Hii akiba ya fedha za kigeni dola Bilioni 6,253 aliyosema Rais Samia kiboko, deni la Taifa lingekuwa hela ya peremende

Hii akiba ya fedha za kigeni dola Bilioni 6,253 aliyosema Rais Samia kiboko, deni la Taifa lingekuwa hela ya peremende

Kumbuka Rais anapelekewa hotuba sio lazima aanze kuipitia,wasaidizi wanaweza kufanya makosa
Kuna kitu kinaitwa common sense. Uketewa taarifa unapaswa na wewe ushirikishe ubongo.
Kwa hiyo siku akiandikiwa kuwa shinyanga kuna bahari ma yeye atasoma Kama ilivyo?
 
Katika kipande kifupi cha video hapa chini ni Rais Samia akihutubia jana kuelekea siku ya mwaka mpya.

Katika kipande hiki cha video Rais anadai kuwa nchi ina akiba za fedha za kigeni kiasi cha dola za kimarekani 6253 bilioni Kitu ambacho siyo sahihi wala siyo kweli kwa sababu hii ni zaidi ya trilioni 14,000 kwa fedha za Kitanzania.

Kinachotia kichefuchefu na kukasirisha ni kwamba alieandaa hotuba hii anapaswa kuihariri kisha kumpa Rais.Rais nae anapaswa kuihariri hotuba yake ndipo apande nayo hewani.
Sasa Chifu mbona hata wewe mwenyewe unajichanganya?

Dola Billion 6000 ni = $6000x1000,0000,000 = $ 6 Trillion ambayo ni karibu na 14 QUADRILLION na sio 14 TRILLION uliyoisema wewe! Unaona sasa mambo ya namba yalivyo magumu? Mkosoaji nae anakosea!!! Tuache namba ziitwe namba!!!

Tukirudi kwenye hoja, bila shaka alitaka kumaanisha Dola Milion 6000 ambayo ni 6000x1000,000 = $6 Billion, ambayo ndiyo italeta hiyo 14 Trillion unayoisema! Hiyo figure inaweza kuwa sahihi! Kwa kawaida, Foreign Reserves yetu inakuwa in terms of Billion USD, na uchumi unataka uwe na akiba ya Foreign reserve inayoweza kutosheleza at least 6 months. Fuatilia hata wakati wa JPM na JK, ilikuwa haijawahi kupungua USD 4 Billion.
 
unaweza sema kwa jiwe tulipatikana alafu kwa maza tumekosekana, tofauti yao ni jinsia tu.
 
Kwa dhahabu iliyokuwwpo chini ya ardhi mambo hayo ya hifadhi za pesa za kigeni ilitakiwa iwe juu zaidi
 
Ni milioni 1.
1,000 zikifika 1,000 Ina badilika inakuwa milioni 1.
Ndo maana Mimi naona muandishi wa ile hotuba alikosea..
Kama alitaka kumaanisha Wana dola bilioni 6,000
Sahihi alitakiwa aandike Wana dola trilioni 6.
Nadhani Mimi ninavyoona walitaka kuandika dola milioni 6,00 hapo kidogo hesabu inakuwa sawa
Zitakuwa elfu elfu moja!Wigwa?
 
Katika ile hesabu ya Jana Kuna typing error.
sidhani Kama alikuwa anataka kusema dola bilioni 6,000+
Badala yake wangesema Wana dola trilioni 6.
Okay.Hoja ni kwamba,kweli kuna akiba ifikiayo kiasi hicho?Kweli?Kuna haja gani tukope.Hoja ndiyo hiyo.Waandaaji na msomaji wa "risala" hawako makini.
 
Katika kipande kifupi cha video hapa chini ni Rais Samia akihutubia jana kuelekea siku ya mwaka mpya.

Katika kipande hiki cha video Rais anadai kuwa nchi ina akiba za fedha za kigeni kiasi cha dola za kimarekani 6253 bilioni Kitu ambacho siyo sahihi wala siyo kweli kwa sababu hii ni zaidi ya trilioni 14,000 kwa fedha za Kitanzania.

Kinachotia kichefuchefu na kukasirisha ni kwamba alieandaa hotuba hii alipaswa kuihariri kisha kumpa Rais.Rais nae alipaswa kuihariri hotuba yake ndipo apande nayo hewani.

Assumption hapa ni kwamba kwa hotuba kubwa na muhimu kama hiyo kutoka kwa Rais wa nchi hayo yote yalifanyika.Lakini cha kushangaza hotuba hiyo imesomwa na Rais ikiwa na makosa kama hayo.

Makosa haya yanaweza kuwa na maana moja kati ya maana hizi mbili.Kwanza inawezekana hotuba hii alieiandika hakuihariri kabisa na pia alipopewa Rais nae hakuihariri kabisa hadi anapanda hewani,kitu ambacho ni ngumu kuamini.

