He! Kumbe Quran nayo ilipangwa vitabu, Machapisho na Ayyah zake na binadamu kama ilivyo kwa Biblia

He! Kumbe Quran nayo ilipangwa vitabu, Machapisho na Ayyah zake na binadamu kama ilivyo kwa Biblia

Shalom, Salam alaikum.

Baada ya kusoma Biblia kuanzia Genesis Hadi Revelation nikaamua kuanza kusoma pia Quran (Mwaka huu).

Ila Huwa napenda kufahamu chanzo, uandishi Hadi uwasilishaji wa kitabu kabla ya kuanza kukisoma kitabu hicho (Napima uzito).

Na Hiki ndicho nilichogundua kwa upande wa chanzo cha Quran.

Vitabu vya Quran vilivyokuwa vimeandikwa kabla ya kifo cha Mtume Muhammad vilikusanywa na kuunganishwa kuwa kitabu kimoja baada ya kifo chake. Mchakato huu ulifanywa hasa na makhalifa wawili wa mwanzo, Abu Bakr na Uthman ibn Affan. Hapa kuna muhtasari wa hatua muhimu katika uunganishaji wa Quran:

1. Wakati wa Uhai wa Mtume Muhammad: Wakati Mtume Muhammad alikuwa hai, wahyi wa Quran ulipokelewa na kuandikwa na wafuasi wake kwenye nyenzo mbalimbali kama vile ngozi, mifupa, na majani. Wengi walikuwa pia wameuhifadhi katika akili zao.

2. Mchakato wa Abu Bakr: Baada ya kifo cha Mtume Muhammad mwaka 632 CE, baadhi ya wafuasi ambao walikuwa wamehifadhi Quran kwa kuikumbuka waliuawa katika mapigano. Khalifa wa kwanza, Abu Bakr, alihofia kwamba wahyi huo ungepotea, hivyo akaamuru uandikaji wa Quran kuwa kitabu kimoja. Zayd ibn Thabit, mmoja wa wahitimu wa Mtume, aliteuliwa kukusanya na kuandika vipande vya Quran kutoka kwa vyanzo mbalimbali.

3. Uthman na Usawazishaji: Baadaye, chini ya utawala wa Khalifa Uthman ibn Affan (644-656 CE), aliona kwamba katika maeneo mbalimbali kulikuwa na tofauti za usomaji na maandiko. Ili kuleta usawa, Uthman aliamuru kutengenezwa nakala rasmi ya Quran na kupeleka nakala hizo katika maeneo tofauti. Nakala nyingine zilisitishwa ili kuepuka tofauti.

Mchakato huu wa uunganishaji na usawazishaji ulihakikisha kwamba Quran iliifadhiwa katika fomu moja na inayoaminika hadi leo, kulingana na imani ya Kiislamu.
Aliyesema kuwa ilishusha alikuwa ana uelewa finyu kwa kudhani kuwa mbinguni ni huko anga za juu
 
Sidhani kama kitabu hiki kinaukamilifu haswa pale ninapovuta picha kwamba Kuna baadhi ya vitabu viliondolewa na binadamu Uthman aliondoa baadhi ya vitabu (editing) na kubakisha anavyovipenda ye 🧐🧐🧐
Uongo na uzushi Quran haina editing ina publication tu,usitafute ulinganifu wa kasoro na vitabu vyengine Quran haina kasoro
 
Mzee nahisi kama shule ulienda kuzuga tu, kuna baadhi ya vitu vinadecay na kupotea mazima kama magome ya miti na material yanayofana nayo, ko ni ngumu kuihifadhi vitu namna hiyo hasa kwa jamii za wakati huo na kingine hiyo Quran inashauriwa kuzika aina yoyote ya material yaliyotumika kuhifadhia Quran kimaandishi ili isije kudhalilishwa kwa kukanygwa, kutapakaa mitaani na mwishowe ikapatwa na uchafu.

We endelea kugoogle maelezo kutoka kwenye vyanzo vyako, mi nipo tayari kupoteza mida kudibunk hoja zako za kitoto mpaka utakapomaliza kugoogle.
Document ya muhimu kama Quran ya Uthman haiwezi kupotea bila kubakia hata traces kidogo kama kweli ilikuwepo.

Quran ni centre ya maisha ya watu wa uarabuni,ni kila kitu kwao . How come walishindwa kuitunza na kubakisha hata baadhi ya copies pages? Kutoka Baghdad, Mecca, Medina mpaka Damascus ni bila bila.

Unaongelea documents kuoza mbona Yemen manuscript ya Quran ni ya zamani kuliko Mohamed na imepatikana ikiwa buried kule Yemen?

Unaweza nitukana lakini ukiuliza maswali magumu ni kwamba uthman Quran haijawahi kuwepo. Jinsi ilivyokuwa ya muhimu waislam wasingeshindwa kuitunza katika miji yote hiyo mikubwa . Qur'an ya mwaka 1924 kutoka Cairo sio ya Uthman.
 
Naona wewe umeelewa logic yangu, maana ushahidi unasema ali-edit vitabu vya Quran na baadhi ya maandishi akayaharibu yasije kuleta taharuki.

Sasa kumbe kuna baadhi ya vitabu vya Quran viliharibiwa aidha kwa maksudi au bahati mbaya.
This is true kitabu cha Quran kilikua compiled hundreds of years ago baada ya kufa Muhammad mimi nilishania hakiwahi kuguswa
 
Acha kujitoa ufahamu, we ndo uliuliza na kusema kuwa Allah baada ya kuteremsha Quran hakuteremsha tena wahy, mi nimekujibu kwa kukupa maana ya wahy na Quran na tofauti zilizopo baina ya vitu hivyo viwili.

