Nakumbuka kuwa niliambiwa watoto tulivyo kuwa wadogo tulikuwa na mfanano sawa karibu kwa kila kitu.
Kadri siku zinapozidi kwenda mbele kila mtoto ataonyesha tabia yake halisi kwa mzazi au mtu mdadisi ataweza kumtambua.
Miaka inavyokatika napo mtoto au watoto wale wale kila mmoja atakuwa na chaguo lake, tofauti na mwenzie hapo ndipo kila mmoja ataweka nguvu na jitihada kupata kile anachokiamni kuwa siku moja atakipata.
Ukumbuke wakati huo huo kila mtoto ana bahati yake na nyota yake kwenye kila kitu maishani mwake.
Sasa kwa umri huu nilionao siwezi mlaumu bibiye mbona Hana mtoto wala mume, sio kazi yangu ikiwa Nina mambo mengi nikiwa mdg nilitamani niyafanikishe na umri huu wa 20+ lakini sina hata moja.
Pengine hata yeye anatamani kuwa na mume au mtoto hatuwezi jua changamoto anazokumbana nazo, na sio mtu wa kuweka maisha yake hadharani.
Wakati mwingine angekuwa ndugu yako au rafiki akikuomba msaada labda sipati mtoto au kila mwanaume anayekuja kwangu anakimbia hapo unaweza mshauri au kumsaidia unavyo ona inafaa,
Ila kuamka na kumzungumzia mtu hivi mara vile aseeh ni kazi ya kutwanga maji kwenye kinu wanasema,
Tufanye lililo letu tuachane na maisha ya watu.