Lakini maana ya pili inawezekana kuwa wote wawili, yaani Rais pamoja na alieandika hotuba hii kusoma namba iliwapiga chenga.Yaani alieandika hotuba namba zilimchanganya akasema iende hivyo hivyo tuuu na Rais nae namba zikamchanganya akasema iende hivyo hivyo tuu.Hii inaleta maana zaidi kwa sababu kwa point ya kwanza ni ngumu Rais kusoma hotuba ambayo yeye mwenyewe hajaipitia.

Hotuba kama hii ambayo mamilioni ya watanzania walikuwa wanaenda kuisikiliza ilipaswa iandikwe kwa makini ikiwa ni pamoja na kuhaririwa na mtu zaidi ya mmoja ikiwa ni pamoja na Rais mwenyewe.

Kitendo cha hotuba hii kwenda hewani ikiwa na makosa ya kizembe namna hii inaonyesha wazi kwamba system nzima ya uongozi katika nchi hii kuanzia Rais hadi wasaidizi wake imeoza.

Makosa ya kijinga kabisa katika hotuba hii yanaibua maswali yafuatayo ambayo yanatia mashaka:

1.Wasaidizi wa Rais wanajua kusoma na kuandika?

2.Wasaidizi wa Rais wapo serious na kazi yao?

3.Rais anajua kusoma na kuandika?

4.Rais yupo serious na kazi yake?

5.Hotuba hii imeibua aina ya Rais tulienae pamoja na wasaidizi wake?

6.Wananchi waliosikiliza hotuba hii wanamchukuliaje Rais wao?

7.Rais ana uwezo wa kuongoza?

8.Je,Tanzania ina kiongozi kipofu ambae anaongoza vipofu wenzake?

9.Nani anastahili lawama kubwa katika hotuba hii zaidi ya Rais mwenye hotuba yake?

10.Kama nchi tuna mfumo mzuri wa kupata viongozi sahihi?

Kwa makosa haya Rais hawezi kukwepa lawama zote hata kidogo kwa sababu yeye ndiye alikuwa mtoa hotuba na alipaswa kuhakikisha kuwa hotuba yake ipo safi kabla hajaenda hewani.Makosa ya kijinga kabisa katika hotuba hii yamewanyima wananchi kupata habari muhimu kabisa juu ya akiba yetu ya fedha za kigeni.
View attachment 2065193
View attachment 2065245
Hongera kwa maswali muhimu.
Kitu cha kujiuliza pia ni wahusika kushindwa kuishtukia namba hata kama kulikuwa na makosa.
Kuna ile ukifanya hesabu zako, unaona kabisa hii namba ninayoipata sio yenyewe.
Yaani impossible number, wao wakachukulia ip.
 
Hakuna mfumo mzuri. Urais ni kama sandakalawe atakaebahatika ndio huyo huyo.
Kazi inaendelea
 
Katika ile hesabu ya Jana Kuna typing error.
sidhani Kama alikuwa anataka kusema dola bilioni 6,000+
Badala yake wangesema Wana dola trilioni 6.
Hakika namba ngumu!
1. SSH kakosea!
2. Mleta mada kako
3. Nawe pamoja na kujitahidi kuelimisha lakini pia umekosea kwa sababu umeongea kile kile alichoongea mleta mada ambae nae amekosea!

Dola Trillion 6 Tanzania tuitolee wapi? SSH alimaanisha $ milion elfu 6; yaani $ 6000x 10000000 = $6 Billion
 
Sasa Chifu mbona hata wewe mwenyewe unajichanganya?

Dola Billion 6000 ni = $6000x1000,0000,000 = $ 6 Trillion ambayo ni karibu na 14 QUADRILLION na sio 14 TRILLION uliyoisema wewe! Unaona sasa mambo ya namba yalivyo magumu? Mkosoaji nae anakosea!!! Tuache namba ziitwe namba!!!

Tukirudi kwenye hoja, bila shaka alitaka kumaanisha Dola Milion 6000 ambayo ni 6000x1000,000 = $6 Billion, ambayo ndiyo italeta hiyo 14 Trillion unayoisema! Hiyo figure inaweza kuwa sahihi! Kwa kawaida, Foreign Reserves yetu inakuwa in terms of Billion USD, na uchumi unataka uwe na akiba ya Foreign reserve inayoweza kutosheleza at least 6 months. Fuatilia hata wakati wa JPM na JK, ilikuwa haijawahi kupungua USD 4 Billion.
Hakuna popote niliposema trilioni 14.
 
Hakika namba ngumu!
1. SSH kakosea!
2. Mleta mada kako
3. Nawe pamoja na kujitahidi kuelimisha lakini pia umekosea kwa sababu umeongea kile kile alichoongea mleta mada ambae nae amekosea!

Dola Trillion 6 Tanzania tuitolee wapi? SSH alimaanisha $ milion elfu 6; yaani $ 6000x 10000000 = $6 Billion
Nimekosea kitu gani?
 
Back
Top Bottom