Hii ndio mikoa ambayo Rais Samia amewekeza nguvu kubwa kuiletea maendeleo

Hii ndio mikoa ambayo Rais Samia amewekeza nguvu kubwa kuiletea maendeleo

Kumbe mnazungumzia Zanzibar? Endeleeni
Ya kuna Mwamba fulan hapo juu alisema kwamba raisi Samia miradi yote kaihamishia Zanzibar kana kwamba Zanzibar haina raisi.

So ndo nilitaka anioneshe prove ya kile alichosema au alichoandika.
 
Hatii saini yoyote anafanyia gizani tu maana anayafanya kihalifu
Toka Lowasa alivyochafuliwa mwaka 2008 na kusafishwa mwaka 2015, sina tena muda wa kuamini maneno ya vijiweni kama haya bila kuoneshwa fact.
 
Mbeya hawapendeki hao na ninwajuaji sio sehemu sahihi kimkakati sana sana anamsaidia Spika Tulia tuu maana bila huyo huo Mkoa wangeshautelekeza una watu jeuri wajuaji na wabishi wanaotaka Ligi mda wote ndio maana ujenzi wao ni hovyo hovyo Bora liende.

Kuna Mikoa ni ya CCM hakuna Cha Upinzani kama Ruvuma,Manyara,Tabora,Katavi,Rukwa,Njombe,Iringa, Morogoro,Pwani,Tanga ,Lake zone yote kasoro Mara.

Kiufupi Tanzania hakuna upinzani labda ccm wakosee kuchaguana
Umelewa ugoro wewe sio bure bralifakeni[emoji846]
 
Ya kuna Mwamba fulan hapo juu alisema kwamba raisi Samia miradi yote kaihamishia Zanzibar kana kwamba Zanzibar haina raisi.

So ndo nilitaka anioneshe prove ya kile alichosema au alichoandika.
Huyo ni mnafiki mwenye chuki na wazanzibar na waislamu mkuu achana naye.
Juhudi kubwa ya mama ipo katika mkoa iliyosahauliwa kwa maksudi na MARAIS waliopita kama vile Kigoma na mkoa ya kusini. Mama anaupiga mwingi hao wachumia tumbo achana nao.
 
Toka Lowasa alivyochafuliwa mwaka 2008 na kusafishwa mwaka 2015, sina tena muda wa kuamini maneno ya vijiweni kama haya bila kuoneshwa fact.
Fact moja inatosha tu kataba la kitapeli la bandari,nikiongezea na uuzwaji wa Ngorongoro kwa waarabu kwa kutaja machache tu
 
Huyo ni mnafiki mwenye chuki na wazanzibar na waislamu mkuu achana naye.
Juhudi kubwa ya mama ipo katika mkoa iliyosahauliwa kwa maksudi na MARAIS waliopita kama vile Kigoma na mkoa ya kusini. Mama anaupiga mwingi hao wachumia tumbo achana nao.
Basi nampa pole sana, sababu chuki yake haitamsaidia kitu. Apendapo Mungu Mama yupo ikulu hadi 2030.
 
Fact moja inatosha tu kataba la kitapeli la bandari,nikiongezea na uuzwaji wa Ngorongoro kwa waarabu kwa kutaja machache tu
Ukiona unaandika kitu bila support ya chawa, juwa unachoandika hakina maana.

Mimi nakuuliza fact wewe unaleta mipasho ya kwenye kanga. Mimi sio miongoni mwa watu wanaoshikiwa akili na wanasiasa uchwara.

Ukiniambia sijui bandari au ngorongoro imeuzwa bila kuweka ushahidi wa mauziano kupitia maandishi, au saini nakuona wewe ni hadija kopa unaetumia ID fake ili usijulikane kama wewe ni muimba mipasho.
 
Mbeya hawapendeki hao na ninwajuaji sio sehemu sahihi kimkakati sana sana anamsaidia Spika Tulia tuu maana bila huyo huo Mkoa wangeshautelekeza una watu jeuri wajuaji na wabishi wanaotaka Ligi mda wote ndio maana ujenzi wao ni hovyo hovyo Bora liende.

Kuna Mikoa ni ya CCM hakuna Cha Upinzani kama Ruvuma,Manyara,Tabora,Katavi,Rukwa,Njombe,Iringa, Morogoro,Pwani,Tanga ,Lake zone yote kasoro Mara.

Kiufupi Tanzania hakuna upinzani labda ccm wakosee kuchaguana
Huna akili wewe,rukwa ipi??mbeya ipi??wekeni tume huru kote huko muone ujinga wenu ulivyo
 
Bora nguvu kazi aelekezee Jiji la Mwanza, jiji pendwa, jiji la biashara na kuishi pia,, pamoja na Dom, Dar na Zanzibar nchi. Huko Kilimanjaro na arusha wasubiri kwanza.
Nimeshashuhudia chuki ya wazi ya watu wa kanda ya ziwa kwa watu wa kilimanjaro na arusha mnatamani hata tungepoteaga tusingekuwepo🤣🤣
 
Nimeshashuhudia chuki ya wazi ya watu wa kanda ya ziwa kwa watu wa kilimanjaro na arusha mnatamani hata tungepoteaga tusingekuwepo🤣🤣
Hapana mkuu, sina chuki hata kidogo, ila baadhi ya watu wa kaskazini hawana ustaarabu, wana wivu sana na ukatili juu.
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Wakuu.... wengi wetu hapa JF na nchini kwa ujumla, tunajua kwamba raisi wa JMT mh Samia S. Hassan anapambana usiku na mchana, ili kuhakikisha serikali yake inaleta maendeleo katika wilaya, mikoa na nchi yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lakini kama ilivyo desturi ya sisi binadamu unapokuwa na mambo, vitu au watu zaidi ya watatu ubavuni kwako, ni wazi kuwa hautoweza kubalance upendo wako kwao yani iwe mia kwa mia kwa kila mtu au kitu. Ni lazima mtu au kitu kimoja utakipenda zaidi ya kiingine.

