dudus
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 25,370
- 57,943
... very shallow! Hivyo vita vya ufisadi, madawa, n.k. alienda kuvipigani Angola? Ghana? Egypt? Au wapi huko? Mwl. Nyerere msimamo wake ulikuwa waziwazi, hatutakuwa huru hadi Afrika yote iwe huru na kilichofuata bada ya hapo kinajulikana; Tanzania iligeuka pepo ya wapigania uhuru kuanzia wale wa Msumbiji, Angola, Zimbabwe, South Africa, n.k. Tulishuhudia vikosi vikipelekwa mstari wa mbele; uliwahi kumsikia Brigedia Mosses Nnaye? Alikuwa nani?SHUJAA- ni mtu anaeshinda jambo fulani, mfano vita au ni mtu anaelikabili jambo lolote kwa ujasiri bila woga, mfano kudhiti ufisadi, madawa na nk..
magufuli anatajwa shujaa wa afrika coz kwa kipindi hiki hakuna rais afrika alieweza pigana kishujaa vita za kifisadi, madawa na nk.. kumfikia yeye.
Nyerere alipingana na madikteta wa Afrika sio tu kwa maneno bali aliwapa support wapinzani wao kuanzia kule Zaire, Malawi, Uganda na kwingineko. Umewahi kumsikia Profesa Wamba dia Wamba? Unzao habari Yoweri Museveni alisoma UDSM miaka ile ya 70 Uganda ikiwa chini ya dikteta Idd Amin?
Umewahi kusoma kitabu cha "How Europe Underdeveloped Africa"? Unamfahamu mtunzi wake? Uliwahi kujua Profesa Walter Rodney alikuwa profesa UDSM miaka ile ya harakati; enzi za Mwalimu?
Contribution ya Mwl. kwa Afrika haielezeki na wala haukna wa kufanana naye nchi hii! Huyo ndiye shujaa wa Afrika! OKW BOBAN SUNZU