Hii akiba ya fedha za kigeni dola Bilioni 6,253 aliyosema Rais Samia kiboko, deni la Taifa lingekuwa hela ya peremende

Hii akiba ya fedha za kigeni dola Bilioni 6,253 aliyosema Rais Samia kiboko, deni la Taifa lingekuwa hela ya peremende

Awamu ya Pili ya uongozi wake angeweza na alikuwa na nafasi ya kufanya hivyo. Kwanini hakufanya?

Unajua Kikwete aliwahi kufanya hivyo? Unajua Dr. Shein alikuwa makamu wake wa awamu ya kwanza, awamu ya Pili akamteua Dr Bilal na Dr. Shein akaenda kuwa Rais wa Zanzibar??

Unajua?
Bilal “alipewa” uVP kama means ya kutuliza hali ya hewa Zenji maana kwenye kura zao kule alimtimulia vumbi kali sana Dr. Shein

BTW, mgombea wa urais wa CCM kimsingi huwa hana say 100% kwenye kuchagua running mate. Ile Central Commitee ndiyo inacontrol haya mambo
 
Ukibadili USD 6253 billion kuwa Tanzania shillings unapata zaidi ya TZS trillion 14,000

Inamake sense kuwa Tanzania ina fedha za kigeni trillion 14,000 za kitanzania?
View attachment 2065238
Mkuu haishangazi mbona, Magufuli aliwahi kutudanganya siku ina masaa 48, kwa siku mtu analazimika kuvaa barakoa 12😀

Maccm maongo maongo tu
 
Huo ni uchaguzi wa kwanza. Vipi awamu ya pili ambapo yeye ndo alishakuwa jiwe na hakukuwa na wa kumpangia. Kwanini hakumpiga chini mama akatupa makamu mzuri?

Pili hujasema hayo maneno aliyasema lini na wapi?
Halimpiga chini kwa kuto mshirikisha alijua kichwan hana kitu, we huji ulizi kwanin kauli zake zina onyesha tuna Raisi mwenye uwezo mdogo Sana wa kutumia akili yake na Mambo mengi ya nchi haya jui kuna kauli aliitoa kwamba miezi mitatu ya uraisi wake alikuwa ana jifunza jinsi ya wizara zinavyo endeshwa chakushangaza alikuwa waziri kwenye serikali ya hawamu ya 4 na makamu wa raisi awamu ya tano bado haikutosha kujua nchi inaogozwaje? maana yeye hakutolewa majalalan kama kabudi
 
Awamu ya Pili ya uongozi wake angeweza na alikuwa na nafasi ya kufanya hivyo. Kwanini hakufanya?

Unajua Kikwete aliwahi kufanya hivyo? Unajua Dr. Shein alikuwa makamu wake wa awamu ya kwanza, awamu ya Pili akamteua Dr Bilal na Dr. Shein akaenda kuwa Rais wa Zanzibar??

Unajua?
Mwendazake angeweza kumtoa je ange mpa ubalozi je ingekuwa sahii kumpeleka mwanamke akawe raisi Zanzibar ? Na wazanzibar wasinge kubali mwamke awe kiongoz wao mkuuu ata siku moja
 
Ni sahihi kwani dola bil 6250 unajua ni shilingi ngapi? Si ni til.14 na huo ndio ukweli
Boss, naomba kufahamishwa hapa, bilioni 6,250 pekee, kihesabu ni sahihi kuiita Trilioni 6.25?

6.25(t) × 2300 = 14,375(t) ni sawa?

Hivyo ni sawa na kusema tuna trilioni 14, 375. Kihesabu, hii tayari ni quadrillion 14.375

Hapo niko sawa? Dola bilioni 6,250.
 
Boss, naomba kufahamishwa hapa, bilioni 6,250 pekee, kihesabu ni sahihi kuiita Trilioni 6.25?

6.25(t) × 2300 = 14,375(t) ni sawa?

Hivyo ni sawa na kusema tuna trilioni 14, 375. Kihesabu, hii tayari ni quadrillion 14.375

Hapo niko sawa? Dola bilioni 6,250.
Dola mil.6250 ndio sahihi
 
Hapana, nimeshangaa kuandika namba kwa ufasaha kwamba yahitaji Hadi usome hesabu kwA kiwango cha shahada hahahahahahaha

Nafikiri kuna tatizo mahari, hata kama umesoma HKL, KLF, HKG hujui hesabu za kawaida Basi kuna tatizo
Chifu, asikuambie mtu! Hapa sio just numbers bali namba zikishafika kwenye mabilioni ni full mgogoro 😂!! Lakini nakubaliana na wewe kiasi kwamba it's not all about HKL Stuff ingawaje hawa nadhani inaweza kuwa zaidi, na siwezi kuwalaumu! Nasema nakubaliana na wewe kwa sababu manamba kama haya haya, kule Twitter yalizua mgogoro hadi Msigwa akawa ana-delete posts! Akadelete mara ya kwanza, lakini alipodhani anaweka sawa, akaharibu zaidi hadi TRA wakaweka in simplified form
TRA.png

😂😂
 
... atoke mwenye hotuba yake arekebishe badala ya wapambe kumsemea. Rais wa nchi hakosei alitutaarifu mwenyewe!
Hakuna suala la upambe hapa! Kama nilivyosema, nimekumbuka mjadala sawa na huu kule Twitter kuhusu haya manamba manamba hadi Gerson Msigwa akalazimika ku-delete post na kuweka nyingine! Alipoweka nyingine, akakosea zaidi hadi wenye namba zao, yaani TRA walipoweka sawa!!

TRA.png
 
Naona wewe ^uli-overlook,^ ila hukukosea! Hatari na nusu!
Hivi unaelewa maana ya ku-spin? Na kama unaelewa, unaweza kufafanua nime-spin vipi au nime-spin nini?!

Na kama unashindwa kuelewa sentensi "sikukosea" bali "nili-overlook" basi you've serious problem unless kama unahangaika ku-prove something in a very wrong way! Nasema you've a long way kwa sababu 14 000 Trillion na 14 Quadrillion ni kitu kile kile, sasa sijui tatizo lako lipo wapi hapo!!
 
Nilidhani sijasikia vyema ikabidi nimfuate kule tube kusikiliza Tena nikajirithisha kuwa masikio yangu ni mazima!
Huenda ni kweli BoT wanazo hizo dollar bilioni elfu sita. Basi walipe deni lote la taifa ili nchi isidaiwe Tena. Au mnasemaje ndugu zangu?
Kama hicho kiwango alichotaja hakipo basi huu ni mkwaju au bakora nyingine Tena tumechapwa nayo wananchi!
Hivi inawezekana kufanya editing kwenye hotuba iliyokwisha ruka hewani?
Nimshauri bi mkubwa kuwa, kabla ya kuisogelea mimbari yoyote asome alichokabidhiwa kwanza ajiridhishe vinginevyo Kuna siku atawekewa barua ya posa ya bintiye naye atatusomea Kama hotuba! Bi mkubwa ajiri waandishi na wanahabari wazalendo na watiifu kwako achana na hao waandishi michongo unaoletewa watakuangushia gari bovu!
Kwani msomaji mwenyewe hajui ukweli? Ukiandikiwa uongo na ukasoma uongo bila kuonyesha kushtukia ina maana wewe ni Rais usiyejua tuna akiba kiasi gani ya fedha za kigeni ni hatari sana

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom