Hawa ni watu waliomdhihaki Mungu na kupatwa na shida

Wala tusiende Mbali Afande sele aliwahi kumdhihaki Mungu na bado tuko nae anadunda.
 
wewe jamaa ni mwongo mwongo sana Eti
Stephen Hawking alimkana huyo Mungu ndio akapata ugonjwa wa ajabu hivi hizi stori hua manazipata wapi?
Hebu Rudi kasome historia ya maisha ya huyo nguli ndio urudi hapa utupige Kamba zako!
Huwa wanazipata kwenye mahubiri ya shehe su mchungaji mtoa mapepo
 
Huwa wanazipata kwenye mahubiri ya shehe su mchungaji mtoa mapepo
Religion is Opium,
Yaani ukiwa mfuasi wa Dini lazima ukubali kua nyumbu,hivi Hawa watu wamefungwaje akili,mbona Mimi naona Kabisa Dini na Imani za Mungu,miungu,mashetani,
mapepo,mizimu,majini nk ni propaganda tu ila still Watu Bado wanaamini tu!
Daaaa Mimi nimeshindwa Hata Kwa kujilazimisha!
 
Hapa kuna funzo kubwa sana, Nami nitaongezea kisa kimoja nilichopata kusimuliwa na watu ninaowaamini.
Miaka ya hapa kati (2010-2015) kanisa moja la Anglican tena ni kanisa kuu la diocese lilikuwa linafanya sherehe za kutimiza karne moja tangu kuanzishwa kwa diocese hiyo, moja kati ya diocese kongwe hapa Tanzania.
Basi Siku hiyo kulikuwa na maandamano ya waumini na viongozi wa kanisa kutoka mahali ambapo ndipo palikuwa na kanisa la kwanza kabisa la dayosisi hiyo mpaka lilipo kanisa kuu la sasa ambalo nalo ni la zamani sana.
Basi maandamano yalikatiza mitaa ya katikati ya mji wakiongozwa na kiongozi wa maandamano aliyebeba MSALABA mkubwa wa mbao.
Waandamanaji walipofika maeneo ya katikati ya mji akatokea bwana mmoja aliyekuwa mchukuzi maarufu wa maeneo hayo kwa jina maarufu CHENGO, basi yule bwana CHENGO alicheka kwa kejeli na kutoa maneno ya kuudhihaki msalaba, alizidi kutoa maneno machafu kwa Waandamanaji na juu ya ule MSALABA MTAKATIFU.
Baada ya maandamano kupita na kuisha katika maeneo yale yule bwana alipata ajali ambayo mpaka leo hakuna ajuaye BWANA CHENGO aligongwa na chombo gani. Hakuna gari iliyoonekana kwa macho ikimgonga lakini ndiyo hivyo yule bwana akapoteza uhai siku ileile tena muda mfupi baada ya kuunanga MSALABA MTAKATIFU

Tuweke akiba ya maneno
 
Umejuaje haya yote, wakati hujawahi kufa?Yote haya uliyoandika ni mambo ya kusimuliwa tu.

kuyaelewa haya inahitaji afya nzuri ya akili kuzitafuta fact
kwanza elewa binaadmu ni muunganiko wa vitu viwili Roho na mwili
soul + body = humanbeing
pia mahitaji na maisha ya binaadamu lazima yawe hivyo kimwili na kiroho ndio maana HAKUNA KUFA BALI KUNAKUHAMA THE DEPARTURE OF THE SOUL FROM BODY
 
Unaposema inahitaji afya nzuri ya akili kuzitafuta fact una maana gani mkuu?

Na ni njia ipi unayotumia kupata facts ambayo inahitaji uwe na afya ya akili?
 
Unaposema inahitaji afya nzuri ya akili kuzitafuta fact una maana gani mkuu?

