Hivi kuna sehemu Tanzania bodaboda wanakimbia kama hawa wa Arusha?

Hivi kuna sehemu Tanzania bodaboda wanakimbia kama hawa wa Arusha?

Umeona pikipiki zenyewe kwanza,hazina side mirror na wengine wamevaa mayebo
Binafsi kama nna safari ya kupanda boda huwa nachagua kuanzia pikipiki mpaka appearance,
 
Bodaboda wa Arusha na Dar na kwingineko Tz...nendeni Bukoba mkajifunze kufuata Sheria...

Tazama hapa kwenye traffic lights...tazameni waanzilishi walivyo wastaarabu


NB. Usafiri wa bodaboda ulianzia Bukoba kwa Tanzania
Screenshot_20230310-132707.jpg
 
Arusha sio boda boda tuu hata hao wanaoemdesha magari wengi wao hawana fair na kutukana ni jadi yao awe mzee au kijana..Arusha ndio mji nimeshangaa unakuta machalii wanatukanana bara barani watu wanaona kawaida tuu na hakuna anaeshangaa wewe ukishangaa ndio wanakuita mang'aa...
 
uhusiano kati ya Kilimanjaro na Arusha ni Nini? ama hujui tofauti kati ya hiyo mikoa miwili Tz? We jamaa bhana
 
Arusha kitu wanachopenda kuprove ni kuwa hawana akili sawa sawa.

Katika kitu huwa kinanistaajabisha ni hicho. Yaani mtu ana hangaika kukuonyesha kwa maneno na vitendo namna ambavyo hana akili sawa sawa na anaona ni sifa muhimu ya kumfanya aonekane katika jamii.

Halafu si wanaume si wanawake si watoto si wazee wote idea zao zinakaribiana. Utasikia "Aiseee chalii yangu mimi ni mwehu mani kaulize sijui mawapi huko nilipo ngarambua kiyechuyechu"

Me huwa nawatazama natikisa kichwa nasepa.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
Akili yako sawa na ujazo wa kisoda! Una-generalize watu wa Arusha kwa mambo ya kishenzi, fanya tafiti kabla ya kuropoka
 
Arusha sio boda boda tuu hata hao wanaoemdesha magari wengi wao hawana fair na kutukana ni jadi yao awe mzee au kijana..Arusha ndio mji nimeshangaa unakuta machalii wanatukana bara barani kawaida tuu na hakuna anaeshangaa wewe ukishangaa ndio wanakuita mang'aa...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nimekulia Moshi Kilimanjaro, yeah kuna vijana wanakimbia na pikipiki mitaa ya Kalimani, kaloleni kule na njoro.
Nimekaa Dar kidogo yes kuna vijana wanajitahidi kukimbia na pikipiki

Ila Arusha hapana vijana kama hawana Roho na nyama, yaani pikipiki unasikia imepita kama mlio wa nyuki halafu sio mmoja sasa ni wengi karibia wote.

Kwa maeneo niliowahi kuishi hapa TZ sidhani kama kuna mkoa unao vunja rekedi ya vifo na ajali za bodaboda kuzidi Arusha.

Anzia kikatiti, usa,kilala mpaka ngara.
Hiyo mitaa wanapatikana vilema wengi wasio na miguu wa ajali za bodaboda
 
Back
Top Bottom