Hawa ni watu waliomdhihaki Mungu na kupatwa na shida

Kikukwa cha kufahamu ni kwamba Mungu hadhihakiwi kwa namna yyt
 
Imani ni nini ?
Imani ni kukubali kitu bila uthibitisho.

Nikikubali kuwa wewe Mubarridi ni Mfalme wa Bahrain, bila uthibitisho, hiyo ni imani.

Kama kiukweli wewe si Mfalme wa Bahrain, imani hiyo kwamba wewe ni Mfalme wa Bahrain, haikufanyi wewe kuwa Mfalme wa Bahrain.

Tukichunguza na kuthibitisha kuwa kweli wewe ni Mfalme wa Bahrain, habari ya kwamba wewe ni Mfalme wa Bahrain inakuwa si imani tena, inakuwa fact iliyothibitishwa.
 
Unaamini unachoamini au umethibitisha?

Unaelewa kuwa kuamini si kuthibitisha?
Ha ha ha ha

Kwa mambo ya Mungu sihitaji uthibitisho wa kibinadamu.

Ninapoona tu kuwa mwanadamu hajaweza kuumba mtu na kumpa pumzi, hajaweza kuufanya mmea usikauke na kufa, hajaweza kuumba dunia nyingine, nathibitisha kuwa yupo mwenye nguvu kuliko wote.... Mungu.
 
Hapo ni sawa na wewe useme kwa kuwa hakuna kiwanda cha BMW Tanzania, basi BMW limetengenezwa na Mungu!
 
Imani ni kukubali kitu bila uthibitisho.
Marejeo ya hii maana ni kwa nani ? Nani amekwambia hii maana.

Sababu nikiipima kwa mzani wa maana ya maana hii maana haikai.
Nikikubali kuwa wewe Mubarridi ni Mfalme wa Bahrain, bila uthibitisho, hiyo ni imani.
Hiyo si imani. Bali umekubali jambo la uongo lisilokuwepo kwa ujinga wako.
Kama kiukweli wewe si Mfalme wa Bahrain, imani hiyo kwamba wewe ni Mfalme wa Bahrain, haikufanyi wewe kuwa Mfalme wa Bahrain.
Umerudia kile kile.
Tukichunguza na kuthibitisha kuwa kweli wewe ni Mfalme wa Bahrain, habari ya kwamba wewe ni Mfalme wa Bahrain inakuwa si imani tena, inakuwa fact iliyothibitishwa.
Sasa imani ina pande mbili uongo na kweli. Kuna imani ya kweli na kuna imani ya uongo.

Mfano mimi nina amini ya kuwa Ulimwengu umeumbwa na haujajiumba wala haujatokea pasi na chochote. Hii ni imani na ni uhalisia.
 
Imani ni nini?
 
Hapo ni sawa na wewe useme kwa kuwa hakuna kiwanda cha BMW Tanzania, basi BMW limetengenezwa na Mungu!
Sasa niambie unafikiri dunia imeumbwa na nani? Au imetokeaje?

Na wewe umetoka wapi?

Mwanadamu wa kwanza alitoka wapi? Aliibuka tu?
 
Imani ni nini?
Imani ni tamko lenye asili ya Kiarabu lenye maana ya kusadiki kwa moyo juu ya jambo yaliyo fichikana na kutamka kwa ulimi juu ua uwepo wa jambo fulani na kutenda kwayo. Yaani kuifanyia kazi imani hiyo.
 
Swali zuri, twende polepole, hatua kwa hatua.

Unakubali kwenye kufikiri kimantiki au hukubali?
Sitaki habari za mantiki katika Mungu, ha ha ha

Lakini kwaajili ya kujifunza

Shusha mistari
 
Imani ni tamko lenye asili ya Kiarabu lenye maana ya kusadiki kwa moyo juu ya jambo yaliyo fichikana na kutamka kwa ulimi juu ua uwepo wa jambo fulani na kutenda kwayo. Yaani kuifanyia kazi imani hiyo.
Kwa hiyo kabla ya Mwarabu kututawala hakukuwa na Imani!?
 
Imani ni tamko lenye asili ya Kiarabu lenye maana ya kusadiki kwa moyo juu ya jambo yaliyo fichikana na kutamka kwa ulimi juu ua uwepo wa jambo fulani na kutenda kwayo. Yaani kuifanyia kazi imani hiyo.
Imani si tamko lenye asili ya kiarabu.

Dhana ya imani ilikuwepo kabla ya kiarabu kuwepo.

Hjaelewa hata nilichokuuliza ni nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…