Haya matukio yamenifanya nijitafakari upya tabia zangu

Kwani ukifa ndani kuna shida gani? Hata ukifia Ikulu hakuna kinachobadilika, Je wale wanaokufa katika ajali za maji na hawaonekani?
 
Kuwa introvert sometimes ni shida sana,Mimi nipo hivyo ni introvert na hali hiyo ilinitesa sana wakati nipo shule na chuo,kuna mazingira yalinilazimu tu nichangamke japo nilishindwa kabisa.Huwa napenda kukaa ndani sana,nikitoka basi jua limeshazama na huwa sichelewi kurudi.Upande wa mahusiano kiukweli nilipitia break up ambayo ilinitesa sana huko nyuma kiasi kwamba moyo umekua mzito hata kuwa na mazoea na wanawake,huwa tunapiga stori lakini ule ukaribu wa kuwa close ndio sina.Pamoja na yote hii hali ya kuwa introvert imenisaidia kusave sana pesa na kufanyia vitu vya kimaendeleo na kujipanga zaidi kimaisha.Na sikuhizi najitahidi kusoma baadhi ya vitabu pdf kuhusu mambo mbalimbali ambayo mwanzoni sikuyajua,love,saikolojia nk,nahisi inanilazimu kuwa na mtu ila introvert linapokuja suala la kuchagua wapenzi au marafiki wa kuwa nao ni mtihani sana,mara nyingi tunapenda kuwa na watu ambao angalau wanafanana na sisi ila hatuwapati na mbaya zaidi watu wengi huwa wanachukulia introvets ni udhaifu wa mtu,looser,ndio maana hata mnapokuwa ktk group flani watu huwa wanatuignore zaidi introvert.Nipo na 28 yrs inanilazimu sasa kujichanganya tu kutafuta patner [emoji38]
 
Mi bora niishi na yeyote kuliko peke yangu.
Kuna wakati unashikwa hata simu washindwa ifata uwataarifu watu wakusaidie.

Utoto unawasumbua wengi
 
So sad [emoji20], lakini kukaa peke yako kuna vibe ambayo haielezeki . Mm binafsi sipendi kujichachanganya na watu, hata wakija washkaji kunitembelea huwa natamani mda uende waondoke . Sijui kama n tatizo lakini huwa napenda sana kua mwenyewe
 
Kifo ni kifo tuu mkuu, ikitimia hayo yote hayana umuhim.
 
Huu uzi unafundisha sana, niliwai kusoma makala moja kutoka ulaya uko, kuna dada alikuja kugundulika kama kafa baada ya miaka miwili polisi walikuta mifupa ndani sababu ndio iyo iyo ya kujifungia ndani kuishi maisha ya umimi. Bila shaka wale wabinafsi uzi huu utawafundisha kitu
 
Akina Da'Vinci hao....ukiwaona jf wanaandika magazeti utajua waongewji. Yaani mazungumzo namtu lazima aboreke tu maana lete Habari, sawa haina shida zinakua nyingi sana😟
 
Kikubwa uwe na watu mnaojuliana hali time after time, mimi hii hali kuna muda inanitokea najikuta naenda kazini nikitoka ni kujifungia mpk siku ya pili na sometimes mood inanituma nisiende job siku ya pili nazima tu simu au naweka kindege nalala sema kuna wanangu wa job wakiona hivyo lazima wafike home kunikurupusha

Sent from my OPPO F1S using JamiiForums mobile app
 
A
Aisee Mkuu kama upo Dom Town em tuwe marafiki maan naona una Slogan kam zangu kabisa
 
Kuna uzi mmoja upo humu nilishawahi kuwaonya maintrovert kuhusu kujitenga sana

Sasa hivi kila mtu introvert Aaaaagh !

Alafu imekuwa ni Kama sifa
 
Kuna uzi mmoja upo humu nilishawahi kuwaonya maintrovert kuhusu kujitenga sana

Sasa hivi kila mtu introvert Aaaaagh !

Alafu imekuwa ni Kama sifa
Sometimes hua nashawishika kuamini kwamba wengi walio katika huu mtandao ni introvert. Ndio maana sio wote wanaweza kuendana na mtandao huu. Since it's anonymous Platform mtu anaweza kujifanyia maujinga yake bila kujulikana. Hapo ndio utakuta watu wanaigiza kua waongeaji sana ila kiuhalisia sio waongeaji. Okopa sana wanaojifanya wakimya humu ndio hua waongeaji saaaana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…