Hivi inakuwaje mtu anajua kusoma Quran ila lugha ya kiarabu haijui?

Hivi inakuwaje mtu anajua kusoma Quran ila lugha ya kiarabu haijui?

Wanakaririshwa matamshi kwa kiswahili ukimtoa pembeni na alivyo kariri kwisha
Mfano unakariri hapa
Qul Huwa Allahu
 
Kuna jamaa ni mjuvi wa mambo mbalimbali na dini hiyo kaishika sana.
Siku moja nilimbishia kuwa kwa kusoma tu Quran au madrasa siamini kama kweli lugha ya kiarabu mnaweza kuimudu vyema.Jamaa alinibishia sana akasema kiarabu anakiweza tu kwani elimu aliyoipata kupitia dini inamwezesha!

Siku moja nilimtega gazeti kama ulivyowafanyia hao jamaa.Nilishangaa jibu lake,alidai mtindo wa uandishi uliotumika siyo mzuri hivyo haumuwezeshi kuyatambua maandishi yale!
Kweli kuna watu wabishi!
 
12 October 2022
ISLAMIC EDUCATION PANEL YATANGAZA MATOKEO
1665650183082.png


Mjumbe wa jopo la wataalam wa elimu ya kiislamu IEP Sheikh Mussa Yusuph Kundecha ametangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba wa elimu ya dini ya kiislamu uliofanyika septemba 14,2022 na kusema kuwa jumla ya shule 3710 katika mikoa 25 na halmashauri 151 zilishiriki kufanya mtihani huo.

Akizungumzia na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati wa kutangaza matokeo hayo,Sheikh Kundecha amesema kuwa jumla ya watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 163,143 na waliofanya mtihani ni 142,522 sawa na asilimia 87.36

Aidha ameendelea kusema kuwa idadi ya watahimiwa ambao hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali ni 20621.

Amesema idadi ya watahiniwa waliofaulu kwa kupataa daraja A hadi C ni 95,166 sawa na asilimia 66.77 ya watahiniwa wote 142522.

Aidha amesema idadi ya watahiniwa waliopata madaraja ya D na E ni 47,356 sawa na asilimia 33.23 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani.

“ndugu wanahabari idadi ya watahiniwa na madaraja yao ni kama ifuatavyo waliopata daraja la kwanza (A) ni wanafunzi 3,567,daraja la pili (B) ni wanafunzi 22,587,daraja la tatu (C)ni 69,012,daraja la nne (D)45,781 huku.daraja la mwisho (E) ikiwa ni 15,575″amesema mjumbe huyo wa IEP

Akizitaja shule 10 bora katika la shule zenye watahiniwa 20 na kuendelea, Sheikh Kundecha amezitaja kuwa ni Mumtaz (Mwanza),Istiqaama(Tabora),Rahma (Dodoma),Algebra Islamic(Dar es salaam),Dumila(Morogoro)Islamiya(Mwanza)Hedaru (Kilimanjaro),Daarul Arqaam(Dar es salaam),Mbagala Islami(Dar es salaam pamoja na Maarifa Islamic (Dar es salaam

Hata hivyo amesema kuwa shule 10 za mwisho zilizopata ufaulu mdogo kabisa ni pamoja na shule za msingi Kilimani (Ilala),Mwasenga(Kigoma Ujiji),Umoja (Tabora),Bugoyi (Shinyanga),Mvuti(Dar es salaam)Kasamwa(Geita),Muzdalifa Islamic(Lindi),Mawala (Kilimanjaro)Sipungu (Tabora)pamoja na Izumangabo (Geita)

Katika hatua nyingine Sheikh Kundecha ambaye pia ni mkuu wa baraza kuu la jumuiya na taasisi za kiislamu Tanzania amewaasa viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini,kuacha kujiingiza katika vitendo viovu,visivyompendeza mwenyezi Mungu.

Hatua hiyo ya Sheikh Kundecha imekuja kutokana na kuibuka kwa vitendo viovu ikiwemo ubakaji na ulawiti wa watoto vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa dini.


video courtesy of Mwanahalisi TV


Tovuti ya Islamic Education Panel : www.iep.ipc.or.tz
 
In recent years, the term Modern Standard Arabic (MSA) has come about. MSA is almost identical to the classical, formal Arabic of the Qur’an, with the exception of the addition of modern words and some differences in grammar constructions. MSA is the most common form of Arabic and is the variety taught in schools and colleges and is most commonly used in the workplace, in government and in the media.

