Katika kipande kifupi cha video hapa chini ni Rais Samia akihutubia jana kuelekea siku ya mwaka mpya.
Katika kipande hiki cha video Rais anadai kuwa nchi ina akiba za fedha za kigeni kiasi cha dola za kimarekani 6253 bilioni Kitu ambacho siyo sahihi wala siyo kweli kwa sababu haya ni matrilioni kwa fedha za Kitanzania.
Kinachotia kichefuchefu na kukasirisha ni kwamba alieandaa hotuba hii anapaswa kuihariri kisha kumpa Rais.Rais nae anapaswa kuihariri hotuba yake ndipo apande nayo hewani.
Assumption hapa ni kwamba kwa hotuba kubwa na muhimu kama hiyo kutoka kwa Rais wa nchi hayo yote yalifanyika.Lakini cha kushangaza hotuba hiyo imesomwa na Rais ikiwa na makosa kama hayo.
Makosa haya yanaweza kuwa na maana moja kati ya maana hizi mbili.Kwanza inawezekana hotuba hii alieiandika hakuihariri kabisa na pia alipopewa Rais nae hakuihariri kabisa hadi anapanda hewani,kitu ambacho ni ngumu kuamini.
Lakini maana ya pili inawezekana kuwa wote wawili, yaani Rais pamoja na alieandika hotuba hii kusoma namba iliwapiga chenga.Yaani alieandika hotuba namba zilimchanganya akasema iende hivyo hivyo tuuu na Rais nae namba zikamchanganya akasema iende hivyo hivyo tuu.Hii inaleta maana zaidi kwa sababu kwa point ya kwanza ni ngumu Rais kusoma hotuba ambayo yeye mwenyewe hajaipitia.
Hotuba kama hii ambayo mamilioni ya watanzania walikuwa wanaenda kuisikiliza ilipaswa iandikwe kwa makini ikiwa ni pamoja na kuhaririwa na mtu zaidi ya mmoja ikiwa ni pamoja na Rais mwenyewe.
Kitendo cha hotuba hii kwenda hewani ikiwa na makosa ya kizembe namna hii inaonyesha wazi kwamba system nzima ya uongozi katika nchi hii kuanzia Rais hadi wasaidizi wake imeoza.
Makosa ya kijinga kabisa katika hotuba hii yanaibua maswali yafuatayo ambayo yanatia mashaka:
1.Wasaidizi wa Rais wanajua kusoma na kuandika?
2.Wasaidizi wa Rais wapo serious na kazi yao?
3.Rais anajua kusoma na kuandika?
4.Rais yupo serious na kazi yake?
5.Hotuba hii imeibua aina ya Rais tulienae pamoja na wasaidizi wake?
6.Wananchi waliosikiliza hotuba hii wanamchukuliaje Rais wao?
7.Rais ana uwezo wa kuongoza?
8.Je,Tanzania ina kiongozi kipofu ambae anaongoza vipofu wenzake?
9.Nani anastahili lawama kubwa katika hotuba hii zaidi ya Rais mwenye hotuba yake?
10.Kama nchi tuna mfumo mzuri wa kupata viongozi sahihi?
Kwa makosa haya Rais hawezi kukwepa lawama zote hata kidogo kwa sababu yeye ndiye alikuwa mtoa hotuba na alipaswa kuhakikisha kuwa hotuba yake ipo safi kabla hajaenda hewani.Makosa ya kijinga kabisa katika hotuba hii imewanyima wananchi kupata habari muhimu kabisa juu ya akiba yetu ya fedha za kigeni.
View attachment 2065193