Heche Aache Janja Janja . Ajibu Mpaka Sasa Amepokea Kiasi Gani Cha Pesa Kupitia Akaunti yake Binafsi na Zipo Wapi?

Wewe si ni Chawa wa mama Samia Suluhu Hassan, kweli au siyo kweli...?

Mambo binafsi ya John Heche wa CHADEMA, hasimu wenu mkuu kisiasa yanakuhusu nini..?

Anyway, let's forget about that. Tukujibu tu upuuzi wako huu...

Principle kubwa kuhusu tuhuma zozote za mashitaka inataka anayetuhumu ndiye athibitishe tuhuma zake kwa vielelezo vya ushahidi...

Sasa, unaweza kuanza kuthibitisha tuhuma zako kwa kujibu maswali haya kama mwongozo wako;

✓ Hizo pesa John Heche alizipokea toka kwa nani
✓ Ilikuwa lini
✓Kiasi gani
✓ Zikaingia Benki Account ipi na Benki gani
✓ Muulize mweka pesa hizo aseme alimpa John Heche kwa ajili ya nini. (Hili ni swali la kijinga lakini kwa kuwa mmeamua kuwa wajinga na wendawazimu, jitahidi uulize tu)
✓Nini mahusiano ya mtoa pesa na mpokea pesa hizo (iwapo tu ni kweli)

#All in all, nyie wenyewe mnasema kuwa hizo pesa (kama ni kweli zipo) ziliingizwa kwenye personal bank account. If that's the case, hiyo audacity ya kuulizia ulizia na kufuatilia pesa za mtu binafsi mmeitoa wapi? Huu ni ustaarabu wa wapi?

#Ni kweli Personal Bank Account ya mtu inaweza kuchunguzwa iwapo tu inashukiwa kupokea na kutoa pesa isiyo halali, au mwenye Account anashukiwa kuwa anatakatisha pesa nk. Hii haifanyiki kijinga na kienyeji kama mnavyofanya nyie Chawa wa hayawani bali hufanyika kwa kufuata utaratibu wa kisheria kwa vyombo vyenye mamlaka ya kisheria kuchunguza.

#Hiki mnachofanya tunajua ni personal political assassination/attack mkijaribu kumwingiza John Heche kwenye kashfa kama zenu. Lakini fahamuni kuwa hii inaweza kuwageukia na kuwa jinai na mkashitakiwa kwa character defamations na kumlipa jamaa pesa nyingi sana kwa sbb ni tuhuma ambazo hamuwezi kuzithibitisha popote iwe kisiasa au kisheria...
 
Nani aliwapa namba ya akaunti? Kwanini sasa amesema wachangie kwenye chama baada ya kelele nyingi kupigwa? Je bila kelele angepokea hela hizo mpaka lini?

Kwani wale ambao walimchangia mwenyekiti wenu kwa ajili ya kampen za uchaguzi ela alipeleka kwenye account ya chama?

Boss wenu wale ngombe anaopewa mikoani uwa anawapeleka BOT?

Waliotuma kwa account yake walitaka ela ziwe zake

Na wanaotaka ela ziwe za chama then wanajua wapi pa kupata account na utaratibu wote

And best kuliko yote hizo hela sio za kodi, wala sio za serikali, ni hela za mahaba ya watu kwake,

Kwani ww leo mtu akiwa anakoshwa na pumba zako unazoandika hapa na akaamua akupe lunch utasema apeleke ccm?
 
Hii ni kashfa kubwa sana ya utakatishaji fedha
Vipi zile bilioni 133 za EPA zilichotwa benki kuu na kutengenezewa kampuni feki 20 kumbe zimeenda kwenye kampeni za CCM 2005 hadi Mkapa akaandika kwenye kitabu chake haukua utakatishaji na kashfa kubwa jinga lao?

 
Kwa hiyo Chadema imeiga madhaifu ya CCM?
 
Mwambie M.kiti wako wa chama aache janjajanja ya kishamba kabla haja mshauri au hajataka kuona mlanayefanya sahihi akikosea ama akojaribu kuelekezwa uelekeo wa chawa wasiojielewa
 
Kwa hiyo Chadema imeiga madhaifu ya CCM?
Wapi nimesema CHADEMA imeiga madhaifu ya CCM..

Skendo ya EPA imethibitika kiliibwa kiasi gani na nani alihusika na zilienda wapi.

Hii ya Heche hadi sasa mmeshindwa kujibu maswali muhimu.

Heche kaiba kiasi gani?

Wadau hao mnaodai walimtumia pesa ni akina nani .?

Uthibitisho wa kiasi alichotumiwa na kiasi ambacho alifuja kwa matumizi binafsi kama wanavyodai ni kiasi gani?

Kwanini hao wadau hawajitokezi wao tunaona kelele za chawa tu ?

Jibu hayo maswali tuendelee jinga lao.
 
Kuna sehemu kasema CHADEMA imeiga udhaifu wa CCM... Angalia jibu lake kwa muktadha wa hoja aliyokuwa anaijibu.
Naam, umemjibu vyema kabisa nashangaa anasema habari za kuiga na mimi sijaonyesha popote mambo ya kuiga.

Nimeonyesha wizi wa EPA ulithibitika pasina shaka hivyo na wao kama wanataka kusema Heche kaiba waje na data kama alivyotoa Mkapa waache kuzunguka .
 
Maana yeye funaku kaleta mambo ya utakatishaji fedha wewe ukamuonesha utakatishaji fedha huwaje kwa kutumia mfano wa fedha za EPA.

Sasa hizo fedha alizotumiwa Heche ni lini zilikuwa chafu mpaka zisafishwe kwa kuwekwa kwenye akaunti ya Heche?
 
Kwani m.kiti wako amesha kuambia ngapi amekulakwa urefu wa kamba,Na ngapi za kumjia kama hongo na ngapi za kujipendekeza?Ama ngapi ni mnyororo wa kifisadi,na rushwa ya kimkakati?
 
Maneno mengi na tutaendelea kumchangia Mh. Heche mpaka mtapike. Mbogamboga pumzi imekata
 
Mtu unakuta mamake anaugulia vidonda vya umasikini kijijini, halafu anakuja hapa eti tumchangie hechee..

Wazazi wako wameshndia mgagani bila hata ugali tu wa uwele, leo unapanua vidole eti tonetone, halafu heche anaenda kubetia!
Na tutachanga ale na mademu zake mpaka mshangae. Naweza kumwongezea mdogo wangu wa kike hata akitaka kuongeza
 
Maana yeye funaku kaleta mambo ya utakatishaji fedha wewe ukamuonesha utakatishaji fedha huwaje kwa kutumia mfano wa fedha za EPA.

Sasa hizo fedha alizotumiwa Heche ni lini zilikuwa chafu mpaka zisafishwe kwa kuwekwa kwenye akaunti ya Heche?
Sawia kabisa.

Pesa za EPA zilitakatishwa kwa kuunda kampuni feki za mataifa 20 kumbe zinatakatishwa bilioni 133 kwenda kutumika kufanyia kampeni CCM 2005 na hili Mkapa mwenyewe alithibitisha.

Sasa huyu jinga lao anasema Heche ametakatisha pesa ambazo hawataji ni kiasi gani , alitumiwa na nani na kwa kazi gani na yeye kazitakatisha kwenda kufanyia nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…