Kipindi naanza kuitumia ilikuwa ni fruity loops. Yani niliona ndicho kitu kizuri ambacho niliwahi kukiona kwenye computer.
 
Haipo. Hermy B yupo efm/etv ni mkuu wa vipindi

Nilichokuambia ni kuwa studio bongo ni uwekezaji kichaa. Studio ilifeli baada ya kuanza kulipisha wasanii tena kwa pesa kubwa(laki 7 kwa wimbo)
Ukishaanzahivuo tu Hakuna msanii wa maana atakuja na mwisho utafunga mwenyewe tu. Wasanii wanataka kurekodi bure

Uliza maswali kuhusu muziki bongo na wasanii leo nina muda mzuri, mm ndio mrithi wa ruge clouds fm😁😁😁
Sasa kama wana record bure, kina P funk, master Jay, yule mzungu producer jina limenitoka walikuwa wanapata vipi pesa.. na hawa wasanii wakubwa wana record kwao na wanaingiza pesa kina wagosi, kina Mwana Fa, kina prof J
 
amesema ameifunga record label, na kumbukumbu yangu wasanii wake wa mwisho kuwa label ni OMG na hata baada ya OMG kufa studio imeendelea kufanya kazi kama kawaida
Duh mkuu bado tu umekaza? Basi sawa ipo na inafanya kazi
 
Sasa Afande Sele kimuziki unamchukulia poa?? Unashangaa kabisa mtu kuomba ushauri kwa Mfalme wa Rhymes?
Simchukulii powa Ila sjo mtu anaweza kumsaidia mtu kimuziki na kufika mbali. Huo uwezo ndio Hana

Kuwa namba moja darasani haimaanishi unaweza kuwa mwalimu mzuri wa kufundisha wengine.

Huwezi kutaka kufika mbali kimuziki ukamfata afande sele, labda uwe unatania.
 
Tupeni mifano wa hayo mambo coz watoto wetu wanatusumbua mno! Mtoto anakuambia anataka awe kama Diamond!
Vanessa baada ya kuacha music kuna ambavyo kazungumza, alivyozungumza hakuna mtu mwingine anaweza kuzungumza kwa uwazi vile. Mimi nisikueleze chochote maana naweza kukuongopea pia. Wewe katafute you tube alivyozungumza, alafu kichukue kama kilivyo maana ndio ukweli wenyewe
 
Back
Top Bottom