Leo tuna akina Abdul ambao utawaona na kina Mseven huko wakiwakilisha Watanzania na wakati huo huo hawajulikani wananafasi gani hapo serikarini
Watoto wa Magufuli na familia yake kwa ujumla walifundwa siyo siri
Baba yao alikuwa kiongozi mkuu wa nchi hii, lakini niseme ukweli kuwa, sikuwahi kuwaona kwenye Hafla, Ikulu wala kwenye mkusanyiko wowote wa viongozi wakiwa kama watoto wa Rais
Haya ndiyo maadili twapaswa kuwajengea watoto wetu
Mtu unapata nafasi ya Kuongoza nchi, watoto wako nao unataka wawe viomgozi? Haya sidhani kama ni maadili ya kiuongozi!
Ofisi tumpe Rais, watoto nao tuwe tunawahudumia kama viongozi wetu? Watuhoji kwa nini tumechelewa ofisini?
Hii hapana
JPM apewe mauwa yake kwa maadili ya familia yake!