Historia na safari ya utumishi wa Generali Jacob John Mkunda

Historia na safari ya utumishi wa Generali Jacob John Mkunda

Sasa mavyeo yote haya inakuwaje amkimbie Tundu Lissu?
Tundu Lissu ni maji marefu sana yale. Nchi hii hakuna wa kusimama naye na kumshinda kwa haki. Ndo maana jiwe aliona atumie mbinu ambayo hata shetani alikaa zake pembeni, lakini bado aliishia kufeli pia😁

Ndani ya dakika chache tu anaweza kukufanya mwenyewe ujione takataka kabla hata umma haujatoa matokeo yake😁

Kama alivyosema jana bwana Robert Heriel Mtibeli kwamba mtu anayependa heshima yake hawezi kukubali kuwa mahakamani na Lissu kwani vyovyote iwavyo mwamba lazima awe upper hand, lazima aku outshine tu iwe unapenda au hupendi.
 
Ngoja nikusaidie kujibu maana umeshindwa kujibu swali.

Kutokuwepo kwa vita sio kigezo cha amani..

Unasemaje kuna amani kama balozi anapotea akiwa nyumbani kwake miezi 11 sasa hajulikani alipo?

Na sasa kuna balozi mwingine anashikiliwa mateka huku nyie mnapiga propaganda kuna amani huku mkizuia haki yake ya kikatiba ya kuzungumza na kujumuika .

Unasemaje kuna amani iwapo tangu 2016 kuna ripoti ya watetezi wa haki za binadamu kuna maelfu ya watanzania majina yao yako documented walipotea na hawajawahi kujulikana hadi leo walipo?

Amani sio ukosefu wa vita fikiria usitumie kichwa kama mkebe wa kuhifadhi meno.
Hivi shuleni siku hizi mnasoma ujinga na upuuzi. Kupotea kwa mtu sio kigezo cha kukosa amani kwenye nchi. Nenda kwake huyo unaesema yupo mateka kama utomkuta anakunywa chai yake na sambusa... Tatizo liko wapi. NCHI IPO SALAMA NA WANANCHI WAPO SALAMA. Labda unashindwa kutofautisha kati ya ukosefu wa amani nakuwepo crimes like abduction nk. Nchi hii hipo salama na watu wanaishi vizuri na kupiga kazi.
 
Tundu Lissu ni maji marefu sana yale. Nchi hii hakuna wa kusimama naye na kumshinda kwa haki. Ndo maana jiwe aliona atumie mbinu ambayo hata shetani alikaa zake pembeni, lakini bado aliishia kufeli pia😁

Ndani ya dakika chache tu anaweza kukufanya mwenyewe ujione takataka kabla hata umma haujatoa matokeo yake😁

Kama alivyosema jana bwana Robert Heriel Mtibeli kwamba mtu anayependa heshima yake hawezi kukubali kuwa mahakamani na Lissu kwani vyovyote iwavyo mwamba lazima awe upper hand, lazima aku outshine tu iwe unapenda au hupendi.
Sasa atakimbia mpaka lini? Bora tu aje amsikilize Lissu wapange jinsi atakavyomtetea. Lakini akienda nje ya utaratibu atakula konzi hatakuja kumsahau Lissu.
 
Elimu mbalimbali zinazoungana na kutengeneza degree na baadae zinatumika kama elimu. Shida ya hizi elimu ni kuwa, zikipata "heat and pressure" huwa zina tabia ya kukimbia kila elimu kivyake
šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚
 
Sasa atakimbia mpaka lini? Bora tu aje amsikilize Lissu wapange jinsi atakavyomtetea. Lakini akienda nje ya utaratibu atakula konzi hatakuja kumsahau Lissu.
Hapo ni ukisimama nchale, ukikaa nchale.

Akija kwa TAL ni aidha awe against TAL adhalilike na kubaki salama kwenye kiti chake huku akipoteza heshima hata kidogo iliyokuwa imesalia baada ya mo29, au alinde na kuiinua zaidi heshima yake kwa ku side na TAL kwenye haki ila baada ya hapo amfuate nchimbi.
 
Hivi shuleni siku hizi mnasoma ujinga na upuuzi. Kupotea kwa mtu sio kigezo cha kukosa amani kwenye nchi. Nenda kwake huyo unaesema yupo mateka kama utomkuta anakunywa chai yake na sambusa... Tatizo liko wapi. NCHI IPO SALAMA NA WANANCHI WAPO SALAMA. Labda unashindwa kutofautisha kati ya ukosefu wa amani nakuwepo crimes like abduction nk. Nchi hii hipo salama na watu wanaishi vizuri na kupiga kazi.
Una uhakika wananchi wako salama?? Au hao wanatekwa na kuuliwa mchana kweupe kwenu nyie ni wanyama?? Au mpaka ifike zamu yako ndugu??
 
