Hivi ni kwanini watu wengi wanaona aibu kuongeza chakula kwenye sherehe?

Kuna siku tupo kwenye sherehe tunakula biriani na pilau na mikukuz. Ikatangazwa anayetaka kuongeza chakula bado kipo. Bosi wangu akainuka mezani kurudi kwenye bufee kuongeza chakula. Niliona aibu bosi kaniabisha kwa kuongeza chakula. Suala la kuongeza chakula kwenye sherehe/hafla huwa si zuri sana kwa anayejiheshimu na kuheshimiwa utaonekana ni mfakamia vyakula na huwa huli vyakula hivyo nyumbani kwako. Unatakiwa uridhike na ushibe sahani moja tu tena usifike mwisho wa bufee na usijaze sahani utaaibika na kuonekana ni mlafi
 
Huyo boss wako si angekuomba hata wewe ukamchukulie mbona kajiaibisha kama ni mtu mzima sana,lakini mimi naona hii mambo ya kwenda na foleni pia haipo poa wangeweka utaratibu wa kumpitishia kila mtu mezani kwake
 
Wapi huko aisee?. Haki hujawahi kuhudhuria sherehe kanda ya ziwa wewe
 
Ukitaka kuzoa fedheha, nenda na empted stomach kwenye sherehe za watu.
Shiba kwako kwanza ndiyo uende.
Njaa njaa hizi hupoteza usmart wa mtu.
Tena vyakula vyenyewe wanga mtupu, ya nini bhana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…