Hii akiba ya fedha za kigeni dola Bilioni 6,253 aliyosema Rais Samia kiboko, deni la Taifa lingekuwa hela ya peremende

Hii akiba ya fedha za kigeni dola Bilioni 6,253 aliyosema Rais Samia kiboko, deni la Taifa lingekuwa hela ya peremende

Ili bilioni ibadilike iwe trilioni inatakiwa ziwe bilioni ngapi?
Hakika namba ngumu!
1. SSH kakosea!
2. Mleta mada kako
3. Nawe pamoja na kujitahidi kuelimisha lakini pia umekosea kwa sababu umeongea kile kile alichoongea mleta mada ambae nae amekosea!

Dola Trillion 6 Tanzania tuitolee wapi? SSH alimaanisha $ milion elfu 6; yaani $ 6000x 10000000 = $6 Billion
 
Rais ajifunze upya hisabati na asahihishe makosa hadharani. Huo ni uungwana. Kutojua au kukosea jambo ni ubinadamu, tatizo ni pale tunapoacha kujifunza na kujisahihisha
 
Ebu Soma maelezo yako hayo.
Kama hamna trilioni 14.
Ndo maana nikasema mbona hyo hesabu siielewii
Hakuna popote niliposema trilioni 14.
Screenshot_20220101-183754.jpg
 
Katika kipande kifupi cha video hapa chini ni Rais Samia akihutubia jana kuelekea siku ya mwaka mpya.

Katika kipande hiki cha video Rais anadai kuwa nchi ina akiba za fedha za kigeni kiasi cha dola za kimarekani 6253 bilioni Kitu ambacho siyo sahihi wala siyo kweli kwa sababu hii ni zaidi ya trilioni 14,000 kwa fedha za Kitanzania.

Kinachotia kichefuchefu na kukasirisha ni kwamba alieandaa hotuba hii alipaswa kuihariri kisha kumpa Rais.Rais nae alipaswa kuihariri hotuba yake ndipo apande nayo hewani.

Assumption hapa ni kwamba kwa hotuba kubwa na muhimu kama hiyo kutoka kwa Rais wa nchi hayo yote yalifanyika.Lakini cha kushangaza hotuba hiyo imesomwa na Rais ikiwa na makosa kama hayo.

Makosa haya yanaweza kuwa na maana moja kati ya maana hizi mbili.Kwanza inawezekana hotuba hii alieiandika hakuihariri kabisa na pia alipopewa Rais nae hakuihariri kabisa hadi anapanda hewani,kitu ambacho ni ngumu kuamini.

Lakini maana ya pili inawezekana kuwa wote wawili, yaani Rais pamoja na alieandika hotuba hii kusoma namba iliwapiga chenga.Yaani alieandika hotuba namba zilimchanganya akasema iende hivyo hivyo tuuu na Rais nae namba zikamchanganya akasema iende hivyo hivyo tuu.Hii inaleta maana zaidi kwa sababu kwa point ya kwanza ni ngumu Rais kusoma hotuba ambayo yeye mwenyewe hajaipitia.

Hotuba kama hii ambayo mamilioni ya watanzania walikuwa wanaenda kuisikiliza ilipaswa iandikwe kwa makini ikiwa ni pamoja na kuhaririwa na mtu zaidi ya mmoja ikiwa ni pamoja na Rais mwenyewe.

Kitendo cha hotuba hii kwenda hewani ikiwa na makosa ya kizembe namna hii inaonyesha wazi kwamba system nzima ya uongozi katika nchi hii kuanzia Rais hadi wasaidizi wake imeoza.

Makosa ya kijinga kabisa katika hotuba hii yanaibua maswali yafuatayo ambayo yanatia mashaka:

1.Wasaidizi wa Rais wanajua kusoma na kuandika?

2.Wasaidizi wa Rais wapo serious na kazi yao?

3.Rais anajua kusoma na kuandika?

4.Rais yupo serious na kazi yake?

5.Hotuba hii imeibua aina ya Rais tulienae pamoja na wasaidizi wake?

6.Wananchi waliosikiliza hotuba hii wanamchukuliaje Rais wao?

7.Rais ana uwezo wa kuongoza?

8.Je,Tanzania ina kiongozi kipofu ambae anaongoza vipofu wenzake?

9.Nani anastahili lawama kubwa katika hotuba hii zaidi ya Rais mwenye hotuba yake?

