Na ukifunga shule ukaenda likizo,unaporudi unaona shule na mazingira yake kama mapya kabisaa,yanakuvutia na kukupa hamasa ya kusoma..
Kwa sasa shule karibia zote wanawaza mitihani mitihani mitihani tu..ma group ya walimu wamebaki kutumiana mitihani ya kila mahali wakidhani ndiyo Elimu bora hiyo.
Ila nadhani shida imeletwa na wanafunzi wengi wasio na sifa ya kujiunga sekondari wako sekondari wanaigiza kusoma,na viongozi wanawatukana walimu kila kukicha kwa hao wanafunzi wasio na sifa wanapopata matokeo yao stahiki( kufeli).
Ila kwa kizazi kile cha mwanafunzi kujisomea mwenyewe kwa nguvu nyingi na msaada kidogo wa mwalimu,likizo zilifaa sana, ila kwa kizazi hiki cha mwalimu kutumia nguvu nyingi na nguvu kidogoo za mwanafunzi,kazi ipo.
Sent from my Infinix X650 using
JamiiForums mobile app