Hivi Kuna mtu amegonga miaka 30+ na hana mpenzi wala Mtoto?

Hivi Kuna mtu amegonga miaka 30+ na hana mpenzi wala Mtoto?

Unakuta mtu unakuwa na mahusiano mnaweka malengo mfano mko 26..mnakuwa wote miaka sita mfululizo Kisha dakika za mwisho mwenzio anabadili gia angani.hapo kwanini usijikute uko single over 30.
Na wengine pia changamoto za Maisha zinachangia
Na wengine pia changamoto za Maisha zinachangia Sister Abigail 2026.A.D
 
Leo dada naomba nipatie basi Binti Yako mMoja kam unae unajua napitia kipindi kigumu sana cha mahusiano, hata mdogo wako, mi wamenishinda nazinguana nao Kila nikipata
Mi binti yangu hawezi na hana uzoevu wa kukutoa kwenye kipindi kigumu cha mahusiano sijazaa kwa kazi hiyo..

binti zqngu wamefuata Slogan yangu pesa mbele mapenzi nyuma. utaweza?? au ndo stanza kujiita yatima wa mapenzi??
 
Hayo mambo hayana formula , what works for you might not work for another person.
Mr kweka na madam Urassa wapo kwenye 40+ je wanakimbizana na future za watoto wao?
Ni kweli,,

Sasa kweka na mkewe ji mifano michache mno katika jamii!! kweka na mkewe wasikufanye ushindwe kuoa au kuzaa na kutafuta mali.
 
Kuna swali ambalo katika jamii yetu linaonekana rahisi kuliko hesabu ya 1 + 1: “Umeoa?” Ukisema “bado” mtu anakutazama kama vile umeagiza gari lakini umesahau injini. Ukisema “nimeoa” swali linalofuata ni “Watoto wangapi?” Ukisema watatu anauliza “Wa kike yupo?” Ukisema wote ni wavulana, anakutazama kwa huruma kana kwamba wewe ndiye uliyekataa kusaini mkataba wa kupata mtoto wa kike. Na ukisema “Nafikiria talaka” ghafla kila mtu anageuka kuwa mshauri wa ndoa, mwanasheria, sheikh, mchungaji na profesa wa mahusiano - hata yule ambaye jana alikuwa anagombana na mwenza wake kwa sababu ya chumvi! Lakini nyuma ya swali hili la kuchekesha kuna swali kubwa sana ambalo watu wengi hawajawahi kujiuliza: Kwa nini tunadhani kuoa au kuolewa ni hatua inayomfanya mwanadamu awe kamili? Kwa nini mtu ambaye hajaoa huonekana kama bado hajafika, wakati mtu aliyeoa anaonekana kama amefika mwisho wa safari? Na kwa yule anayefikiria talaka, je amechoka na mwenza, amechoka na ndoa, au amechoka na picha aliyokuwa nayo kichwani kuhusu ndoa?

Kabla hatujaongea kuhusu ndoa, lazima turudi nyuma kuliko harusi, kuliko uchumba, kuliko mapenzi yenyewe. Turudi kwenye mwanadamu. Mwanadamu alikuwepo kabla hajawa mume au mke. Katika simulizi la dini ya Ibrahimu, Adam anaonekana kwanza kama mtu mmoja kabla ya kupewa mwenza. Hii inatufundisha jambo ambalo jamii wakati mwingine hulisahau: kuwa mtu si matokeo ya kuwa na mwenza. Utu wako haujaanza siku ulipovaa pete. Thamani yako haikuzaliwa siku uliposikia “ndiyo.” Na maisha yako hayakuwa draft mpaka mtu mwingine aje kusaini ukurasa wa mwisho. Kama hujaoa lakini una akili, vipaji, ndoto, imani, kazi, familia, uwezo wa kupenda na uwezo wa kujenga kitu duniani, ni sehemu gani hasa imekosekana? Na kama umeoa, je umeongezewa utu au umeongezewa mtu wa kushirikiana naye katika safari? Hapo ndipo tunapoanza kuona tofauti kati ya kutokuwa na mwenza na kutokuwa na thamani. Ni vitu viwili tofauti kabisa. Usipooa mapema usijione umechelewa; hata nyumba haijengwi kwa kuanza na pazia.

