Leo Rais Samia wakati akitoa hotuba ya kufunga mwaka 2021 ameitaja akiba ya fedha za kigeni dola za kimarekani bilioni 6,253. Nikajua labda lafudhi ya kizanzibari imenichanganya au kosa la usomaji.
Kumbe ndivyo alivyoandikiwa kwenye hotuba yake, najiuliza mchakato wote wa maandalizi ya hotuba na kwenye mikono iliyopita wameshindwa kung'amua tofauti kubwa hivi ya fedha.
Hizi hela ni zaidi ya trilioni 14,000 za kitanzania, yaani lile deni la trilioni 70 wanalogombania na Ndugai ingekuwa hela ya peremende na sio mboga.
View attachment 2064430