Hii akiba ya fedha za kigeni dola Bilioni 6,253 aliyosema Rais Samia kiboko, deni la Taifa lingekuwa hela ya peremende

Hii akiba ya fedha za kigeni dola Bilioni 6,253 aliyosema Rais Samia kiboko, deni la Taifa lingekuwa hela ya peremende

Na wewe una sadiki Kuna dola
Milioni 6,000?
ni sahihi kusema dola milioni 6,000?
Kwa kuangalia takwimu za miaka 10 iliyopita, nasadiki!! Chifu, sio ajabu kuwa na Shilingi Trillion 14 kama akiba ya fedha za kigeni
 
Ni dola milioni 6,000
Au dola trilioni 6?
Kwa kuangalia takwimu za miaka 10 iliyopita, nasadiki!! Chifu, sio ajabu kuwa na Shilingi Trillion 14 kama akiba ya fedha za kigeni
 
SIJAKOSEA CHIFU! Post yangu ya mwanzo ni hii hapa chini

Unaona hapo nimeandika 14 QUADRILLION! Sasa kama ningeandika 14,000 QUADRILLION, hiyo ingekuwa ni 14 Sextrillion na sio 14 Quadrillion! Ndo maana nimesema, usipoangalia, nawe utajikuta unaanza kuandika makorogesheni1
Niliposema ^rejea posti ya mwanzo,^ sikuwa na maana ya posti yako, bali bandiko la mleta-mada. Endelea kukosea tu, mwishoni utakosekana.
 
Sasa hakuna trilioni 14,000.
Unakuwa hauna tofauti na Samia aliyesema Ana
Dola bilioni 6,000+.
Sijui unanielewa tunapopishana?
Wewe ndiye ambae hujanielewa!Nilichomaanisha kwenye uzi wangu ni kwamba dola za kimarekani alizotaja Rais ukizibadili kuwa fedha za Kitanzania ni sawa na trilioni 14,000.Nimeyasema haya kuonyesha jinsi Rais alivyokosea.
 
Sasa hakuna trilioni 14,000.
Unakuwa hauna tofauti na Samia aliyesema Ana
Dola bilioni 6,000+.
Sijui unanielewa tunapopishana?
Aiseee! Hii mada inanikumbusha zile calculations za jamaa kilomita alizokimbia kutoka Kigoma hadi Dar kuja kushuhudia mechi ya Watani wa Jadi. Tanzania tuna safari ndefu sana. Nachelea, japo kinyonge sana, kusema, kwa mtaji huu, kuibiwa ni haki yetu ya kuzaliwa.
 
Quadrillion 14
Sio trilioni 14,000.
Sawa yote kwa yote Samia na wasaidizi wake wamekosea
Wewe ndiye ambae hujanielewa!Nilichomaanisha kwenye uzi wangu ni kwamba dola za kimarekani alizotaja Rais ukizibadili kuwa fedha za Kitanzania ni sawa na trilioni 14,000.Nimeyasema haya kuonyesha jinsi Rais alivyokosea.
 
Niliposema ^rejea posti ya mwanzo,^ sikuwa na maana ya posti yako, bali bandiko la mleta-mada. Endelea kukosea tu, mwishoni utakosekana.
Sasa wewe ndo unakuza mambo kwa sababu hapo juu nilishakiri kwamba nilikosea kumkosoa Behavorist lakini sikukosea figures zagu! Na pia nikasema wazi kwamba SSH amekosea ama yeye mwenyewe au waandishi! Nikaendeleakusema, kwa vyovyote itakuwa Dola Million Elfu 6 ambayo ni kiwango cha kawaida, na ndicho kiwango nilichokuambia kwamba kinaweza kuwa sahihi!!
 
Umemnukuu sawa aliposema "billion elfu 6000" lakini Billion Elfu 6 ni pesa mingi mno, na sio Trillion 14 ulizosema wewe! 14 Trillion kuna zero 12, wakati Dola Bilion Elfu kutakuwa na zero 15 ambayo itakuwa almost 14 QUADRILLION na sio TRILLION
Hakuna popote nilipoandika trilioni 14.Unaweza kunionyesha ni wapi nimeandika trilioni 14?
 
