LGE2024 Hii ya Samia kupanga foleni kujiandikisha inafikirisha kidogo

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Nikujulishe kwamba mimi sipo upande wowote wa chama chochote. Sijaandika hapa kiupinzani bali kizalendo.

Umeongea mengi kuhusu CHADEMA, wapo hapa watasoma hoja yako.

Kama kumpisha barabarani ni suala la kiusalama nakubalia na wewe. Lakini pia ni ningeshauri kwamba kama ni usalama basi uwepo sehemu zote.. kumpanga hivyo foleni ya kujiandikisha usalama ukwapi? Kama ni maadui wanaweza kuwepo popote pale.

Angefika akaenda moja kwa moja kujiandikisha ingetosha kuhamasisha wana CCM wenzake kwenda kujiandikisha. Tunafahamu kwamba yeye ni kiongozi wa nchi, hizi kero za foleni sio size yake tuache kudanganyana.
Hiyo foleni ya kuzuga kwa mtu yotote mwenye akili timamu ataona ni kichekesho.

Iko hivi:
Ukisikia Rais Ameenda kufungua shamba la miti basi na yeye lazima atapanda mti

Ukisikia Rais Ameenda kufungua chumba cha Darasa lazima na yeye ataingia na atakaa kwenye meza au dawati

Yani lazima atafata utaratibu wa sehemu anayokwenda kufungua Hilo tukio

Sasa Kwa tukio la juzi ilitakiwa apange foleni,

Na pale usalama wake ni mkubwa Sana, kwanza Yule mdada wa mbele Yake ni mlinzi wake, hapo bado watu wa nyuma yake na pembeni

Kwa tukio la kuandikisha haikutakiwa watu wampishe ilitakiwa kuwa vile

Hayo ndio mambo ya inchi za demokrasia

Unakumbuka usajiri wa simu?

Hata magu alipanga folen kwenda Kwa wakala
 
ukishindwa kutumia akili "ubongoni kwako" unaweza ukawa unatumia vitu vingine kuufikirisha ubongo...mtu anaweza simama juu ya ugali aliousonga mwenyewe kabla ya kura. Yaani barabarani awasimamishe watu kwa mabunduki ili apite alafu kwenye kujiandikisha apange foleni???? huu usanii hata steve nyerere hawezi kuufanya...is more than utoto😛.. kwani miaka mingine huko nyuma ktk mazoeziya namna hii amewahi panga foleni au kaanzia mwaka huu?. Maigizo yao yanatuchosha mda mwengine...yanatupunguzia kiwango cha kuwafatilia ktk utendaji wao 😎
 
HIi imenishangaza yaani akili yangu imegoma kuelewa.

Yaani, mtu alikuwa anaelekea kujiandiandikisha kupiga kura, huko barabarani msafara wake umesababisha watu na magari kusimamishwa ili kuruhusu “mheshimiwa awahi” aendako (hili ni la ajabu pia lakini tumeshalizoea hakuna namna ya kulibadilisha kwa sasa)

Kilichonistaajabisha hadi kufikia kuandika huu uzi ni yeye baada ya kufika huko kwenye kujiandikisha eti akapanga foleni, yaani eti aliowakuta hawakumpisha.

Naona kama vile wananchi wamekosa adabu, iweje ushindwe kumpisha mheshimiwa apite mbele wakati huko barabarani watu wamempisha na kusababisha kuchelewa kwenye shughuli zao na wengine wagonjwa wamechelewa kufika hospitali kwa wakati kupata matibabu.

View attachment 3122399
Hapo sio barabarani ni eneo ambalo usalama wa taifa hawana shaka juu ya ulinzi wa Rais kwahiyo acha apange foleni maana kwahiyo picha wote walio mbele yake wanaonekana ni wazee
 
Iko hivi:
Ukisikia Rais Ameenda kufungua shamba la miti basi na yeye lazima atapanda mti

Ukisikia Rais Ameenda kufungua chumba cha Darasa lazima na yeye ataingia na atakaa kwenye meza au dawati

Yani lazima atafata utaratibu wa sehemu anayokwenda kufungua Hilo tukio

Sasa Kwa tukio la juzi ilitakiwa apange foleni,

Na pale usalama wake ni mkubwa Sana, kwanza Yule mdada wa mbele Yake ni mlinzi wake, hapo bado watu wa nyuma yake na pembeni

Kwa tukio la kuandikisha haikutakiwa watu wampishe ilitakiwa kuwa vile

Hayo ndio mambo ya inchi za demokrasia

Unakumbuka usajiri wa simu?

Hata magu alipanga folen kwenda Kwa wakala
Sawa Boss
 
Hapo sio barabarani ni eneo ambalo usalama wa taifa hawana shaka juu ya ulinzi wa Rais kwahiyo acha apange foleni maana kwahiyo picha wote walio mbele yake wanaonekana ni wazee
Basi sawaaa
 
Imepangwa iwe hivyo kwa ajili ya kutafuta KICK kwa wananchi wa Tanzania wasio na akili
 
Simkejeli maana yeye nadhani anafata miapango iliyowekwa. Niwashangaa walioshindwa kumpisha kwenye foleni
Apishwe kwani yeye sio binadamu? Kuna liwaziri limoja jinga wakati wa jk linafika kwenye ATM linasema mi ni waziri linawapita watu! Rubbish!
 
hahahahahaha, umasikini wa watanzania hutumika kuwarubuni na kuwafanya watumwa.

Njia pekee yakuonyesha ni kiongozi Bora ni kuhakikisha maisha yaunaowaongoza ni mepesi na wote wanayamudu, huduma za Afya bora na huduma rahisi affordable, mfumo wa elimu unakuwa Bora na affordable Kwa Kila raia.
 
Na watu wanampisha😀
Obama alikuwa anapanda treni Ili asiwasumbue watu hapa majinga yako airport watu sijui mwenge wameshaambiwa wapaki magari pembeni! Miafrika hovyo! Halafu mnataka maendeleo! Huyo waziri Mpuuzi wakati wa jk nisingempisha pangechimbika! Kwanza sisi wananchi ndio tumemwajiri halafu tunamwogopa! Hivi unaweza kumwogopa kijana wako wa kazi nyumbani???
 
HIi imenishangaza yaani akili yangu imegoma kuelewa.

Yaani, mtu alikuwa anaelekea kujiandiandikisha kupiga kura, huko barabarani msafara wake umesababisha watu na magari kusimamishwa ili kuruhusu “mheshimiwa awahi” aendako (hili ni la ajabu pia lakini tumeshalizoea hakuna namna ya kulibadilisha kwa sasa)

Kilichonistaajabisha hadi kufikia kuandika huu uzi ni yeye baada ya kufika huko kwenye kujiandikisha eti akapanga foleni, yaani eti aliowakuta hawakumpisha.

Naona kama vile wananchi wamekosa adabu, iweje ushindwe kumpisha mheshimiwa apite mbele wakati huko barabarani watu wamempisha na kusababisha kuchelewa kwenye shughuli zao na wengine wagonjwa wamechelewa kufika hospitali kwa wakati kupata matibabu.

View attachment 3122399
Nyerere alipishwa njiani na aliambatana na msururu wa magari japo ulikuwa mdogo lakini alipanga foleni kama anavyofanya Samia pichani hapo.

Nyerere alifikia hatua ya kucheza bao na wazee wa mitaani, pale ikulu utotoni palikuwa na mikate inauzwa enzi za awamu ya kwanza ya Mwalimu. Tulikuwa tukiifuata mida ya jioni tunakutana nae kwenye korido, halafu tukimuamkia anatuitikia kiungwana tu huku mikono akituwekea vichwani.

Misafara mirefu na wapambe kuwa wengi imekuja miaka ya kuanzia awamu ya tatu baada ya hatari ya rais kuwa karibu na watu kuongezeka.
 
Nikujulishe kwamba mimi sipo upande wowote wa chama chochote. Sijaandika hapa kiupinzani bali kizalendo.

Umeongea mengi kuhusu CHADEMA, wapo hapa watasoma hoja yako.

Kama kumpisha barabarani ni suala la kiusalama nakubalia na wewe. Lakini pia ni ningeshauri kwamba kama ni usalama basi uwepo sehemu zote.. kumpanga hivyo foleni ya kujiandikisha usalama ukwapi? Kama ni maadui wanaweza kuwepo popote pale.

Angefika akaenda moja kwa moja kujiandikisha ingetosha kuhamasisha wana CCM wenzake kwenda kujiandikisha. Tunafahamu kwamba yeye ni kiongozi wa nchi, hizi kero za foleni sio size yake tuache kudanganyana.
Hiyo foleni ya kuzuga kwa mtu yotote mwenye akili timamu ataona ni kichekesho.

Hiyo kuzuga ndio usalama wenyewe sasa .
Huko barabarani hawezi kuzuga kwa kuingiliana na magari ya mchongo lakini hapo kwenye foleni ni eneo salama sana kwa sababu ni mtaani kwake na ni makazi ya viongozi wakiwemo wastaafu wa usalama na viongozi waliotumikia chama chake na serikali.

Sasa huko barabarani kuna mpaka madereva walevi wasiojali ,wavuta bangi na kadhali na wote sio kwamba wanafanya kwa kumhujumu wengine inaweza kuwa ni ajali ya bahati mbaya kutokana na gari kumshinda Dereva au kuharibikia ghafla njiani .

Lakini faileni ya kujiandikisha yupo na ndugu zake hapo na marafiki na watu wa usalama wamejipanga pamoja.

Ni hamasa nzuri sana na ya mfano wa kuigwa .

Naipinga sana serikali ya CCM lakini Samia anajua kucheza na akili za watoto. Huyo ni mama Mjanja sana.
Watanganyika wakizubaa anatawala mpaka 2035 na anamwachia Mshendelwa kiti . Wakati huo akina Makondakta ,Mkulu chembani ,Februari, Nepi nanuye , na wengine watakua wamefyekellwa mbali kabisa hakuna mwenye jina tena.

Yajayo yanafurahisha.
Watanganyika wako bize na foleni ya Rais. 😂😂😂😂😂
 
Nyerere alipishwa njiani na aliambatana na msururu wa magari japo ulikuwa mdogo lakini alipanga foleni kama anavyofanya Samia pichani hapo.

Nyerere alifikia hatua ya kucheza bao na wazee wa mitaani, pale ikulu utotoni palikuwa na mikate inauzwa enzi za awamu ya kwanza ya Mwalimu. Tulikuwa tukiifuata mida ya jioni tunakutana nae kwenye korido, halafu tukimuamkia anatuitikia kiungwana tu huku mikono akituwekea vichwani.

Misafara mirefu na wapambe kuwa wengi imekuja miaka ya kuanzia awamu ya tatu baada ya hatari ya rais kuwa karibu na watu kuongezeka.
Umenikumbusha mbali sana
Watoto wadogo kama hawa wakina Tlaatlaah hawawawezi
Kujua haya mambo

Ova
 
Back
Top Bottom