Hivi ni kwanini watu wengi wanaona aibu kuongeza chakula kwenye sherehe?

Hivi ni kwanini watu wengi wanaona aibu kuongeza chakula kwenye sherehe?

Habari za wakati huu wana jukwaa, swali langu ni hilo hapo juu nimehudhuria sherehe kadhaa utakuta mtu amepakuliwa chakula kidogo amekula na hajashiba linapotolewa tangazo la wanaohitaji kurudia wakaongeze chakula kipo cha kutosha unaweza usione wanaoinuka, shida inakuwaga nini?
😆😆😆😆
 
Kuna siku nilienda kumuwakilisha bosi wangu kwenye kikao cha kazi cha wakuu wenzake. Wakati wa kula zikaletwa sahani tayari zimepakuliwa biriani na nusu kuku kila sahani. Tukaenda ziliko sahani kuchukua chakula, ile nachukua sahani tu mama mmoja bosi akanibadilishia sahani na kuniachia yake baada ya kuona sahani yangu ina kuku mkubwa kuliko wake. Nilikuwa mpole na mwenye nidhamu ya kula na wakuu wangu wa kazi ingawa kuna mabosi hawakuonesha nidhamu ya kula hasa kuchagua sahani zenye minofu mikubwa ya kuku
 
Hizi aibu zangu za kula shehereni zilinikosesha layer cream nikaishia kupata ukoko japo sikuula. Siku hizi sina aibu kula shereheni. Wakitangaza sasa ni wakati wa kula nawahi fasta mbele kuwahi vinono vingi vya mwanzo kabla ya wagawaji hawajapunguza mkono wa kugawa chakula. Wa mwishoni hupata kidogo au hukosa kabisa
 
Back
Top Bottom