Hii akiba ya fedha za kigeni dola Bilioni 6,253 aliyosema Rais Samia kiboko, deni la Taifa lingekuwa hela ya peremende

Mwandishi atakuwa Francophone. Wafaransa ndio wanatumia koma kwenye nukta. Yaani kwa Kifaransa bilioni 6,253 = bilioni 6.253. Lakini kusema ukweli Ikulu yetu ni jumba bovu. Nyaraka za Ikulu km vile press release za uteuzi zimejaa typos!!
Leo ndio umeona Mkuu unakuta font tu sio uniform, Tangazo zima ni bold. Personally naona Rais Hana muda wa kuwahakiki wasaidizi wake yeye anapokea tu
 
Halafu inatosha kwa miezi saba...
 

Sasa mkuu, kama haiwezi kuzilipia deni inawezaje kuzifanyia matumizi ya kununulia chakula?
 
Mh Rais kwenye hotuba yake hapo jana kwa wananchi amesema kuwa nchi yetu hadi leo ina akiba ya pesa za kigeni zaidi ya dola billion elfu sita miambili hamsini na tatu (Dola billion 6253).

Ukiangalia hiki kiasi kwa kukifanyia mahesabu utagundua Tanzania ina ukwasi mkubwa sana na tena tunaweza kuihudumia hata Marekani kibajeti na kwa hakika tunapaswa kulipa madeni yote hapo kesho kama kweli hichi kiasi cha pesa kipo chote na kweli kama alivyosema Mh Rais!

Mh Rais hizo hela ulizotaja hata USA awezi kuwanazo kwa haraka!

Ni kweli Mh Rais tuna dola trillion 6+ kama akiba?

Hakika kama ni kweli basi Marekani +China +Japani tunawakaribisha waje kukopa kwetu!

Ni kweli tuna akiba ya dolla billion 6253?
 
Nadhani kwny B ilipaswa kusomeka M

Wewe pengine ndio unakosea maana Rais anasoma hotuba hatoi kichwani kabisa sasa watu hadi wanaandika ni wazi wanajua ukweli na Rais lazima alipitia hotuba kabla ya kusoma! Pengine hicho kiasi kipo kweli hivyo tulipe kabisa madeni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…