Lakini tatizo linaanza pale mtu anapoanza kuishi maisha ya kusubiri ndoa. “Nikishaoa nitaanza biashara.” “Nikiolewa nitakuwa na furaha.” “Nikishapata mume nitapata utulivu.” “Nikishapata mke mambo yangu yatafunguka.” Hapo ndoa imepewa jukumu ambalo haikupewa. Ndoa inaweza kukuletea mshirika, familia, fursa, changamoto, furaha na majukumu mapya, lakini haiwezi kukupa kusudi ambalo hukuwa nalo. Yesu kwa mfano, katika simulizi za dini hakufunga ndoa lakini hilo halikumzuia kutimiza kile alichokiona kuwa jukumu la maisha yake. Hii haimaanishi kila mtu anapaswa kuwa single; maana yake ni kwamba ndoa si tiketi pekee ya kufika kwenye maana ya maisha. Jiulize: Kama ungeambiwa leo kwamba hutaoa au kuolewa kwa miaka kumi ijayo, ungeendelea na ndoto zako au ungeweka maisha yote pause? Kama ungeweka kila kitu pause, huenda tatizo si kwamba hujampata mwenza; tatizo ni kwamba umempa mtu ambaye bado hajafika mamlaka juu ya maisha yako. Solution ni kuanza kuishi sasa. Jenga akili yako sasa. Jenga kazi yako sasa. Jenga tabia yako sasa. Tafuta kusudi lako sasa. Ukija kuoa, usimkaribishe mtu aje kuanza maisha yako; mkutane katika maisha ambayo tayari yana mwelekeo. Usiweke ndoto zako kwenye foleni ya ndoa; kwani ndoa nayo ina foleni zake.
Nimekuelewa sana kwenye hili bandiko lako....
 
Mi binti yangu hawezi na hana uzoevu wa kukutoa kwenye kipindi kigumu cha mahusiano sijazaa kwa kazi hiyo..

binti zqngu wamefuata Slogan yangu pesa mbele mapenzi nyuma. utaweza?? au ndo stanza kujiita yatima wa mapenzi??
Hayo sio mapenzi bali ni biashara,mapenzi ni hisia japo hela ni muhimu
Kwahiyo huyo Mwanume siku hela ikikata inabidi wamteme?
 
Hayo sio mapenzi bali ni biashara,mapenzi ni hisia japo hela ni muhimu
Kwahiyo huyo Mwanume siku hela ikikata inabidi wamteme?
Mwanaume akikosa pesa anatemwa vizuri tu!!!
lakini kabla ya kutemwa tunaangalia tabia zake akiwa na ukwasi zilikuwaje???
Kwa sababu mwanaume anaye onyesha tabia zake halisi ni mwanaume mwenye pesa tu!!!
mwanaume maskini asiye na pesa huwa ana fake tabia siku zote.
 
My dia kiuhalisia mama yao na kupenda kwangu pesa nakiri sijachezewa.
Hivyo basi watoto wangu hawatchezewa nimewapa nilishawapa code mungu akinipa uhai ntasimamia hilo.......
Usiwa amini sana nikupe mfano Kuna Binti katunzwa balaa mama yake akawa anajua mwanae bikra kitimbwi kimekuja baada ya kupata mimba, mama wa watu kapaniki balaa, wakamdaka jamaa mwenye mimba jamaa akasema hata yeye alivo piga mara ya kwanza Binti hakua bikra Ina mana alikua kesha chapwa muda tu mama hoii
 
Usiwa amini sana nikupe mfano Kuna Binti katunzwa balaa mama yake akawa anajua mwanae bikra kitimbwi kimekuja baada ya kupata mimba, mama wa watu kapaniki balaa, wakamdaka jamaa mwenye mimba jamaa akasema hata yeye alivo piga mara ya kwanza Binti hakua bikra Ina mana alikua kesha chapwa muda tu mama hoii
Hakuna sehemu niliyosema nawaamini!!! haipo
Nikwambie tu kwa mfano wako ni sahihi!!!
lakini kumbuka hapa duniani tunaishi tofauti tofauti sana.. mfano wa familia moja hauwezi kubeba mustakabali wa familia zote Tanzania.
 
Back
Top Bottom