10.Kama nchi tuna mfumo mzuri wa kupata viongozi sahihi?

Kwa makosa haya Rais hawezi kukwepa lawama zote hata kidogo kwa sababu yeye ndiye alikuwa mtoa hotuba na alipaswa kuhakikisha kuwa hotuba yake ipo safi kabla hajaenda hewani.Makosa ya kijinga kabisa katika hotuba hii yamewanyima wananchi kupata habari muhimu kabisa juu ya akiba yetu ya fedha za kigeni.
View attachment 2065193
View attachment 2065245

Watanzania wengi nimegundua wana matatizo kwenye hili hata magazeti yanakosea sana. Inabidi mwandishi apewe ovyo. Lakini hata wakati wa Magufuli walikuwa wanakosea hivyo tusilaumu kama vile imeanza leo
 
Mwandishi atakuwa Francophone. Wafaransa ndio wanatumia koma kwenye nukta. Yaani kwa Kifaransa bilioni 6,253 = bilioni 6.253. Lakini kusema ukweli Ikulu yetu ni jumba bovu. Nyaraka za Ikulu km vile press release za uteuzi zimejaa typos!!
Nakubaliana na wewe. Niliandikiwa bill na Indian asee nilitaka changanyikiwa, kumbe wao wanatumia koma Instead of nukta.

Pia TZ haiwezi kuwa na reserve nyingi kiasi hicho. Wakati corona Inaanza China Ilikuwa na reserve ya $3,000 B ( USD Elfu tatu Bilioni) Kwa hali hii means TZ Ina mara mbili ya reserve compared to China??? Jibu ni haiwezekani hata miaka elfu 10 Ijayo.

Hiyo ni aina ya uandishi. Simply mama amekosea tu kusoma lakini uandishi upo sahihi. Ila angetakiwa apewe taarifa mapema maana aina hiyo ya uandishi hautumiki hapa TZ. Kosa linaenda kwa aliyeandika hiyo hotuba.

Happy New Year to you all.
 
Nimeandika TZS 14,000 trilioni.
Kukosoa , kuonesha makosa katika kazi iliyofanywa na mtu mwingine, ni miongoni mwa kazi rahisi duniani .
Taz.

"Katika kipande hiki cha video Rais anadai kuwa nchi ina akiba za fedha za kigeni kiasi cha dola za kimarekani 6253 bilioni Kitu ambacho siyo sahihi wala siyo kweli kwa sababu hii ni zaidi ya trilioni 14,000 kwa fedha za Kitanzania."
 
KOSA. hamna hela hyo
Ni sawa na Samia aliyesema Wana dola bilioni 6,000+.
Samia sahihi alitakiwa asema Wana akiba ya dola trilioni 6.
Hapo namaanisha Kama kweli walikusudia kusema Wana hyo akiba ya dola bilioni 6,000.
Ndo maana ninasema typing error kwenye uandishi mpaka kwenye matamshi wamekosea
Ameandika trilioni elfu kumi na nne(14,000).
 
Pamoja Na facts zote hizo bado unauliza? Kweli Tanzania kuna vilaza
Haupo makini tatizo, baada ya mimi kuuliza
Ndo wadau wamejaribu kufafanua hizo figure.
Sasa wewe ndo kilaza kumbe.
 
Kwanza Rais anafahamu kiasi cha akiba ya fedha zilizopo hata bila kuandikiwa, hivyo alipaswa kustuka hata kabla ya kutamka. Kwa kututamkia matango pori hakika tumepigwa!
Anafahamu yeye ndio anatunza pesa au anauliza waliopewa dhamana?
 
UMEMSOMA VIZURI? HIZO NAMBA UMEZIONA? Ameandika trilioni 14,000 na wala siyo trilioni 14. Trilioni 14,000 = trilioni 14,000,000,000,000,000.
Umemnukuu sawa aliposema "billion elfu 6000" lakini Billion Elfu 6 ni pesa mingi mno, na sio Trillion 14 ulizosema wewe! 14 Trillion kuna zero 12, wakati Dola Bilion Elfu kutakuwa na zero 15 ambayo itakuwa almost 14 QUADRILLION na sio TRILLION
^kwa sababu hii ni zaidi ya trilioni 14,000 kwa fedha za Kitanzania.^
 
Back
Top Bottom