Haya mambo yanachosha sasa. Kila saa lawama ileile tu. Kama Samia sio Rais mzuri wa kumlaumu ni Mwendazake.... Yeye ndie alimchagua awe makamu wake mara zote mbili.

So far sijaona tatizo lolote la mama zaidi ya malumbano ya vikundi vinavyokinzana... wachumia tumbo kazi kwelikweli
Mwendazake alisha semaga Hussein mwinyi ndiye alikuwa chaguo huyu Mama ali sukumiziwa tu
 
Huenda mkuu upo sahihi.Huenda sisi tunaosema kuwa amekosea tukawa wajinga!
Hapana mzee, naamini tatizo la waandishi! Nakumbuka siku moja kule twitter kulitokea tatizo kama hili! Baada ya watu kukosoa, ile taarifa wakierekebisha lakini wakaendelea kuikosea! Tusisahau education backgrounds za hawa waandishi wa hotuba!! Majority kama sio wote ni watu wa HGL/HKL/HGK ambao wao na namba ni vitu viwili tofauti
 
Sasa wewe ndo unakuza mambo kwa sababu hapo juu nilishakiri kwamba nilikosea kumkosoa Behavorist lakini sikukosea figures zagu! Na pia nikasema wazi kwamba SSH amekosea ama yeye mwenyewe au waandishi! Nikaendeleakusema, kwa vyovyote itakuwa Dola Million Elfu 6 ambayo ni kiwango cha kawaida, na ndicho kiwango nilichokuambia kwamba kinaweza kuwa sahihi!!
Na mimi nilipokukosoa, ilikuwa kwa mantiki ileile kwamba hukuwa na sababu ya kumkosoa mleta-mada kwa vile yuko sahihi ^car-bee-sir!^ Umeelewa sasa makosa yako? Niliposema una-spin, ni kama sasa unapotambua umekosea, then unakimbilia kusema nakuza mambo. FYI: Sina magnifier yoyote hapa ya kukuzia mambo. Naomba uthibitisho, tafadhali.
 
Mwendazake alisha semaga Hussein mwinyi ndiye alikuwa chaguo huyu Mama ali sukumiziwa tu
Nani alikuwa na jeuri ya kumpangia mwendazake. Nitajie mmoja nani ntakuonesha nguzo ya umeme inayozaa papai

Na unaweza kuniambia ni lini na wapi mwendazake aliyasema hayo?
 
Watanzania wengi nimegundua wana matatizo kwenye hili hata magazeti yanakosea sana. Inabidi mwandishi apewe ovyo. Lakini hata wakati wa Magufuli walikuwa wanakosea hivyo tusilaumu kama vile imeanza leo

Kwamagu nadhani labda walikosea kitu kingine, sio hesabu Magu kwenye hesabu alikuwa vizuri.
 
Hapana mzee, naamini tatizo la waandishi! Nakumbuka siku moja kule twitter kulitokea tatizo kama hili! Baada ya watu kukosoa, ile taarifa wakierekebisha lakini wakaendelea kuikosea! Tusisahau education backgrounds za hawa waandishi wa hotuba!! Majority kama sio wote ni watu wa HGL/HKL/HGK ambao wao na namba ni vitu viwili tofauti
Aisee!
 
Haiwezi kuwa Dola Billion 6,000 wala Dola Trillion 6! Jibu ni NDIYO, ama alikosea yeye, au ni kama alivyosema Mleta Mada inawezekana waliomwandikia walikosea! Hiyo itakuwa Dola Milion Elfu 6, yaani Dola 6000 Million, sawa na Dola 6 Billion! Dola Trillion 6 ni MINGI MNO SANA, na hatuna hiyo pesa! Lakini Dola Million 6000, ni pesa ya kawaida!
... atoke mwenye hotuba yake arekebishe badala ya wapambe kumsemea. Rais wa nchi hakosei alitutaarifu mwenyewe!
 