Hivi shuleni siku hizi mnasoma ujinga na upuuzi. Kupotea kwa mtu sio kigezo cha kukosa amani kwenye nchi. Nenda kwake huyo unaesema yupo mateka kama utomkuta anakunywa chai yake na sambusa... Tatizo liko wapi. NCHI IPO SALAMA NA WANANCHI WAPO SALAMA. Labda unashindwa kutofautisha kati ya ukosefu wa amani nakuwepo crimes like abduction nk. Nchi hii hipo salama na watu wanaishi vizuri na kupiga kazi.

Hujajibu maswali hapo, balozi amepotea miezi 11 akiwa nyumbani kwake je yuko wapi?

Baada ya October 29 tuliambiwa na jaji Chande watu 700 walipotea hadi leo hawajulikani walipo?

Leo tunavyoongea kuna balozi tangu August 25 yuko mateka utasemaje kuna amani ?

Hao wananchi walio salama ni wale walioamua kuwa chawa na mazuzu kukubali kuburuzwa wanaopinga wanapotezwa na kukimbia nchi.
 
Huyu mpaka 2020 alikuwa kanali tu ndio maana unaona alikuwa kamanda kikosi, huwezi kuwa kamanda kikosi brigedia. Hakuwa brigedia 2020.
Ndo maana huwa nasema huyo jamaa ni kilaza.

Yaani kuanzia mwaka 1992 mpaka 2014 hakuwa na shahada ya chuo kikuu?

Kumbe kasoma elimu ya watu wazima ya chuo kikuu…..

Ningependa kuona transcripts zake kutoka hicho chuo alichosomea.

Yawezekana hicho chuo ni diploma mill.
Jeshini ukiwa msomi uwezi kupewa cheo, Wasomi wa chuo Kikuu wakiingia Jeshini mwisho wa cheo wanaishia Kanali, Ukiona Mwanajeshi ana cheo cha Brigedia huyo anakua Daktari.
 
Jenerali Jacob John Mkunda alizaliwa tarehe 2 Aprili mwaka 1968 katika Kijiji cha Chakwale, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro. Alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Kwaru iliyopo Wilaya ya Mbulu, Mkoa wa Manyara, Mwaka 1979 hadi 1985. Akajiunga na Elimu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Mavu mwaka 1986 hadi 1989 na Shule ya Sekondari Ndanda mwaka 1990 hadi 1992.

Baada ya kumaliza Elimu yake ya Sekondari Alijiunga na Elimu ya chuo kikuu katika Chuo Kikuu cha Mount Meru mwaka 2014 hadi 2017 na kutunukiwa shahada ya sanaa katika Utawala wa Umma na Usimamizi wa Rasilimali Watu.

Jenerali Jacob John Mkunda alijiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa "JKT" kwa mujibu wa sheria mwaka 1992 na ulijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania "JWTZ " Tarehe 1 Aprili mwaka 1993. Pia alihudhuria mafunzo ya Afisa Mwanafunzi na kutunukiwa kamisheni katika Chuo cha Monduli tarehe 25 Juni mwaka 1994.

Katika utumishi wake Jeshi Jenerali Jacob John Mkunda, Alipata nafasi ya kuhuduria mafunzo mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwemo:

Afisa Mwanafunzi Tanzania (1994), Kozi ya awali ya maafisa wa mzinga (1995), Gun Position Officers Course katika Shule ya Mzinga Tanzania (1998), Kozi ya utawala wa kikosi, Shule ya Mafunzo ya Huduma Pangani (2001), Field Artillery Company Commander nchini Marekani (2002), Regimental Survey Officers Course Tanzania (2003), Kozi ya Waangalizi wa Amani wa Umoja wa Mataifa Tanzania (2007), Kozi ya Makamanda na Unadhimu nchini Uganda (2008), Artillery Battalion Commander Course nchini Bangladesh (2010), Kozi ya Ulinzi wa Taifa nchini India (2016)

Jenerali Jacob John Mkunda Katika utumishi wake Jeshini umepandishwa vyeo mbalimbali kama ifuatavyo:

1. Luteni: Tarehe 5 - Oktoba 1995
2. Kapteni: Tarehe 21 - Januari 2001
3. Meja: Tarehe 3 - Novemba 2006
4. Luteni Kanali: Tarehe 19 - Machi 2010
5. Kanali: Tarehe 17 - Januari 2015
6. Brigedia Jenerali: Tarehe 30- Juni 2016
7. Meja Jenerali: Tarehe 2 - Julai 2020
8. Jenerali: Tarehe 29 - Juni 2022

Kutokana na kisomo chake Jenerali Jacob John Mkunda aliweza kushika Madaraka mbalimbali katika Jeshi letu la Ulinzi "JWTZ" ikiwemo:

1. Platoon Commander, Shule ya Mzinga (1993–2000)
2.Afisa Tawa 451 Regiment (2001–2006)
3. Battery Commander 451 Regiment (2006)
4. Mkufunzi, Shule ya Mzinga (2007–2009)
5. Kaimu Kamanda 977 Regiment (2009–2011)
6. Kamanda Kikosi 977 Regiment (2011–2018)
7. Kaimu Kamanda Brigedi 202 (2018–2020)
8. Kamanda Jeshi la Nchi Kavu (2020–2021)
9. Mkuu wa Tawi la Mafunzo na Utendaji Kivita, Makao Makuu ya Jeshi (2021–2022)
10. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania kuanzia tarehe 30 Juni 2022, Madaraka uliyonayo hadi sasa.

Jenerali Jacob John Mkunda Katika utumishi wake jeshini, Rais na Amiri Jeshi Mkuu alikutunuku nishani mbalimbali kama zifuatazo:

1. Nishani ya Miaka 40 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
2. Nishani ya Operesheni Demokrasia Comoro.
3. Nishani ya Miaka 50 ya Uhuru.
4. Nishani ya Miaka 50 ya Muungano.
5. Nishani ya Miaka 50 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
6. Nishani ya Miaka 60 ya Uhuru.
7. Nishani ya Utumishi Mrefu.
8. Nishani ya Utumishi Uliotukuka.
9. Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Nne.

Huyu ndio CDF wetu Jenerali Jacob John Mkunda..!!!
Elimu ya juu 2014! Yaani, shahada ameipata baada ya kuwa ameishaingia jeshini!? What a shame, chuo alichosoma mount Meru! Aibu tupu, na amezaliwa 68! Kwa nini hakuwekwa mtu aliyesoma UDSM, au, nje! Nendeni mkasome CV ya mtoto wa Museveni na wajukuu zake,?!
Huyu jamaa hakuna kitu, elimu yake ni ndogo Sana, inaelekea alikuwa "weak academically"
Mijitu kama hii huwa na chuki Sana na wasomi waliobobea
 
[/QUOTE
Aliekudanganya Nani mkuu!? Jeshini Wenye Elimu iliyonyooka na kubwa huwa mara nyingi ni watu wakawaida tu na utawakuta Ofisini
Kweli Mkuu Jeshini ukiingia umesoma utaishia mwisho kanali tu, Jeshi linataka uingie ukiwa na Elimu ya kidato cha sita, wao wanasema Ukiingia na Elimu ya chini unakua unalijua jeshi vizuri kwasababu unakua umeanzia chini tofauti na ukiingia na PHD unakua unaenda moja kwa moja monduli.
 
Elimu ya juu 2014! Yaani, shahada ameipata baada ya kuwa ameishaingia jeshini!?
Ndiyo - Haswaa. Elimu haina mwisho.
What a shame, chuo alichosoma mount Meru! Aibu tupu, na amezaliwa 68!
Kwani Mount Meru kina mapungufu gani broo.?
Kwa nini hakuwekwa mtu aliyesoma UDSM, au, nje!
Alitimiza vigezo. Kwani UDSM ina nini cha kipekee?
Nendeni mkasome CV ya mtoto wa Museveni na wajukuu zake,?!
Huko mbona ni Uganda na sio Tz? Kila mtu anapaswa ashinde mechi zake.
Huyu jamaa hakuna kitu, elimu yake ni ndogo Sana, inaelekea alikuwa "weak academically"
Wewe una nini? Tuambie kiwango cha Elimu yako na perfomance yako academically ulipokuwa masomoni.. Hapa sio kwamba namtetea bali naona waliomteua waliangalia mambo mengi (Vetting): sifa zake kielimu, kiutendaji - Utii, Uvumilivu, Weledi na Kumudu majukumu yake......... na yale ya ziada.
Mijitu kama hii huwa na chuki Sana na wasomi waliobobea
Thibitisha. Vinginevyo hiyo inaitwa ni Husda au Roho ya "Kwa nini".
Wahenga walisemaga; "Aliyekupa ww kiti ndiye aliyeninyima ukumbi"
 
Back
Top Bottom