Hii ndio mikoa ambayo Rais Samia amewekeza nguvu kubwa kuiletea maendeleo

Umeshajijibu tayari kwamba anakamilisha maana yake hakuna mradi wa kutoka kwenye akilizake anaoufanya
 
Bado mapema mkuu, tulieni muda wenu wa kufaidi neema huenda unakuja.
 
Kwa vile raisi Mwinyi katika kampeni za uchaguzi aliahidi kuleta maendeleo, na sasa kaamua kukamilisha ahadi yake kwa wapiga kura wake wewe ni nani mpaka uhoji maendeleo hayo mkuu?

Au ulitaka afanye kama kina Lisu, Mbowe na Zito waliokaa bungeni zaidi ya miaka kumi bila kuchimba hata visima katika majimbo yao?
 

Kuna wimbo fulani wa mkongwe Bitchuka unasema "hasidi" hana sababu.

Ukiusikiliza vizuri ule wimbo na kusoma ulichoandika naamini utahisi kama vile alikuwa amekutungia wewe mkuu.

Endelea kujifanya hauoni vile ambavyo wengi tunaviona.
 
Hata Kigoma enzi za kina Kaburu ilikuwa hivyo hivyo lkn mwisho wa siku wakaja kugundua kama wanatumiwa tu kama daraja la kisiasa la wanasiasa uchwara fulani, huku kutumiwa huko kukitumiwa kama fimbo ya wao kukosa maendeleo.

Wakakaa chini na kupinga utumwa huo. Hivi leo mkoa huo unakuwa miongoni mwa mikoa inayopendwa na kupewa kipaumbele na serikali. Hivyo hata Mbeya kuna siku wale wanaotumia watagoma kutumiwa na wanasiasa uchwara, na kuwa miongoni mwa wafanya siasa safi kama mikoa mingine.
 
Naona maana ya kuhoji imekupita kando.... Nilichoandika ni taarifa kama thread inavyosema.
 
Wale wa Mangi wa Arusha na moshi waendelee kuzungusha mikono tu ,walikuwa ni mikoa ya awali kupata maendeleo makubwa baada ya Dar ila kwa kuumbatia ushetani wa CDM ni swala la muda tu hata lindi itawafikia kwa maendeleo
 
Asante mkuu kwa maelezo mazuri. Huyo jamaa ni adui wa maendeleo. Hivyo hata umueleze vipi bado ataendelea kupinga tu ili kuwaridhisha wanaomtuma ku comment tofauti hapa JF.
 
Ubarikiwe mkuu kwa maelezo yako yanayojitosheleza πŸ™
 
Wale wa Mangi wa Arusha na moshi waendelee kuzungusha mikono tu ,walikuwa ni mikoa ya awali kupata maendeleo makubwa baada ya Dar ila kwa kuumbatia ushetani wa CDM ni swala la muda tu hata lindi itawafikia kwa maendeleo
Aisee nimejikuta nacheka sana mkuu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Usitusemee sisi watu wa mwanza
 
Umeshajijibu tayari kwamba anakamilisha maana yake hakuna mradi wa kutoka kwenye akilizake anaoufanya
Nafikiri hata hilo jambo la kukamilisha pia linastahili pongezi. Vipi kama asingekamilisha na kuamua kutafuna hizo pesa za miradi.

Wakati Kikwetwe anaingia madarakani alimalizia yale yote yenye tija yalioachwa na mtangulizi wake, kisha na yeye kuanzisha ya kwake.

Alivyoingia Magufuli pia na yeye alikamilisha au kuzindua miradi iliyoachwa na mtangulizi wake likiwepo daraja la Kigamboni na baadhi ya barabara zingine ambazo zilikuwa hazijamaliziwa chini ya uongozi wa Kikwete. Baada ya hapo ndo akaanzisha miradi yake.

Hivyo na huyu kakamilisha miradi ya mtangulizi wake lkn pia kuna yake mfano ujenzi wa madarasa, hospital au zahanati nk.

Lkn pia bado ana muda madarakani hivyo hatujui mpaka 2025 atakuwa ameshaanzisha au kukamilisha miradi yake mingapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…