Na ni njia ipi unayotumia kupata facts ambayo inahitaji uwe na afya ya akili?

njia rahisi nikujiuliza tu ila unapojiuliza lazima uwe na akili timamu
yapo maswali kama 4 hivi na zaidi
1. Mimi ni nini ?
2 na kabla ya kuwepo hapa nilipo nilikua wapi?
3, hapa nilipo ni kwa hiyari yangu na kupenda kwangu au ni nguvu fulani ilionisukumia hapa.
4, nikitoka hapa nilipo nitakwenda wapi na kwenda kwangu itakua hiari yangu au ni nguvu fulani itakayo nisukuma huko
 

Utakuwa umshiba ukavimbiwa unaongea kwa kibri
 
Nitwaminije ya kwamba Hii kweli na si chai,je tutajuaje kama wale Watu wa Dini walimfanyia tukio Ili ionekane eti aliukashifu msalaba na amepigwa tukio na huyo Mungu,
Kisa chako kina walakini kwanza Mimi najua mbinu za hao wanaojiita watu wa Dini kutengeneza matukio Ili kuwatisha na kuwahadaa watu na Hapo wakiita ni miujiza,
Kwangu Mimi hilo tukio naona ni coisendence ya kawaida tu au Kuna figisu alifanyiwa huyo bwana ila swala la kusema ni laana au sijui miujiza nooop!
 
Kumbe unajua kuna laana na miujiza? Mimi sikuelezea hivyo
 
Kumbe huna hoja ya kuthibitisha hakuna Miungu.

Unafikiri hiyo akili ya kujua mantiki sijui nini kakupa nani? Kwanini mbuzi hawajui habari za mantiki?

Unakwepakwepa tu.

Utakuwa ulipitia magumu ndio maana unaona hakuna Mungu.
watu wasomuamini mungu hua na mtindio wa ubongo, mungu amekua jawabu la mambo mengi ambayo science wanayoitukuza imeshindwa, mfano; vipimo na matibabu ya kisayansi yanamwambia mtu hawezi kupata mtoto isipokua kwa kupandikiza bt ukija mbele za mungu utapata mtoto bila hata kupandikiza.
 
Ngoja nijibu maswali yako

1. Mimi ni mtu naye tambulika kwa majina matatu niliypewa na wazazi wangu

2. Kabla ya kuwepo, sikuwepo. Kuuliza mahali nilipokuwa wakati sipo ni contradiction

3. Hapa nipo kwasababu ya juhudi zangu za kjjiepusha na hatari zinazoweza kufanya nisiwepo, nipo hapa kwasababu cell zangu hazichachoka. Kwa hiyo hakuna nguvu yeyote inayonisukuma

4. Nikitoka hapa kwa namna gani? Kama una maanisha kufa, basi jibu ni simple, kilichokufa hakiwezi kufanya movements yeyote ya kwenda sehemu nyingine, labda kama unakusudia kuzikwa

Kwa hiyo hayo maswali ulivyokosa majibu ndio yalikusababisha mpaka ukaamini Mungu?
 
wewe jamaa ni mwongo mwongo sana Eti
Stephen Hawking alimkana huyo Mungu ndio akapata ugonjwa wa ajabu hivi hizi stori hua manazipata wapi?
Hebu Rudi kasome historia ya maisha ya huyo nguli ndio urudi hapa utupige Kamba zako!
Wewe ndio ukatafute historia yake ujifunze vizuri
 
Kumbe huna hoja ya kuthibitisha hakuna Miungu.

Unafikiri hiyo akili ya kujua mantiki sijui nini kakupa nani? Kwanini mbuzi hawajui habari za mantiki?

Unakwepakwepa tu.

Utakuwa ulipitia magumu ndio maana unaona hakuna Mungu.
Mimi nina hoja ya kuthibitisha Mungu hayupo

Kwasababu mimi ndio Mungu wa kweli na Mungu unayemdhania wewe sio wa kweli hayupo

Unabisha?

Kama unabisha thibitisha mimi sio Mungu wa kweli
 
Wala tusiende Mbali Afande sele aliwahi kumdhihaki Mungu na bado tuko nae anadunda.
Walisema ameomba radhi ila baada ya kusikia kuna njama za watu kumfata na mapanga usiku

So wangemkata na mapanga halafu wanegekuja na kauli kua ni laana ya Mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…