Hili hutokea hata kwa mzazi mwenye watoto mfano wa5 hujikuta anampenda mtoto mmoja au wawili zaidi ya awapendavyo waliobaki, japo kama mzazi huwa haoneshi moja kwa moja upendeleo wake huo kutokana na kutaka wale wengine wasijisikie kubaguliwa nk.

Hivyo basi hata raisi wetu, ni raisi wa nchi nzima, lkn ukweli ni kwamba kuna baadhi ya mikoa ambayo amekuwa akionesha kuipenda na kuijali zaidi ya mikoa mingine, na hili limekuwa likionekana kupitia miradi mbali mbali kabambe aliyoielekeza katika mikoa hiyo hata kama anajaribu kutokuonesha kuwa ana baze zaidi huko, lkn wafuatiliaji tunaona wenyewe kwa macho yetu na kusikia pia kwa masikio yetu.

Mikoa hiyo ambayo inabahati mno na serikali hii ni 👇

1. Dodoma.
Mkoa huu pamoja na kwamba raisi aliekuwepo madarakani hayati John P. Magufuli aliupenda na kuelekeza zaidi macho yake huko, pia umeendelea kuneemeka na uongozi huu wa awamu ya 6 chini ya raisi Samia na kupelekea miradi mingi ya maendeleo kupelekwa huko.

Nafikiri haya yamesababishwa na hadhi yake kama mji wa serikali na makao makuu ya nchi.

2. Kigoma.
Mkoa wa Kigoma pia unazali na uongozi huu wa raisi Samia. Japo mkoa huu una kiongozi mmoja mkubwa wa chama cha upinzani, na historia yake ya baadhi ya vijana kushikiwa akili na kupenda kuunga mkono wapinzani mbali mbali, lkn raisi Samia hakujali hayo.

Ameelekeza nguvu na miradi katika mkoa huo kuliko kiongozi mungine yoyote aliewahi kutawala kabla yake. I hope hiyo miradi ikikamilika basi Kigoma itakuwa Small "Chicago", achilia mbali zile stori za mh Kikwete kwamba angeigeuza Kigoma kuwa Dubai kwa maneno tu matupu bila vitendo wala kutoa hela za miradi husika.

3. Mbeya.
Huu mkoa nao ni miongoni mwa mikoa inayofaidika kwa kasi kupitia uongozi huu wa awamu ya tano. Kabla ya hapo mkoa huo ni kama vile ulikuwa umesahaulika kimtindo, maana hata miundo mbinu ya mkoa huo kwa upande wa barabara, shule, hospital nk vilikuwa hovyo, ila toka raisi Samia aingie amekuwa akionesha kushirikiana na mbunge Mbeya mjini ambae pia ni spika wa bunge kuleta maendeleo ya kweli katika mkoa huo.

Kwa kuonesha kuwa anaupenda mkoa huo kwa vitendo, serikali ya raisi Samia tayari imeshatoa mamilioni ya miradi kwa ajili ya shule, barabara nk. Japo kuna baadhi ya watumishi wa serikali kutoka mkoa huo wanaonekana kutohitaji maendeleo katika mkoa huo kwa kutafuna mamilioni ya baadhi ya miradi kama alivyosema raisi Samia alipokuwa ziarani mkoani huko, lkn ni kama vile bado hajachoka kuendeleza miradi katika mkoa huo, bila kujali baadhi ya wapinzani ambao wao wanachotaka ni kuingia bungeni tu bila kujali maendeleo anayowaletea raisi Samia katika mkoa wao.

Baadhi ya wanasiasa wenye familia zao Ulaya na Marekani ambao kiasili hawatoki katika mkoa huo, wamekuwa wakiwahadaa vijana ambao wengi wao walikimbia shule mkoani hapo, wapinge miradi hiyo ya maendeleo ili uchaguzi mkuu utapofika wachaguliwe wao tu na vyama vyao.

4. Mwanza.
Mkoa wa Mwanza pia ni kama Dodoma. Ulikuwa na zali chini ya serikali ya awamu ya 5 ya hayati Magufuli, na bado umeendelea kuwa na bahati pia chini ya serikali hii ya awamu ya 6 ya raisi Samia.

5. Mtwara....

6. Lindi....

Kama kuna mikoa mingine ambayo imeneemeka na uongozi wa raisi Samia alaf sikuiandika basi ndugu msomaji unaweza kuiandika hapo chini....

Karibuni.
Mkoa wa Mwanza maendeleo gani aliyofanya mama Samia? Mfano miundombinu ya barabara ni mibovu kupindukia hasa ndani ya Wilaya ya Nyamagana
 
Kwa vile raisi Mwinyi katika kampeni za uchaguzi aliahidi kuleta maendeleo, na sasa kaamua kukamilisha ahadi yake kwa wapiga kura wake wewe ni nani mpaka uhoji maendeleo hayo mkuu?

Au ulitaka afanye kama kina Lisu, Mbowe na Zito waliokaa bungeni zaidi ya miaka kumi bila kuchimba hata visima katika majimbo yao?
Tatizo hela zinatoka Tanganyika kuendeleza nchi jirani ya Zanzibar.
 
Back
Top Bottom