Over the centuries of its existence, the Arabic language has adopted words from other languages including Hebrew, Aramaic, Persian, Greek, English and French. It has also influenced other languages as well including Turkish, Bengali, Hindi, Indonesian and Tagalog.
andika kiswahili wewe wewe kiumbe mchochezi!
 
Kwa hiyo tukubaliane kuwa;
1. kujua quran sio kujua kiarabu. hivyo
2. quran sio kiarabu.
Sasa hebu tuambieni quran imandikwa kwa lugha gani?
 
Quran ni maneno ya mwenyezi mungu ndio maana unaona matamshi yake yako tofauti kidogo


Halafu kwa hizi madrasa zetu za kibongo hawafundishi kiarabu kama kilivyo bali ni mwendo wa alifu badala ya ....
 
Wanapo wakaririsha watoto kule Madrasat wanatakiwa wawafundishe na grammar na syntax yake ili wawe wanaelewa wanacho kariri.

Mtoto anaimba qurani yote kwa kichwa ukimwuliza hapa panasema nini haelewi na ndio wanakua hivyo hivyo hadi wanakuwa Mashehe bila kuelewa nini kimeandikwa.

Ndio dini yenyewe hiyo. Dini ya kuriri sauti za kiarabu.
Waacheni na dini yao ya mchongo [emoji848]
 
Lugha ya mapepo ilitumika, unaweza kuikariri lakini wala huielewi.
 
na wapo hao waarabu wanaokaa uarabuni wamezariwa uarabuni wanaojua kiarabu na kukisoma kiarabu pia na hata kukiandika

lakini hawawezi kusoma QURANI

JE UNAJUA HILO
Apo umetupiga, Labda wasielewe nini kinazungumzia haswa ila kusoma kama kusoma wanaweza asee
 
Tatizo hujakutana na Ustadh kama unavyosema, Umekutana na mtu aliyejifunza kusoma na kutafsir Qur-an.
 
Wanakaririshwa kwa lazima huku wakila mboko..hapo hakuna kuelewa zaidi ya kukariri ili usilambwe bakora.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mfano ni huu:-

kwa kuruani kuhesabu wanaanza na arif(moja) ,be(mbili) ,te(tatu) ,se(nne) ila kwa kiarabu wanaanza na wahed(moja),khamsa(tano),thalatha(tatu) ,sasa kama wote ni waarabu mbona zinatofautiana? Means kuruani sio kiarabu.
 
Pale wana Deal na elimu Akhera jinsi utakavyo ishi kaburini mwako.

Ndo maana kuna tofauti kati ya Waarabu na waislam ml
Huo ni ujuha huo unaoufikiria.

Qur'an ni elimu ya maisha yako ya kila siku unayoishi.

Na Uislam ni mfumo kamili wa maisha Yqko. Ubora wa Uislam hauna mfano.
 
Wanakaririshwa kwa lazima huku wakila mboko..hapo hakuna kuelewa zaidi ya kukariri ili usilambwe bakora.

#MaendeleoHayanaChama
Kwa Tanzania hii ni shule ipi haikaririshi kwa mboko? Au mwenzetu ulisomea mwezini?
 
na wapo hao waarabu wanaokaa uarabuni wamezariwa uarabuni wanaojua kiarabu na kukisoma kiarabu pia na hata kukiandika

lakini hawawezi kusoma QURANI

JE UNAJUA HILO
Wewe upo Tanzania na Kiswahili ni lugha yako ya taifa na hujuwi kukitamka wala kukiandika ipqsavyo.

"Wamezariwa" ndio mdudu gani?
 
Wewe upo Tanzania na Kiswahili ni lugha yako ya taifa na hujuwi kukitamka wala kukiandika ipqsavyo.

"Wamezariwa" ndio mdudu gani?
Ungekuwa Libya na nchi nyingine za kiarabu, Waislamu wenzako wangekukamata, kukuuza kama mtumwa na kukufanya Malaya pamoja na Uislamu wako. Wee ni kama ngedere tu mbele ya Waarabu.
 
Back
Top Bottom