Katika kipande kifupi cha video hapa chini ni Rais Samia akihutubia jana kuelekea siku ya mwaka mpya.

Katika kipande hiki cha video Rais anadai kuwa nchi ina akiba za fedha za kigeni kiasi cha dola za kimarekani 6253 bilioni Kitu ambacho siyo sahihi wala siyo kweli kwa sababu hii ni zaidi ya trilioni 14,000 kwa fedha za Kitanzania.

Kinachotia kichefuchefu na kukasirisha ni kwamba alieandaa hotuba hii alipaswa kuihariri kisha kumpa Rais.Rais nae alipaswa kuihariri hotuba yake ndipo apande nayo hewani.

Assumption hapa ni kwamba kwa hotuba kubwa na muhimu kama hiyo kutoka kwa Rais wa nchi hayo yote yalifanyika.Lakini cha kushangaza hotuba hiyo imesomwa na Rais ikiwa na makosa kama hayo.

Makosa haya yanaweza kuwa na maana moja kati ya maana hizi mbili.Kwanza inawezekana hotuba hii alieiandika hakuihariri kabisa na pia alipopewa Rais nae hakuihariri kabisa hadi anapanda hewani,kitu ambacho ni ngumu kuamini.

Lakini maana ya pili inawezekana kuwa wote wawili, yaani Rais pamoja na alieandika hotuba hii kusoma namba iliwapiga chenga.Yaani alieandika hotuba namba zilimchanganya akasema iende hivyo hivyo tuuu na Rais nae namba zikamchanganya akasema iende hivyo hivyo tuu.Hii inaleta maana zaidi kwa sababu kwa point ya kwanza ni ngumu Rais kusoma hotuba ambayo yeye mwenyewe hajaipitia.

Hotuba kama hii ambayo mamilioni ya watanzania walikuwa wanaenda kuisikiliza ilipaswa iandikwe kwa makini ikiwa ni pamoja na kuhaririwa na mtu zaidi ya mmoja ikiwa ni pamoja na Rais mwenyewe.

Kitendo cha hotuba hii kwenda hewani ikiwa na makosa ya kizembe namna hii inaonyesha wazi kwamba system nzima ya uongozi katika nchi hii kuanzia Rais hadi wasaidizi wake imeoza.

Makosa ya kijinga kabisa katika hotuba hii yanaibua maswali yafuatayo ambayo yanatia mashaka:

1.Wasaidizi wa Rais wanajua kusoma na kuandika?

2.Wasaidizi wa Rais wapo serious na kazi yao?

3.Rais anajua kusoma na kuandika?

4.Rais yupo serious na kazi yake?

5.Hotuba hii imeibua aina ya Rais tulienae pamoja na wasaidizi wake?

6.Wananchi waliosikiliza hotuba hii wanamchukuliaje Rais wao?

7.Rais ana uwezo wa kuongoza?

8.Je,Tanzania ina kiongozi kipofu ambae anaongoza vipofu wenzake?

9.Nani anastahili lawama kubwa katika hotuba hii zaidi ya Rais mwenye hotuba yake?

10.Kama nchi tuna mfumo mzuri wa kupata viongozi sahihi?

Kwa makosa haya Rais hawezi kukwepa lawama zote hata kidogo kwa sababu yeye ndiye alikuwa mtoa hotuba na alipaswa kuhakikisha kuwa hotuba yake ipo safi kabla hajaenda hewani.Makosa ya kijinga kabisa katika hotuba hii yamewanyima wananchi kupata habari muhimu kabisa juu ya akiba yetu ya fedha za kigeni.

Imagine hawa ndiyo viongozi wanaosimamia miradi mikubwa ya mabilioni ya fedha za walala hoi kama vile SGR na Stigler gorge.Tutawaamini vipi hawa?!
View attachment 2065193
View attachment 2065245
Mwamba Kachiri on this one.
20211231_170349.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom