Hii ndio mikoa ambayo Rais Samia amewekeza nguvu kubwa kuiletea maendeleo

Hii ndio mikoa ambayo Rais Samia amewekeza nguvu kubwa kuiletea maendeleo

Miradi ya maendeleo katika hiyo mikoa siyo zawadi, wala hisani, ni pesa zetu zinazotokana na kodi, na mikopo ambayo inalipiwa na Kodi zetu.

Kwahiyo wanainchi wataunga mkono chama kutokana na sera.
Kila chama cha siasa duniani kina sera nzuri. Tatizo linakuja katika utekelezaji wa sera zenyewe. Wakenya waliompigia kura Ruto kwa sera zake nzuri ndio hao hao walioandamana na kumtaka atoke kabla hata ya miaka miwili baada ya kugundua kuwa hatekelezi kile alichoahidi kwenye sera.

Hivyo kuona serikali inaendeleza sera ya miradi ya maendeleo katika mikoa mbali mbali ni jambo la kushukuru na kuiunga mkono. Maana kuna vyama vingine unaweza kuvichagua vikatafuna kodi yako na hiyo miradi ya maendeleo ukaisikia kwenye makaratasi tu. Kama mtu ameweza kubadilisha katiba ya chama chake kihuni ili atawale milele sasa hata akiingia madarakani akatafuna kodi yako yeye na genge lake utamfanya nini?
 
1) Kwenye kuchagua viongozi wa chama cha upinzani taifa.. Ni lazima mwenyekiti, makamu, katibu mkuu na viongozi wengine waandamizi watokee kaskazini.

2) Kwenye kuchagua sehemu ya kufanya maandamano ambayo yatasababisha vurugu, biashara za watu kufungwa, watu kupigwa, kujeruhiwa na wengine kupata ulemavu wa kudumu basi ni lazima iwe Mbeya au Songwe.

Yani mpaka leo 2024 watu wa Songwe na Mbeya wameshindwa kujua tu kama wanatumiwa na wanasiasa wa kaskazini kwa faida zao na familia zao. Haitotokea kuona maandamano ya aina hii yanapangwa kutokea Moshi hata siku 1. Sababu watu wa Moshi wanajitambua, hakuna atakaekuwa tayari kufunga biashara yake eti aende akaandamanishwe na Mbowe.
Nyinyi BAWACHA kongamano la mwisho ambalo mama kizimkazi alikuwepo lilifanyika wapi kweli? Dada
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Wakuu.... wengi wetu hapa JF na nchini kwa ujumla, tunajua kwamba raisi wa JMT mh Samia S. Hassan anapambana usiku na mchana, ili kuhakikisha serikali yake inaleta maendeleo katika wilaya, mikoa na nchi yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lakini kama ilivyo desturi ya sisi binadamu unapokuwa na mambo, vitu au watu zaidi ya watatu ubavuni kwako, ni wazi kuwa hautoweza kubalance upendo wako kwao yani iwe mia kwa mia kwa kila mtu au kitu. Ni lazima mtu au kitu kimoja utakipenda zaidi ya kiingine.

Hili hutokea hata kwa mzazi mwenye watoto mfano wa5 hujikuta anampenda mtoto mmoja au wawili zaidi ya awapendavyo waliobaki, japo kama mzazi huwa haoneshi moja kwa moja upendeleo wake huo kutokana na kutaka wale wengine wasijisikie kubaguliwa nk.

Hivyo basi hata raisi wetu, ni raisi wa nchi nzima, lkn ukweli ni kwamba kuna baadhi ya mikoa ambayo amekuwa akionesha kuipenda na kuijali zaidi ya mikoa mingine, na hili limekuwa likionekana kupitia miradi mbali mbali kabambe aliyoielekeza katika mikoa hiyo hata kama anajaribu kutokuonesha kuwa ana baze zaidi huko, lkn wafuatiliaji tunaona wenyewe kwa macho yetu na kusikia pia kwa masikio yetu.

Mikoa hiyo ambayo inabahati mno na serikali hii ni 👇

1. Dodoma.
Mkoa huu pamoja na kwamba raisi aliekuwepo madarakani hayati John P. Magufuli aliupenda na kuelekeza zaidi macho yake huko, pia umeendelea kuneemeka na uongozi huu wa awamu ya 6 chini ya raisi Samia na kupelekea miradi mingi ya maendeleo kupelekwa huko.

Nafikiri haya yamesababishwa na hadhi yake kama mji wa serikali na makao makuu ya nchi.

2. Kigoma.
Mkoa wa Kigoma pia unazali na uongozi huu wa raisi Samia. Japo mkoa huu una kiongozi mmoja mkubwa wa chama cha upinzani, na historia yake ya baadhi ya vijana kushikiwa akili na kupenda kuunga mkono wapinzani mbali mbali, lkn raisi Samia hakujali hayo.

Ameelekeza nguvu na miradi katika mkoa huo kuliko kiongozi mungine yoyote aliewahi kutawala kabla yake. I hope hiyo miradi ikikamilika basi Kigoma itakuwa Small "Chicago", achilia mbali zile stori za mh Kikwete kwamba angeigeuza Kigoma kuwa Dubai kwa maneno tu matupu bila vitendo wala kutoa hela za miradi husika.

3. Mbeya.
Huu mkoa nao ni miongoni mwa mikoa inayofaidika kwa kasi kupitia uongozi huu wa awamu ya tano. Kabla ya hapo mkoa huo ni kama vile ulikuwa umesahaulika kimtindo, maana hata miundo mbinu ya mkoa huo kwa upande wa barabara, shule, hospital nk vilikuwa hovyo, ila toka raisi Samia aingie amekuwa akionesha kushirikiana na mbunge Mbeya mjini ambae pia ni spika wa bunge kuleta maendeleo ya kweli katika mkoa huo.

Kwa kuonesha kuwa anaupenda mkoa huo kwa vitendo, serikali ya raisi Samia tayari imeshatoa mamilioni ya miradi kwa ajili ya shule, barabara nk. Japo kuna baadhi ya watumishi wa serikali kutoka mkoa huo wanaonekana kutohitaji maendeleo katika mkoa huo kwa kutafuna mamilioni ya baadhi ya miradi kama alivyosema raisi Samia alipokuwa ziarani mkoani huko, lkn ni kama vile bado hajachoka kuendeleza miradi katika mkoa huo, bila kujali baadhi ya wapinzani ambao wao wanachotaka ni kuingia bungeni tu bila kujali maendeleo anayowaletea raisi Samia katika mkoa wao.

Baadhi ya wanasiasa wenye familia zao Ulaya na Marekani ambao kiasili hawatoki katika mkoa huo, wamekuwa wakiwahadaa vijana ambao wengi wao walikimbia shule mkoani hapo, wapinge miradi hiyo ya maendeleo ili uchaguzi mkuu utapofika wachaguliwe wao tu na vyama vyao.



4. Mwanza.
Mkoa wa Mwanza pia ni kama Dodoma. Ulikuwa na zali chini ya serikali ya awamu ya 5 ya hayati Magufuli, na bado umeendelea kuwa na bahati pia chini ya serikali hii ya awamu ya 6 ya raisi Samia.

5. Mtwara....

6. Lindi....

Kama kuna mikoa mingine ambayo imeneemeka na uongozi wa raisi Samia alaf sikuiandika basi ndugu msomaji unaweza kuiandika hapo chini....

Karibuni.
Ungetaja hayo maendeleo au miradi aliyopeleka kwenye mikoa hiyo ni yapi/ipi?
 
Mbeya hawapendeki hao na ninwajuaji sio sehemu sahihi kimkakati sana sana anamsaidia Spika Tulia tuu maana bila huyo huo Mkoa wangeshautelekeza una watu jeuri wajuaji na wabishi wanaotaka Ligi mda wote ndio maana ujenzi wao ni hovyo hovyo Bora liende.

Kuna Mikoa ni ya CCM hakuna Cha Upinzani kama Ruvuma,Manyara,Tabora,Katavi,Rukwa,Njombe,Iringa, Morogoro,Pwani,Tanga ,Lake zone yote kasoro Mara.

Kiufupi Tanzania hakuna upinzani labda ccm wakosee kuchaguana
Ficha upumbavu wako,mbeya Sio Wabishi ila Wana akili.wasomi ni wengi usitake kulinganisha na takataka za kigoma, Rukwa,singida,songwe nk nk nk nk
 
Ni lini Mbowe ata andaa maandamano Moshi? Au anahofia hayatopata watu? Maana hakuna mtu wa Moshi atakaekuwa tayari kufunga duka lake eti akaandamanishwe na Mbowe ambae walimpa ubunge miaka 15, akawa anaishi zake Dar bila kuwasaidia chochote.
Sijui mumeo ni wa sehemu gani Moshi? tuonyeshe pale Hai kwenye shida ya maji? kama Mbowe alikuwa Dar muda wote kwanini mlifyeka green house yake au nayo alikuwa nayo Dar? dada jitafakari
 
Sijui mumeo ni wa sehemu gani Moshi? tuonyeshe pale Hai kwenye shida ya maji? kama Mbowe alikuwa Dar muda wote kwanini mlifyeka green house yake au nayo alikuwa nayo Dar? dada jitafakari
Hili ndo tatizo lenu kina mama. Yani comment zenu huwa hazijifichi. Pengine ni kwa sababu ya kuzoea kusikiliza taarab.
 
Ficha upumbavu wako,mbeya Sio Wabishi ila Wana akili.wasomi ni wengi usitake kulinganisha na takataka za kigoma, Rukwa,singida,songwe nk nk nk nk
Wangekuwa na akili wasingetumiwa kirahisi na wajanja wachache kutoka Moshi.

Nafasi kubwa kubwa za chama wanapeana watu wa Moshi na maeneo mengine ya Kaskazini. Halafu maandamano, fujo na unaharakati uchwara ndo vipangwe kufanyikia Mbeya.. Hiyo akili au matope? Kama Mbeya ni muhimu kwao kwanini hawajaipa hata Katibu mkuu wa chama? Au umuhimu wa Mbeya ni kuandamana na kupambana na serikali kwa faida ya wakuu wa chama ambao ni wa kaskazini?
 
Hii mada ya ajabu. Rais anaamua wapi apeleke maendeleo? Hakuna mipango ya taifa?

Serikali haiwi na sera! Vyama vya siasa ndivyo huwa na sera “wanazouza” kwa wananchi ili kupewa ridhaa ya kuongoza. Sera sio miradi. Ni miongozo kuhusu mikakati ya maendeleo, matumizi ya rasilimali na ustawi wa jamii.

Chama hakitekelezi sera zake. Serikali ya chama kilicho madarakani huandaa mipango na miradi kulingana na sera za chama hicho na kuipeleka bungeni. Bunge (la vyama vyote) hujadili na kupitisha, kukataa hata kubadili baadhi ya mapendekezo ya serikali. Bunge hutoa maamuzi yake kuhusu mapendekezo ya mipango na miradi ya maendeleo iliyowasilishwa na serikali.

Serikali inatekeleza maamuzi ya Bunge kwa kuzingatia katiba na sheria za nchi. (Maamuzi ya Bunge si sawa na sera za chama tawala. Kuna input ya vyama vingine pia). Huko Marekani jinsi serikali inavyofanikiwa kupitisha mapendekezo yake bungeni (legislative mandate) ni kigezo kikubwa na muhimu sana cha utendaji wa Rais. Ni mtihani kweli kweli.

HIYO ni kwa nchi MAKINI yenye utawala bora unaozingatia katiba, sheria na kanuni za demokrasia ya vyama vingi.
 
Back
Top Bottom