Leo tuna akina Abdul ambao utawaona na kina Museveni huko wakiwakilisha Watanzania na wakati huo huo hawajulikani wana nafasi gani hapo serikalini
Watoto wa Magufuli na familia yake kwa ujumla walifundwa siyo siri
Baba yao alikuwa kiongozi mkuu wa nchi hii, lakini niseme ukweli kuwa, sikuwahi kuwaona kwenye Hafla, Ikulu wala kwenye mkusanyiko wowote wa viongozi wakiwa kama watoto wa Rais
Haya ndiyo maadili twapaswa kuwajengea watoto wetu
Mtu unapata nafasi ya Kuongoza nchi, watoto wako nao unataka wawe viomgozi? Haya sidhani kama ni maadili ya kiuongozi!
Ofisi tumpe Rais, watoto nao tuwe tunawahudumia kama viongozi wetu? Watuhoji kwa nini tumechelewa ofisini?
Hii hapana
JPM apewe mauwa yake kwa maadili ya familia yake!
Tunapozungumzia maadili ya kiuongozi na kuondoa sintofahamu ya familia za viongozi wetu kufanya watoto wao wawe frontline kiasi cha kwamba nao ni viongozi wetu, tungependa kuwa Taifa la namna gani,?
Taifa la kichief na kifalme? Au ni taifa linalofuata taratibu na sheria za nchi?
Tumpigie kura mtu fulani, badala yeye tu kuwa ndiye kiongozi na anayepaswa aheshimiwe, badala yake kunakuwepo na watoto wake tena ambao nao anataka wewe sehemu ya uongozi wake na nusu ya heshima yake, ipelekwe pia kwa watoto wake!
Je, hakuna utata wowote mtoto wa Rais kuwa sehemu ya kiuongozi?