Heche, dawa ya tuhuma sio wanawake kukufariji ni kujibu tuhuma na kupisha uchunguzi

Kuweni na ngozi ngumu kama Samia, mbona mnafukuza kila anaekosoa viongozi?
kuvuliwa madaraka sio kufukuzwa. Kwani sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam amefukuzwa kwenye dini yake kwa uzinzi?
 
Screenshot_20260714-183814~2.png
 
Kama ni hivyo nyinyi CCM na tuhuma kibao za ufisadi, ubadhirifu wa mali za uma, uuaji, utekaji,wizi n.k mngekua mmeishapisha kitambo sana.
 
Hakuna mwanacha isipokuwa nyie CCM ndio mnatumia njia za kitoto kuyatafuta maridhiano kwa kutumia pesa za walipa kodi kumchafua heche kwa sababu hataki maridhiano mpaka lisu atoke jela
Hata CCM nao huwa wanasema hivyohivyo kwa kila anaewakosoa. Kila anaeikosoa ccm ni mpinzani. Chadema kumbe nao ni hayohayo tu.
 
nenda kawajibu wanachama wa CCM wanaohoji utekaji na mauaaji yaanayofanywa na serikali yao ya CCM
Hii ni sawa na kusema cdm hawakerwi na tabia za ccm bali wanakerwa na njaa zao tu. Huwezi kuniambia kama Heche akiwa Rais hatalitumia jeshi dhidi ya CCM kubaki madarakani, no no no, tena hali itakuwa mbaya sana. Wacha survival of the fittest ichukuwe mkondo wake.
 
Tuhuma hazipigwi rungu. Charity begins at home, mpende jirani yako kama unavyoipenda nafsi yako.

Hawa wanawake wanasema, tuhumu na kutaja watu bila kutoa ushahidi mbele ya Heche. Demokrasia ndani ya vyama ndiyo inayozaa demokrasia serikalini. Unapotuhumiwa dawa ni kujisafisha kwa kupisha uchunguzi badala ya kuita wanawake wakusafishe.

View: https://youtu.be/T_uWhOHGAKA?si=qPQA8_iodS_1Q8YX

Mkuu Kavulata, hoja yako hapa haina mashiko ya kitaaluma (academic merit), inakiuka misingi ya sheria, na inaegemea upande mmoja kimantiki.

Unaposema "tuhuma hazipigwi rungu" huku ukitaka mtuhumiwa apishe uchunguzi kabla ya kubainika na hatia, unakiuka misingi mikuu ya utawala wa sheria, kanuni ya Presumption of Innocence, na msingi mkuu wa kisheria wa Burden of Proof (Mzigo wa Ushahidi). Duniani kote, kanuni ya dhahabu inasema: “He who alleges must prove” (Mwenye kutuhumu ndiye mwenye jukumu la kuleta ushahidi). Huwezi kuamka asubuhi na kutupa tuhuma za kijamii zisizo na thibitisho thabiti (substantive evidence), kisha ukadai mzigo wa kujisafisha uende kwa mtuhumiwa. Hiyo siyo sheria wala demokrasia, bali ni mob justice ya kisiasa inayolenga kufanya tabia ya kuua wahusika kisiasa (character assassination).
Kama kweli unataka kutumia kipimo hicho unachokipigania kama benchmark ya uwajibikaji, hebu tuiangalie serikali yako na mfumo wa chama tawala kupitia mifano halisi:
  1. Ufisadi wa Kimfumo (Systemic Graft): Tuhuma ngapi nzito za mikataba mibovu ya rasilimali, ubadhirifu wa fedha za umma, na ufisadi ulioripotiwa mara kwa mara na CAG zimeelekezwa kwa vigogo wa serikali na hakuna kiongozi hata mmoja wa CCM aliyetakiwa kukaa pembeni? Mbona huko hamuombi Burden of Proof ifanye kazi yake?
  2. Kuvunja Misingi ya Demokrasia: Baada ya mtikisiko mkubwa wa kisiasa na kisheria ulioambatana na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025—ikiwemo ripoti rasmi zilizobainisha mamia ya vifo vya raia na matumizi mabaya ya nguvu ya vyombo vya dola—ni kiongozi gani wa ngazi ya juu wa serikali au CCM aliyewajibika au kupisha uchunguzi wa kimataifa?
Mbona katika skandali hizi kubwa zenye athari za kitaifa mfumo mzima wa dola unajipanga kuwalinda watuhumiwa? Unaponyamazia makosa makubwa ya kiuongozi ndani ya serikali ya CCM lakini ukakimbilia kushupalia tuhuma nyepesi zisizo na mashiko upande wa pili, huu unakuwa ni undumilakuwili wa wazi (sheer double standards).
Rai yangu kwa Wana-JamiiForums:

Ni lazima tuchukue hatua za makusudi kuinusuru JamiiForums ili isirudi nyuma na kuwa jukwaa la upashkaji na majungu. Mtandao huu ulizaliwa kama Think Tank mbadala ya Great Thinkers nchini. Ni aibu kuu kuacha mijadala ya kitaaluma na kimkakati ishushwe hadhi na MACHAWA wa CCM ambao wanajaza kurasa za jukwaa hili kwa propaganda nyepesi na habari za kutungwa kwa lengo la kusafisha mabwana zenu. Turudishe jukwaa hili kwenye misingi yake ya uchambuzi wa kina na hoja zenye mashiko ya kisayansi na kiintelijensia!
 
Ukiwajibu wapumbavu na wewe utakuwa mpumbavu
 
Tuhuma hazipigwi rungu. Charity begins at home, mpende jirani yako kama unavyoipenda nafsi yako.

Hawa wanawake wanasema, tuhumu na kutaja watu bila kutoa ushahidi mbele ya Heche. Demokrasia ndani ya vyama ndiyo inayozaa demokrasia serikalini. Unapotuhumiwa dawa ni kujisafisha kwa kupisha uchunguzi badala ya kuita wanawake wakusafishe.

View: https://youtu.be/T_uWhOHGAKA?si=qPQA8_iodS_1Q8YX

Siku zote mchezaji mwenye mpira ndiye anakabwa, maccm wote nchi nzima mnamuandama Heche tu, hakika huyu Mkurya amewakwama kooni sasa hivi kumeza hamuwezi na kutema hamuwzi. Heche komaa nao hawa mbogamboga hadi wakate pumzi kabisa .
 
Walishazoea siasa mdebwedo na kujiamulia mambo.Wapambane kwa hoja na majukwaa huru tuwatambue uwezo wa kufikiria kwao unapoishia.
 
Ameomba watu binafsi wamchangie fedha ya kuendesha kampeni na kuzipokea yeye kwa acount yake binafsi bila kuziwasilisha kwanza kwa kwa wanachadema
Hao watu ni akina nani?

Wewe ni miongoni mwa hao watu?

Hao "watu" hawana majina?

Hao watu walimchangia kiasi gani?

Hao watu kwanini wasije wao kusema hizo pesa aliwaomba lini na kwa sababu zipi au wamekufa?

Hao watu kwanini walimtumia pesa kama mnavyodai ni za chama kwenye account yake na si account ya chama ? Je asiyejua hapo taratibu za kiofisi ni hao watu au ni Heche?
 
Inaonekana waliokutuma hawajakusugua vizuri. Nenda kasuguliwe kisawa sawa, yawezekana akili yako itarudi mahala pake.
Kwa taarifa yako, Heche ni Dhahabu ya Watanzania.
 
Mkuu Kavulata, hoja yako hapa haina mashiko ya kitaaluma (academic merit), inakiuka misingi ya sheria, na inaegemea upande mmoja kimantiki.

Unaposema "tuhuma hazipigwi rungu" huku ukitaka mtuhumiwa apishe uchunguzi kabla ya kubainika na hatia, unakiuka misingi mikuu ya utawala wa sheria, kanuni ya Presumption of Innocence, na msingi mkuu wa kisheria wa Burden of Proof (Mzigo wa Ushahidi). Duniani kote, kanuni ya dhahabu inasema: “He who alleges must prove” (Mwenye kutuhumu ndiye mwenye jukumu la kuleta ushahidi). Huwezi kuamka asubuhi na kutupa tuhuma za kijamii zisizo na thibitisho thabiti (substantive evidence), kisha ukadai mzigo wa kujisafisha uende kwa mtuhumiwa. Hiyo siyo sheria wala demokrasia, bali ni mob justice ya kisiasa inayolenga kufanya tabia ya kuua wahusika kisiasa (character assassination).
Kama kweli unataka kutumia kipimo hicho unachokipigania kama benchmark ya uwajibikaji, hebu tuiangalie serikali yako na mfumo wa chama tawala kupitia mifano halisi:
  1. Ufisadi wa Kimfumo (Systemic Graft): Tuhuma ngapi nzito za mikataba mibovu ya rasilimali, ubadhirifu wa fedha za umma, na ufisadi ulioripotiwa mara kwa mara na CAG zimeelekezwa kwa vigogo wa serikali na hakuna kiongozi hata mmoja wa CCM aliyetakiwa kukaa pembeni? Mbona huko hamuombi Burden of Proof ifanye kazi yake?
  2. Kuvunja Misingi ya Demokrasia: Baada ya mtikisiko mkubwa wa kisiasa na kisheria ulioambatana na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025—ikiwemo ripoti rasmi zilizobainisha mamia ya vifo vya raia na matumizi mabaya ya nguvu ya vyombo vya dola—ni kiongozi gani wa ngazi ya juu wa serikali au CCM aliyewajibika au kupisha uchunguzi wa kimataifa?
Mbona katika skandali hizi kubwa zenye athari za kitaifa mfumo mzima wa dola unajipanga kuwalinda watuhumiwa? Unaponyamazia makosa makubwa ya kiuongozi ndani ya serikali ya CCM lakini ukakimbilia kushupalia tuhuma nyepesi zisizo na mashiko upande wa pili, huu unakuwa ni undumilakuwili wa wazi (sheer double standards).
Rai yangu kwa Wana-JamiiForums:

Ni lazima tuchukue hatua za makusudi kuinusuru JamiiForums ili isirudi nyuma na kuwa jukwaa la upashkaji na majungu. Mtandao huu ulizaliwa kama Think Tank mbadala ya Great Thinkers nchini. Ni aibu kuu kuacha mijadala ya kitaaluma na kimkakati ishushwe hadhi na MACHAWA wa CCM ambao wanajaza kurasa za jukwaa hili kwa propaganda nyepesi na habari za kutungwa kwa lengo la kusafisha mabwana zenu. Turudishe jukwaa hili kwenye misingi yake ya uchambuzi wa kina na hoja zenye mashiko ya kisayansi na kiintelijensia!
Ahsante kwa kuandika. Ukweli dhamira yangu kuu hapa ilikuwa kuchora mstari ambao unatenganisha kati ya cdm na ccm katika weledi, haki na demokrasi. Nimegundua hata cdm wanaituhumu CCM muda wote bila kutoa ushahidi. Mfano, cdm wanasema hawa wanaomkosoa HEche wamelipwa na ccm kumchafua HECHE bila proof.

Nyani haoni kundule. Tuhuma sio kosa mpaka ithibitishwe, lakini kupitisha kiti ili usafishwe au uingizwe kwenye hatia ni takwa la kisheria. MIMI nikituhumiwa jambo nitataka jina langu lisafishwe ili kuthibitidha niko safi. nitathibitisha kuwa niko safi kwa kwenda mahakamani tu kuomba mtuhumu alete uthibitisho sio kwa kumtisha na kumfukuza chama.
 
Inaonekana waliokutuma hawajakusugua vizuri. Nenda kasuguliwe kisawa sawa, yawezekana akili yako itarudi mahala pake.
Kwa taarifa yako, Heche ni Dhahabu ya Watanzania.
Kaka tuhuma zinatoka ndani ya wanachadema. Heche anatakiwa kuwashitaki mahakamani wote anaodhani wanamchafua kwa kutumwa. Kama ni ushahidi utapelekwa mahakamani, na ili ushahidi upatikane mtuhumiwa lazima akae mbali na nyaraka za chama kwa muda ili zipitiwe na vyombo vya uchunguzi. Huwezi kusema walete uthibitisho huku wewe ukiwa bado unaatamia nyaraka za chama ofisini. Ushahidi unapelekwa mahakamani sio kwako.

Kwanini huendi mahakani kuwashitaki watu ambao una uthibitisho kuwa wametumwa na CCM wakuchafue? Unaogopa nini kwenda mahakamani ambaki haki zinapatikana?
 
Hao watu ni akina nani?

Wewe ni miongoni mwa hao watu?

Hao "watu" hawana majina?

Hao watu walimchangia kiasi gani?

Hao watu kwanini wasije wao kusema hizo pesa aliwaomba lini na kwa sababu zipi au wamekufa?

Hao watu kwanini walimtumia pesa kama mnavyodai ni za chama kwenye account yake na si account ya chama ? Je asiyejua hapo taratibu za kiofisi ni hao watu au ni Heche?
Kama Heche anaona wanaomtuhumu ni waongo mbona haendi mahakamani kuomba fidia ya kuchafuliwa? Mbona anakimbilia kuwafukuza badala ya kuwashitaki mahakamani?
 
Back
Top Bottom