Na kingine mtume alipofariki aliacha litabu kinachoitwa Quran "nimekuachieni vitu viwili hamtapotea kamwe kama mkivishika(mkivifuata) kitabu cha mwenyezi mungu (Quran) na sunnah"

Naomba uniletee ushahidi kuhusu hoja yako ya mtume kutoiacha Quran wakati anafariki.
Mohamed mwenyewe alikuwa anasahau verse za Quran, sembuse wafuasi wake shehe? Bukhari 5038.
 
Uongo na uzushi Quran haina editing ina publication tu,usitafute ulinganifu wa kasoro na vitabu vyengine Quran haina kasoro
It was edted na Othman bro soma vizuri mbona hii issue ilishazua mjadala mkubwa duniani na mpaka Imams and Scholars wa kiislam wakawa kwenye Taharuki
 
Tafuteni hii on YouTube ambayo ilizua mjadala "The Standars Narrative has holes in it" ilikua interview kati ya Sheikh Yasssir Qadhi na Muhammad Hijab hii interview ilivyofanyika yaani it caused an uproar na hii ikafanya ongezeko la apostate ndani ya Uislam
 
Acha kujitoa ufahamu, we ndo uliuliza na kusema kuwa Allah baada ya kuteremsha Quran hakuteremsha tena wahy, mi nimekujibu kwa kukupa maana ya wahy na Quran na tofauti zilizopo baina ya vitu hivyo viwili.

Na kingine mtume alipofariki aliacha litabu kinachoitwa Quran "nimekuachieni vitu viwili hamtapotea kamwe kama mkivishika(mkivifuata) kitabu cha mwenyezi mungu (Quran) na sunnah"

Naomba uniletee ushahidi kuhusu hoja yako ya mtume kutoiacha Quran wakati anafariki.
Unauhakika mtume aliacha kitabu cha quran..hebu acha uongo..Hayo maneno nimekuachieni vitu viwili..aliyatamka akiwa mahututi au akiwa ameshakufa tayari..unajua kuna vitu havi make sense kabisa.
 
Document ya muhimu kama Quran ya Uthman haiwezi kupotea bila kubakia hata traces kidogo kama kweli ilikuwepo.

Quran ni centre ya maisha ya watu wa uarabuni,ni kila kitu kwao . How come walishindwa kuitunza na kubakisha hata baadhi ya copies pages? Kutoka Baghdad, Mecca, Medina mpaka Damascus ni bila bila.

Unaongelea documents kuoza mbona Yemen manuscript ya Quran ni ya zamani kuliko Mohamed na imepatikana ikiwa buried kule Yemen?

Unaweza nitukana lakini ukiuliza maswali magumu ni kwamba uthman Quran haijawahi kuwepo. Jinsi ilivyokuwa ya muhimu waislam wasingeshindwa kuitunza katika miji yote hiyo mikubwa . Qur'an ya mwaka 1924 kutoka Cairo sio ya Uthman.
kwenye paragraph ya pili, hifadhi kubwa ya Quran ni kupitia watu.

Kwenye paragraph ya tatu, Muhammad ni wa kwanza then ikafuata Quran kwa sababu Muhammad ndio ameteremshiwa Quran, ko haiwezekani ianze Quran halafu ije Quran, sijui umenielewa we mbumbumbu much knower.

Kama utafanikiwa kukifahamu kiarabu au omba kwa mtu akueleweshe, kwenye kurasa za mwanzo kabisa za kila mas'hafu kuna maelezo ya chapa ya Quran kuwa imenakiliwa kutoka katika maandishi ya uthman, mas'hafu zote zipo hivyo iwe imechapishwa kutoka misr, saudia, uhindi, Qatar, Ethiopia na kwingineko.

We huwa unatoa wapi huu ujinga!
 
Mohamed mwenyewe alikuwa anasahau verse za Quran, sembuse wafuasi wake shehe? Bukhari 5038.
Tatizo we husomi, huwa unaenda Google unaandika sehemu unayoitaka, mfano Muhammad alisahau Quran unasearch ko majibu yoyote wanayokupa we unatupestia huku.

We ni mkubwa kwangu ila ni mjinga zaidi yangu!
 
Unauhakika mtume aliacha kitabu cha quran..hebu acha uongo..Hayo maneno nimekuachieni vitu viwili..aliyatamka akiwa mahututi au akiwa ameshakufa tayari..unajua kuna vitu havi make sense kabisa.
Kwa kukusaidia tu naona we umeshindwa aidha kuuliza au kuelewa maana ya Quran na mas'hafu!
 
Kwa kukusaidia tu naona we umeshindwa aidha kuuliza au kuelewa maana ya Quran na mas'hafu!
Hapana wewe ndio umeshindwa kuelewa ,mi hoja yangu hapa ni kuwa Muhammad mpaka anakufa hajaacha kitabu kinachoitwa quran
 
Aliyesema kuwa ilishusha alikuwa ana uelewa finyu kwa kudhani kuwa mbinguni ni huko anga za juu
Kwahiyo umeamua kukazia?..... Hebu tukisome kitabu hiki kwanza.
 
Uongo na uzushi Quran haina editing ina publication tu,usitafute ulinganifu wa kasoro na vitabu vyengine Quran haina kasoro
Enzi hizo hakukuwa na publication na kama unabisha nikuulize, Je ni nani aliipublish Quran tukufu?
 
This is true kitabu cha Quran kilikua compiled hundreds of years ago baada ya kufa Muhammad mimi nilishania hakiwahi kuguswa
Kiliguswa mara nyingi TU ata kabla Uthman hajakusanya nakala zilizosalia na kuunda Quran Moja.
 
Back
Top Bottom