Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Leo ndio umeona Mkuu unakuta font tu sio uniform, Tangazo zima ni bold. Personally naona Rais Hana muda wa kuwahakiki wasaidizi wake yeye anapokea tuMwandishi atakuwa Francophone. Wafaransa ndio wanatumia koma kwenye nukta. Yaani kwa Kifaransa bilioni 6,253 = bilioni 6.253. Lakini kusema ukweli Ikulu yetu ni jumba bovu. Nyaraka za Ikulu km vile press release za uteuzi zimejaa typos!!
Kichwa boksiHangaya anahujumiwa,ila yeye haelewi hilo.
Halafu inatosha kwa miezi saba...Nilidhani sijasikia vyema ikabidi nimfuate kule tube kusikiliza Tena nikajirithisha kuwa masikio yangu ni mazima!
Huenda ni kweli BoT wanazo hizo dollar bilioni elfu sita. Basi walipe deni lote la taifa ili nchi isidaiwe Tena. Au mnasemaje ndugu zangu?
Kama hicho kiwango alichotaja hakipo basi huu ni mkwaju au bakora nyingine Tena tumechapwa nayo wananchi!
Hivi inawezekana kufanya editing kwenye hotuba iliyokwisha ruka hewani?
Nimshauri bi mkubwa kuwa, kabla ya kuisogelea mimbari yoyote asome alichokabidhiwa kwanza ajiridhishe vinginevyo Kuna siku atawekewa barua ya posa ya bintiye naye atatusomea Kama hotuba! Bi mkubwa ajiri waandishi na wanahabari wazalendo na watiifu kwako achana na hao waandishi michongo unaoletewa watakuangushia gari bovu!
Hizo ni zaid ya dola trilioni sita, karibu sana na bajeti ya Marekani ambayo ni dola trilioni 6.82.Leo Rais Samia wakati akitoa hotuba ya kufunga mwaka 2021 ameitaja akiba ya fedha za kigeni dola za kimarekani bilioni 6,253. Nikajua labda lafudhi ya kizanzibari imenichanganya au kosa la usomaji...
wangekata deni la watu angalau lipungue tubaki na tri 3 zinatosha maana hadi aje amalize muhula tutakua tumekopa kufikia 85-90Hizo ni zaid ya dola trilioni sita, karibu sana na bajeti ya Marekani ambayo ni dola trilioni 6.82.
Hizo sio hela za umma tu ni pamoja na za sector bijafsi.
Stock ya dola ina maana wakichukua dola zote za serikali, na zile zinazomilikiwa na watu binafsi kwenye bank na bureau ndio unapata akiba ya fedha za kigeni. Kusema serikali ikazilipie deni sio sahihi maana sio hela zake
Hayo mambo ya kuongopa alikuwa nayo Jiwe. Huyu mama itakuwa kakosea kusoma tarakimu bila shaka
Na hii pia atakuwa kadanganywa na wasaidizi wake au uwezo wake mdogo.
hotuba ya lisu ilimtia wenge mama akawa anajiropokea tu.
Nadhani kwny B ilipaswa kusomeka M